Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga akiongea na waandishi wa habari leo amezungumzia suala la Lugumi leo baada ya kutumbuliwa kwake
Amesema Lugumi aliingia mkataba na kampuni ya marekani ambayo ina uwezo wa kufanya kazi na polisi, kampuni hiyo ikanunua vifaa Dell na na kampuni hiyo ikaiomba Dell vifaa hivyo ivifunge Tanzania, Dell wakamchagua Inforsystems hivyo Infosys haina uhusiano wowote na polisi wala Lugumi bali ilikuwa inafanya kazi kwa niaba ya Dell
Pia akijibu swali la kuhusu kutumbuiwa kwake kama linahusiana na Lugumi Kitwanga alitumia majibu aliyedai kuwa ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwa waandishi jijini Nairobi Kenya kwa kuhoji ''Hivi mtu akikuuliza mimi ni mume wa mama yako utakubali?'' na kutaka asiulizwe tena swali hilo
Ila alivokuwa anaongea sina uhakika kama ndio ongea yake au alikuwa 'ametupia' tena