Kweli uchawi upo.
Kijiji fulani huko mikoa ya nyanda za juu Kusini. Ni msimu wa uchaguzi. Kampeni kila siku kila mahali. Mshikemshike narudisha kadi nahamia upinzani mara narudisha kadi nahamia CCM.
Siku hiyo ni zamu ya upinzani kwenye moja ya vitongoji hapo kijijini. Mwenyekiti wa kitongoji ni CCM pure. Akawaambia CHADEMA kuwa sitaki upinzani kwenye kitongoji changu. Wakampuuza wakafunga mziki mnene wakitumia jenereta.
Matangazo yakaendelea, kelele mtindo mmoja.
Mara wingu hafifu angani. Hakuna aliyehofu maanake ni katikati ya kiangazi. Hakuna hata dalili ya manyunyu.Burudani kwa kwenda mbele.
Ghafla ilishuka radi kavu, ilikula kuanzia jenereta, spika, hadi mic zote.
Usiniulize kilichofuata. Ninashukuru Mungu hakuna aliyekufa wala kujeruhiwa.
Sent from my Infinix X688B using
JamiiForums mobile app