Kituko kingine Wizara ya Afya, Waziri abariki uteuzi wa AMO kuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu

Kituko kingine Wizara ya Afya, Waziri abariki uteuzi wa AMO kuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu

Mkuu Mwita Maranya,..hatusemi sisi "binafsi" bali ni utaratibu na hivyo hilo ndilo nadhani lililojadiliwa sana hapa!Yaani he should have a Bachelor of MD, na MPH, 7yrs experience..Na kama ndivyo equating ya Diploma ni sawa na MD,..inakuwaje AMO mwenye EXPERIENCE bado arudi shule tena ili awe MD, If masomo, na cheti kina usawa??

Ukweli ni kwamba, AMOs na MDs kuna UTOFAUTI(ambao watu wameshachangia kabla) lakini kiutendaji wanategemeana!

Pili inategemea katika sera na utaratibu wenyewe, kwamba katika level gani anakuwepo nani, wangapi, wakitoa huduma kwa watu wangapi na chini ya usimamizi wa nani..Hii huanzia katika Dispensary(Zahanati), Health Centre/Kituo cha Afya, Hospitali(Wilaya, Teule, Mkoa, Rufaa, Taifa).

Binafsi nadhani, kuna udhaifu uliopo katika sekta ya Afya, ikiwa ni utofauti wa wazi kati ya MDs na AMOs.(ingawa si sehemu zote)..mfano(mkuu japo nilisoma Ufundi Civil Engineering sijui katika taaluma yenu huko ukoje)..tulikuwa tunafundishwa(shuleni) "HIVI NDIYO INAPASWA" na si kwanini tunapaswa kufanya hivyo...yaani unaweza
ukakuta watu wanabishana the mason v/s foreman..na hii ndiyo hasa tatizo huku kwenye sekta yetu ya Afya...wengine kufanya kwa mazoea na wengine kuhitaji utaratibu ufuatwe!
hippocratessocrates Nadhani naelekea kukuelewa isipokuwa bado kidogo tu hapo kwenye elimu.
AMOs wanahold Ordinary Diploma ama ni Advanced Diploma? kwakuwa hizo ni ngazi mbili za kitaaluma zilizo tofauti. Mtu mwenye Ordinary Diploma akitaka kujiendeleza kitaaluma anaweza kusoma Bachelor ama ADvanced Diploma ambazo ni level za juu yake kielimu.

Katika mjadala huu tangu mwanzo imetajwa kwamba RMO mteule wa Simiyu ana Advanced Diploma, lakini kwa maelezo yako hapo juu ni kama vile unasema RMO mteule ana ordinary diploma. Hapo ndipo ningependa kupata ufafanuzi wako ili nikuelewe vizuri.
 
Last edited by a moderator:
Radii Mambo mengine ni wivu na choko choko ambazo hazina msingi wowote. Hawa AMO ndio wamejaa katika Hospitali nyingi na ndio wanaotoa tiba kwa sehemu kubwa ya Watanzania. Hawa AMO wamekuwa wakishika nafasi za DMOs ambayo haina tofauti na RMOs. Hii si nafasi ya utabibu ni nafasi ya Utawala ambayo hata Nesi, Afisa Afya au hata Katibu wa Afya anaweza akashika. Mkoa wa Tanga ulikuwa chini ya Afisa Afya akishika nafasi ya RMO kwa muda mrefu sana.

Sawasawa , Mi nashangaa huo ni wivu uliopitiliza, mtoa mada lazima hii nafasi unaitaka wewe au ndugu yako sasa mmekosha ndio mmemaindi. sasa huyu anahatarisha vip maisha ya wana Simiyu? umesikia yeye ndio anaatend wagonjwa? yeye ni mtawala zaidi. acha majungu wewe. ingekuwa wewe una hizo qualification na umeteuliwa ungekataa?
 
Mwita Maranya, Niwie radhi mkuu, Assistant Medical Officer(AMO) anakuwa awarded Advanced Diploma in Clinical Medicine...hivyo ni Advanced Dip. na siyo Ordinary Dip.
 
Last edited by a moderator:
meningitis,
Kama hutojali unaweza kutoa ufafanuzi wa hii qualification ya RMO ya kwamba;

The RMO shall be a graduate in Medical/Dental from a government-recognized
university with a postgraduate qualification in Public Health and training in
leadership and management.

