We kama sio illuminant basi unatumia nguvu za kiruminant ambazo zimekupofusha macho yako usitambue uwepo wa Mungu licha ya uwepo wa supernatural creatures.
Sasa inaonesha umepotea zaidi maana hata washilikina wanaamini kuna nguvu zaidi yao itokayo kwa Mungu.
Sio lazima leo uamini ila nakuombea siku ukipata mwanga wa kuona nuru ya uwepo wa Mungu basi mgeukie Mungu haraka isije ikafika siku ya kiama bado hujatubu dhambi zako.
Ufahamu wetu mdogo katika masuala ya roho ni sawa na falsafa ya Astria ya shimo iliyoelezwa Wayunani wa kale.
Ulielezwa hivi; wapo watu ambao maisha yao yote waliishi shimoni kwenye giza. Na kila watu walipopita nje vivuli vyao vilionekana ndani nao wakaamini vivuli vile ndio watu halisi hadi mmoja wao alipotoka nje na kuuona mwanga wa jua.
Lakini aliporudi shimoni kutokana na mwanga wa jua uliompiga usoni hakuweza kuona vizuri. Ndipo wenzie walipomwambia “sasa unaona huko nje sio kuzuri kwani huwezi kuona tena”.
Huyu Bwana akaamua kutoka mle shimoni na kuishi nje kwenye mwanga wa jua na kuacha wenzie wakiendelea na maisha ya shimoni ya kuamini vivuli kuwa watu.
Ninajaribu kukufananisha wewe na watu waishio shimoni wanaodhani dini wanazoamini na kuabudu ndio za kweli na wasioamini dini zao ni wapotevu.
Huu ni upofu na ujinga ambao hata ukitwangwa kwenye kinu hauwezi kumtoka mtu!
Niliwahi kuandika kuwa ujio wa dini hizi za mashariki ya kati yani Uislamu na Ukristo ulitokana na mchakato mzima wa ukoloni mkongwe ambao hatunabudi kupingana nao kwa nguvu zote.
Upo usemi wa kale usemao;’’Mwafrika anaenda kanisani au msikitini na msaafu kwapani lakini hawezi kusahau hirizi kiunoni.’’ Huu ni uthibitisho kuwa dini pepe hazijafua dafu mbele ya dini au imani za Kiafrika zilizoitwa ushenzi na washenzi hasa.
Tuna shuhudia viongozi wetu wa kisiasa wakikesha katika nyumba za ibada lakini kamwe hawawezi kuacha kwenda kwa sangoma kutizama upepo wa uchunguzi ujao.
Hivyo basi kunilazimisha kuamini Yehova ni mungu wa kweli nikutonitendea haki kifikra.
Sote tunapapasa kama kipofu aliegusa sikio la tembo na alipoulizwa unamjua tembo? Akasema; “ndio, tembo anafanana na beseni kubwa la kuogeshea watoto”.
Karl Max, muumini wa sosholojia alibainisha,’’dini ni ulevi, umlevya mtu kama bangi.’’ Nimelishuhudia hili pale Manzese darajani jijini Dar-es-salaam ambapo watu wana shindana kutetea dini ngeni barani Afrika kiasi cha kutokwa mapovu mdomoni mithili ya mgonjwa wa kifafa!
Dini ngeni imetumika sehemu nyingi duniani kudhoofisha jamii mbalimbali kisiasa, kiuchumi na kimahusiano.
Mwandishi Chinua Achebe anasema; “mtu mweupe ni mjanja sana, tazama aliingia kwetu, nasi tukampokea; amedhoofisha watu, hatuwezi tena kutenda kwa umoja wetu kwani hata imani zetu zimedhoofishwa”.
Haya niyasemayo yametokea nchini Ghana hivi karibuni baada ya Ghana kuwa pagumu kuingilika kwa lengo la kupora rasilimali hasa madini.
Marekani na maswahiba wao wakaamua kuanzisha madhehebu ya kilokole kila kona huku injili kuu ikiwa ni; “msihangaikie mali ya dini kwani thawabu yenu iko mbinguni ambako Yesu alienda kuandaa makao”.
Leo asilimia 90 ya vyombo vya habari nchini Ghana vinamilikiwa na madhehebu ya kiroho yenye asili ya Marekani.
Hapa ndipo kampuni ya kimataifa ya uchimbaji madini ya Barik inayomilikiwa kwa asilimia kubwa ya hisa na familia ya Rais George Walker Bush ilipoanza kuchota dhahabu hadi sasa wamehakikisha nchi ya Ghana imebaki mahandaki (sasa mapango).
Sasa Barki imehamia Tanzania sambamba na ujio wa kila aina ya kanisa inayoponya “mapepo” kwa jina la Kristo.
Hapa ndipo tunapojiuliza Ukristo wa kweli ni upi? Huu wa sasa au ule wa kihafidhina?
Ni ushahidi upi wa kitafiti unaoonyesha imani zetu za kiafrika ni ushenzi kiasi cha waamini wa hizi dini kudharau asili yao?