Miaka fulani nikiwa chuo nilienda field kijiji fulani huko Dodoma. Sehemu niliyokuwa nafanya field ilikuwa nje kidogo na sehemu yalipo maduka. Sasa siku moja nilikuwa napita njiani nikasikia watu wanaambiana "huyu kijana anapitaje hiyo njia usiku huu". Sikuelewa sababu ya wao kutokupita ile njia usiku
Sasa siku moja tukiwa watatu na jamaa zangu ninaofanya nao field, mida ya saa moja jioni kigiza giza ndio kinaingia. Tunawa tunavuka kuna sehemu kulikuwa na mto kwenye hiyo njia ila hauna maji. Sasa kwa mbele tukaomuona mzee mmoja aliyeonekana umri umeenda sana anatembea polepole kwenye ukingo wa pili wa mto, tulitegemea tukija kuibuka tutampita. Lakini tulipokuja kutokea hatukuona chochote.
Mwanzoni nilidhani nimeona peke yangu nikakaa kimya. Baadae tukiwa tumeshafika yule mshikaji nae akaniuliza kama niliona lile tukio. Mshikaji wetu mmoja yeye hakuona alikuwa yuko bizzy kuchati na simu muda tukio linatokea.
Tulishangaa sana maana ile sehemu haikuwa na mti wala kichaka cha kujificha ni eneo plain tu. Na ilikuwa ni kitendo cha sekunde chache sana, yule mtu kutokomea kabisa asionekane, hata ingekuwa gari ni lazima tungeikuta.
Sasa uniambie ilikuwa ni hallucination uone kama sijakuzabua makofi.