Kwenye RHO na RNO imekuwa very clear kwamba lazima mtu huyo awe na University Degree au Advanced Diploma. Lakini kwa hii ya RMO imetajwa kwamba awe ni "graduate". Nini kimejificha hapa kwenye graduate?
 
Last edited by a moderator:
Ni bora huyu kuliko hao mnaofikiria wanafaa maana hao wasomi wameprove zero upstairs.

Makosa mwawili hayahalishi moja kuwa sahihi. RMO ni cheo kikubwa sana kwa upande wa afya, huwezi ukaweka mtu mwenye CV kama hiyo wakati tuna MD wengi tu.
 
Katika hali inayoendelea kuonesha uozo ulipo katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Waziri wa Afya, Katibu Mkuu na Mganga Mkuu wa Serikali wamehusika katika kumteua Daktari Msaidizi/ Assistant Medical Officer (AMO) kutoka Singida kushika wadhifa wa Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO katika Mkoa mpya wa Simiyu. Uteuzi huu umekiuka miongozo inayosema kuwa Mganga Mkuu wa Mkuu natakiwa kuwa Daktari kamili yaani Medical Doctor mwenye shahada ya kwanza ya Udaktari wa Bidanamu na siyo Advance Diploma. Kwa mantiki hiyo Waziri na Timu yake wanachezea Maisha yawana Simuyu kwa kupelekuwa Daktari wa Mkoa ambaye hana sifa hii ni hatari kwa wananchi wa Mkoa wa Simuyu

=================

The Regional Medical Officer The RMO is the equivalent of to the Director, Regional Health Services, who is the team leader and the overall in charge of coordinating the RHMT as a team, linking vertically to the Regional Administrative Secretary and horizontally with other departmental heads within the Regional Secretariat. The RMO is responsible and accountable to the RAS on a day to day basis on administrative and technical issues and is responsible and accountable on professional / technical issues to the Chief Medical Officer of the MOHSW.

Qualification The RMO shall be a graduate in Medical/Dental from a government-recognized university with a postgraduate qualification in Public Health and training in leadership and management. The RMO shall have at least 7 years working experience in district work in a similar position.
Mytake
1. Waziri wa Afya na timu yake wamewazarau wakazi wa mkoa wa Simuyu kwa kuwateulia Mtu ambaye hana sifa kushika nafasi ya Mganga mkuu wa Mkoa

2. Waziri wa afya na Timu yake amewazarau Medical Doctor wote Tanzania wenye sifa ya kushika wadhifa huo na hasa amewadharau Waganga wakuu wa Halmashauri waliopo katika Mkoa wa Simuyu ambao wanasifa za kutosha na kuliko Bosi mteule wa wawaziri na CMO

3 Waziri na timu yake wanamtengenezea mazingira magumu AMO huyo aliyeteuliwa kushika wadhifa wa RMO kwani hataweza kuwasimamia Madaktari ambao wanamdhidi sifa na kisomo na hasa madaktari bingwa katika mkoa huo

4. Jumuia ya Madaktari Tanzania kwasasa inafanya mawasiliano na MoHSW kutengua uteuzi huo na kama wakigoma MDs wote Tanzania wataingia katika Mgogoro na Serikali 5. Huu ni upuuzi mwingine wa wizara ya Afya na OWM TAMISEMI

5. Uteuzi huu unabaraka za JK kama ulivyo uteuzi wa Majaji

6. Waziri aombe radhi kwa MDs wote Tanzania kwa dharau aliyowaonesha

==============================

chuki nyingine sio issue nafikiri una chuki na huyu bwana, kwani elimu ulionesha hukusema kama ana masters yoyote na mimi nilisoma naye masters. huna uhakika na history yake umesikia sana maneno ya watu
 
CCM wanavuruga vuruga vuruga utaratibu as wao wakiumwa wanaenda apollo health city,so wanajua wao na familia zao hawawezi kukutana na hao magumashi

hiyo apollo nurse tu ana bachelor of science in nursing sio kama nadanganya ( nimefika nikaona na muulize yeyote aliefika) huko hakuna siasa unacheza na specialist tu CV za kufa mtu.. Tena apollo walichofanya ukiingia. Reception tu ya hospital kuna list za ma dr wote waliopo na CV zao zipo kwenye notice board imechongwa kama jiwe la uzinduzi watu wapo nondo kweli kweli unakuta undergraduate india then masters,phd etc ni UK na USA na practical za kufa mtu,,, Halafu bongo wanatuwekea magumashi.. Dah bora hii nchi wauze kila mtu apewe chake
 
Mwita Maranya, Niwie radhi mkuu, Assistant Medical Officer(AMO) anakuwa awarded Advanced Diploma in Clinical Medicine...hivyo ni Advanced Dip. na siyo Ordinary Dip.

