The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Kitwanga anasema kuna kundi ambalo limejipenyeza kwa rais na kila mahala linamshauri vibaya Rais.
==========
WAZIRI wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amesema kuna kundi linalomzunguka Rais Samia Suluhu Hassan ambalo limekuwa likiweka vigingi kwa watu, wakiwamo wataalamu, wanaotaka kushauri kuhusu mambo mema ya kuipeleka nchini pazuri zaidi.
Kitwanga amesema mbali na kuweka vigingi kwa watu wenye nia njema, kundi hilo limekuwa likiwaona tishio, hivyo kuwachafua, ili kulinda masilahi binafsi. Amemwomba Rais kuwa makini na kundi hilo.
Kitwanga alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini na kwamba ameona kuna umuhimu wa kumshauri Rais Samia kupitia vyombo vya habari.
Alisema kundi hilo limejipenyeza katika kila sekta zikiwamo taasisi za umma na kwamba lengo lake ni kuharibu nchi kwa maslahi binafsi.
Chanzo: Nipashe