Mkuu nimekuelewa, nadhani siasa ndio zimewavuruga zaidi kuliko uhalisia. Na kutoaka na hali hiyo mmejikuta mnabaguana na kudharauliana wakati ukweli wa mambo ni kwamba wote mnahitajiana na kutegemeana. Katika kada nyingine hizo siasa za Advanced Diploma Vs Bachelors zilishazikwa siku nyingi na watu wanachapa kazi vizuri.
 
Wapendwa ma great thinkers, ni nani aliyewaloga? Mmeanzia kwenye hoja mnaishia kutukanana? Hoja iliyoletwa ni ya msingi sana jamani. Hebu na tuache ushabiki, kebehi na matusi. Tujadili hoja na wayforward, ili Kama kuna haja ya kufanya reform kwenye hii secta muhimu, basi na ifanyike. So far tuangalie yafuatayo:
1. Je taratibu zimekiukwa au la? Kuna Mjumbe kwenye post za nyuma ametupia doc ya wizara ikionesha utaratibu ukionesha cheo husika na qualifications zake. Hivyo sioni kwani ni tuendelee kubishania Hilo.
2. Aliyeteuliwa je sifa anazo? Kwa mujibu wa policy ya recruitment husika?
3. Ni kwanini ma dokta wa ukweli hawaendi huko ndani ndani wakipangiwa (tuishie level ya district), je ni maslahi duni? Je nini kifanyike kuboresha hilo?
3. Hamuoni kuna haja ya kufanya reform ya ukweli kwenye hii wizara nyeti bila kudumbukizana vidole machoni.
3. Nina Hakika ma dokta wakiweka madudu yote yaliyofanyika huko na hawa madokta wasaidizi, basi JF hapatatosha. Hilo la kichwa na mguu ni chamtoto.

Mwisho, tusikuhukumiane kwa past issues, yaliyopita si ndwele tugange yajayo. MD na AMO ni ndg ktk kazi, hata sisi wachangiaji hatujui yakikukuta ni nani ataokoa uhai wako au wa ndg yako, maana likizo tunaenda vijijini, au safari zingine za kawaida.

Only that structure iangaliwe upya na iboreshwe. Hata sisi tusio na maprofession makubwa Wakati mwingine tunakosea, only when that happens we see it as a challenge, we take it for better future and a source of improvement.

God bless u all.
Queen Esther
 
Ninachokiona hapa ni muendelezo wa siasa tu katika taaluma, hali kama hii ilipata kuwepo siku za nyuma kwenye taaluma ya uhandisi, ambapo kulikuwa na ubaguzi wa hali ya juu sana kwa wahandisi wenye advanced diploma lakini baade mambo yalikuja kuwekwa sawa, na baada ya kuanza kutolewa kwa shahada ya uhandisi (Bachelor of Engineering) ya miaka mitatu ndipo mzizi wa fitna umekatwa kabisa. Mara nyingi kinachogombewa ni majina tu lakini kitaalamu unakuta wote wanafanya kazi zile zile.

Kwa mtazamo wangu huu ugomvi wa MDs dhidi ya AMOs ukiachwa uendelee bila kupatiwa ufumbuzi itakuwa ni hatari kwa ustawi na maendeleo ya sekta ya afya nchini, na bahati nzuri watanzania wengi tunapenda misifa na utukufu, na zaidi ya yote tunaamini zaidi katika majina ya vyeti kuliko utendaji kazi kwa uhalisia wake.
Kihalisia hata wagonjwa wanawazidi hao MD kujitibu.
Ugonjwa mdogo hata mkubwa vipimo malaki, matibabu millioni. Mtu anaachana nao anaenda duka la dawa ananunua dawa ya 2,000/- anapona.
Wale wa magonjwa sugu ma MD wanawanyonya kama kupe wakiwamaliza damu wanawaacha wajifie kwa taaluma badala ya uhalisia.
 
Makene ndg yangu, matibabu ni ghali duniani kote, Ndio maana ni vizuri ujiunge na social security Mifuko Kama NHIF ni vizuri. Ku meet medical expenses ni vizuri ukawa na insurance. Pia NSSF Wana SHIBU.
Pitia website za NSSF na NHIF uone namna unavyoweza kusaidika. Pia kuna private insurance Kama wewe ni mtu wa kipato cha Kati au cha juu. Wale wa kipato cha chini au kawaida weande NHIF, hata Mimi niko huko huduma sio mbaya sana, ila Agakhan hawatutaki.

Bless u.
Queen Esther
 
Arifu usichanganye mambo hapa, inawezekana huku kwenye kada ya uhandisi hupafahamu vizuri. Post yangu ya mwanzo kwenye thread hii nimeelezea lakini nitarudia tena kwa faida yako na wengine wa aina yako.

Mtu mwenye Advanced Diploma in Engineering ni Mhandisi sawa na Mtu mwenye Bachelor of Science in Engineering au Mtu mwenye Bachelor of Engineering.

FTC ni kada ya chini kwa Engineer, kwahiyo usijichanganye na kuilinganisha na Advanced Diploma. Kwenye engineering tunao wahandisi wa wilaya na mikoa ambao wana Advanced Diploma na wanafanya kazi bila bugudha kutoka kwa wenzao wenye Bachelor degrees. Huko kwenye afya sijui mnasumbuliwa na nini!?

Kitu ambacho niliwauliza na ambacho bado hamjakiweka sawa ni kwanini kwenye sekta yenu ya Afya ma MDs mnajiona bora kuliko ma AMOs?

H
izi kelele tunazoziona hapa mnajenga hoja kwamba AMO kateuliwa kuwa RMO ni kinyume na utaratibu kwa kuwa hana sifa za kielimu, mnataka kutuambia kwamba Advanced Diploma is nothing katika sekta ya afya!!??

Kumbe hujui halafu unajibishia tu.
AMO hawezi kuwa sawa na MD, kwa vile AMO anahitaji kula shule 5yrs, na Mmoja wa Internship ili awe sawa na MD.
Amo ni mtu mwenye diploma, alienda mafunzo maalum ya miaka miwili ya upasuaji hasa, na internal medicine kidogo, na hiyo kada yao kwa vile ilianzishwa km crash program, kufidia pengo la MD, kamwe hawawezi kuwa sawa na MD, hakuna EQUIVALENCY WALA EQUALITY HAPO ewe mtu.
Amo hawezi kuwa specialist, hd akafanye MD kwanza.
Mi nimechoka kukuelimisha bwana, km hutaelewa na hapa.
Km ni ugumu wa kichwa, huu umezidi.
 
Niongezee, kwenye academic qualifications za kuingia chuo kuanza MD, AMO ni sawa na fomu 6 fresh aliyefaulu vema, hivyo AMO ni Equivalent qualification ya kusoma MD, na baadhi ya vyuo vyenye akili hudahili fresh fomu 6 kwanza, nafasi zikibaki, ndo hufikiriwa AMO/CO.
Wakati MD ana Degree of Doctor of Medicine(MbChB-Bachelor of Medicine and Bachelor of Surgery), AMO hana degree hata moja, na wakitoka nje ya nchi, AMO atatambuliwa kwa Diploma yake tu.
Na u RMO unataka Academic Qualification ya u MD, na sio Skills za u AMO, kabla ya kuongezea sifa nyingne.
 
Kihalisia hata wagonjwa wanawazidi hao MD kujitibu.
Ugonjwa mdogo hata mkubwa vipimo malaki, matibabu millioni. Mtu anaachana nao anaenda duka la dawa ananunua dawa ya 2,000/- anapona.
Wale wa magonjwa sugu ma MD wanawanyonya kama kupe wakiwamaliza damu wanawaacha wajifie kwa taaluma badala ya uhalisia.

Thibitisha usemayo mkuu.
 
Thibitisha usemayo mkuu.

Bora umemtaka athibitishe. Wanakoelekea hawa wa namna hii, watasema MD ifutwe, wabaki AMO na CO tu.
Sijui tutaelekea wp baada ya hapo, hosp bila registrars, bila specialists, matibabu bila proper history taking, physical exam, investigation, hosp zitageuka mahali pa ramli au pa waganga wa kienyeji, na theatre zitageuka bucha tu, kwani wanachojua wale jamaa ni kukata na kupasua tu, bila hata indications za kufanya hivyo. Kuna wilaya nilipita, nikakuta rate ya Ceasarean Section(upasuaji wa kutoa mtoto) ni 32%, wkt ya kitaifa ni 15% na WHO recomended ni 10%.
Wao wakiitwa tu na nesi kuona mama mwenye tatizo la kujifungu, bila kujali kuwa maternal na fetal well being ni nzuri na kuna manouver nyingne za kumsaidia mama kuzaa kulingana na tatizo lake.
Wanachojali wao ni sifa ya kupasua tu, na kwa vile wabongo wanakariri anaepasua tu ndiye daktari, wanawapa sifa za kijinga, bila kujua kuwa kupasuliwa bila indication kunampa mtu ulemavu usio na sababu.
Shauri yao wasioelewa, tuwaache waangamie kwa kukosa maarifa.
 
Ninanukuu msemo wa mbunge wa Iringa "haya ndiyo mambo yakuruhusu akili ndogo kutawala akili kubwa" mwisho wa nukuu. kwa kuliruhusu hilo na wenye akili ndogo wanaona wana haki ya kuwaongoza wenye akili kubwa hata bila ya kufuata vigezo husika kujipatia uongozi.Legitimate question hapa ni vigezo tajwa kwa nafasi husika kwenye swala hili vilifuatwa au laah?Jibu ni hapana taratibu zilikiukwa,PERIOD!
Swali la pili ni kuna sababu za msingi zilizopelekea taratibu husika kukiukwa,mfano hapakuwepo na mwenye qualification kushika hiyo nafasi na ktk waliokuwepo huyo ndiyo alikuwa bora kukaimu hayo majukumu au wenye sifa wamepewa nafasi husika na hakuna aliyeripoti kwenye kituo cha kazi kwasababu ni mkoa mpya na kijijini kwani kuna watu huwa wanapangiwa sehemu za kazi maeneo ya umbali na mikoa mikubwa hawaendi kama ndiyo kilichotokea hili linajadilika..................!
 
Bora umemtaka athibitishe. Wanakoelekea hawa wa namna hii, watasema MD ifutwe, wabaki AMO na CO tu.
Sijui tutaelekea wp baada ya hapo, hosp bila registrars, bila specialists, matibabu bila proper history taking, physical exam, investigation, hosp zitageuka mahali pa ramli au pa waganga wa kienyeji, na theatre zitageuka bucha tu, kwani wanachojua wale jamaa ni kukata na kupasua tu, bila hata indications za kufanya hivyo. Kuna wilaya nilipita, nikakuta rate ya Ceasarean Section(upasuaji wa kutoa mtoto) ni 32%, wkt ya kitaifa ni 15% na WHO recomended ni 10%.
Wao wakiitwa tu na nesi kuona mama mwenye tatizo la kujifungu, bila kujali kuwa maternal na fetal well being ni nzuri na kuna manouver nyingne za kumsaidia mama kuzaa kulingana na tatizo lake.
Wanachojali wao ni sifa ya kupasua tu, na kwa vile wabongo wanakariri anaepasua tu ndiye daktari, wanawapa sifa za kijinga, bila kujua kuwa kupasuliwa bila indication kunampa mtu ulemavu usio na sababu.
Shauri yao wasioelewa, tuwaache waangamie kwa kukosa maarifa.
swali la msingi nani amewafundisha huo upasuaji wa dharura ni MD'S AND MEDICAL SPECIALISTS sasa leo hii walimu waonekane hawafai kushika jukumu ambalo linaelekeza linatakiwa kushikwa na watu wenye credential kama zao.JAMII YA KITANZANIA LEO HII INAPENDA KUSHABIKIA MAMBO HATA KAMA UKWELI UNASUGGEST VINGINEVYO!
 
Jamani wapo MD kibao wakuwapa hii nafasi,hii ni hatari kubwa kwa taifa watu hawajali afya za watu! What do you expect for the GOV which can realise a fake ARV to his Peoples!!!!
Ma MD wengi ni vilaza,yaani,hawajui kazi na kwa sababu hizo bado AMO watapeta sana
 
Ma MD wengi ni vilaza,yaani,hawajui kazi na kwa sababu hizo bado AMO watapeta sana
Mimi nilifikiri watu wanajadili kama utaratibu ulifuatwa au hapana ktk kupatiwa madaraka kwa mhusika lakini kinachoonekana hapa ni ushabiki wa nani zaidi.Nawatakieni ushindani mwema baina ya AMOs and MDs.Have a great day!
 
Back
Top Bottom