Kiukweli Wanachadema walimtia aibu Mwenyekiti Mbowe

kama alikua peke yake si wangemuacha aandamane ili aipate aibu vizuri, au walimzuia kumuokoa na aibu, eti ehhe.
Kwanza hakuna maandamano ya mtu 1 wangemuacha tu achape lapa mwenyewe
 
Watanzania watu w amani lkn ukiwasikia mitandaoni utadanganyika lkn siku ya kuandamana wenyewe wamenunua airtime usiku w wakuamkia maandamano wamenyuti home wanafatilia mpambano na washaandaa maneno ya kuwalaani polisi kwa unyama wao. Wengine wao mashabiki wa Israel ukiwasikia wanavyowapamba taifa teule lkn kule Israel wakatoa offers wanaitaji vijana na watepewa haki ya ukaazi ktk taifa teule lenye mibaraka kibao.lkn atuoni ao vijana wakichangamkia iyo fursa wamenyuti kimya kama akuna offers lkn kwenyekushabikia haaaaa wapo moto moto. Utasema wapo Israel adi rahaaa yani.
 
Nikisema “JINI” ndio kama CCM. It is very stable way of economic and political system which has worked on the biggest and populated country in East Africa.

So whatever CCM is doing has worked. We can underestimate CCM because of our subjective ideology of success but in general our beloved government has been successful in maintaining status quo for more than 60 years.

We often feel like we're missing out or inferior compared to more developed countries, What we have is something unconventional and sustainable. Our economic system, though not perfect, allows even those with little to own land, start small businesses, and sell their crops or products. This self-reliance is a strength, not a weakness. We don't consume excessively or migrate in large numbers, make us rooted in our own economy, make us more independent and sovereign as a nation. Instead of seeking validation from external exposure,even though we miss out a lot of things,we should recognize the value of what we already have the ability to sustain ourselves without over dependence on outside forces.
 
Wapumbavu bado mnadhani chadema ni chama cha siasa
..chadema kilisha jifisha siku nyingi wamebaki na sera cha kuchumia tumbo tu kama manabii (kina kiboko ya wachawi kokoo)
 

..Wamaasai hawakutoa taarifa kwa Polisi kuwa wataandamana na Polisi wakawa wamejizatiti eneo la tukio wakiwasubiri wawauwe.

..Maandamano au mgomo hufanikiwa au kufeli kwa kuzingatia upande upi utamuwahi mwenzake kufika eneo la tukio.

..Wamaasai walifika eneo la tukio kabla ya Polisi,matokeo yake Polisi wakasalimu amri.

..Chadema siku ya kumpokea Lissu walifika uwanja wa ndege kwa wingi kabla Polisi hawaja-secure eneo hilo.

..Matokeo yake Polisi wakasalimu amri , na mapokezi ya Lissu yakafunga barabara kwa maandamano toka uwanja wa ndege mpaka Kinondoni Ufipa.

..Kilichotokea ni ELIMU tosha kwa Chadema, vyama vya upinzani, na wanaharakati, kuhusu namna bora ya kuandaa maandamano.

..Bila ELEMENT OF SURPRISE dhidi ya vyombo vya dola hakuna maandamano ya kushinikiza serikali yatafanikiwa.
 
Nchi ni ya wananchi, na si ya wanasiasa pekee. Wananchi kwa ujumla ndio wajenga nchi. Wasipotaka kuijenga nchi yao, wakiwategemea wanasiasa(wachache) waijenge, haitowezekana kamwe.
 

Ukweli usiouona ni huu Hapa:

Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM

Unajipanga vipi kupambana ikibidi hadi kufa na watu wasiojua wanaamini katika nini?

Unadhani Kenya, Bangladesh, Congo, Nigeria au kokote wanakomwagika barabarani polisi wa huko hawachukui dhana za vita?

Unadhani huko wanaokufa kwenye kupigania wanayoamini wanajuta?

Unadhani wapalestina au HAMAS wana majuto yoyote kwenye harakati zao?

Wapi unapoona ni mockery?

Haki za watu hamzijui unadhani angekuwa Lissu hii ngoma isingeanzia Tanga?

Huoni chelewa chelewa ndiyo inayowaangamiza leo Hezbollah Houthi na pole pole itawakuta hadi Iran mmoja baada ya mwingine?

Hakuna mockery hapa zaidi ya kuwa bila kutoka kwenye state of denial ieleweke kuwa tungali tupo tupo sana!
 
Mbona huzungumzii nguvu kubwa ya Polisi kuzima maandamano?
 

Unadhani Hali ni hivyo Hata kama mhamadishaji mkuu angekuwa TAL?

Huko mbona kisingepoa kutokea Tanga?

Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM

Ukweli mchungu huwezi kuwa rafiki wa mungu na shetani wakati mmoja!
 
Kwani wapi nguvu huwa ndogo? Mbona kwingine hayazimiki?
Umewahi kusikia Kenya wakizuia maandamano ki hivyo na kukusanya Polisi kutoka mikoa mingine kuja kuzuia maandamano?
 
Muhimu zaidi message was sent and delivered

Mkuu kwani unadhani oppressors message hawazijui?

Kwamba kama ni messages kumbe hamna haja kabisa hata ya kutaka Maandamano?

Au faida ya Maandamano huijui?

Au wamasai hukuwasikia au hata kuona?
 
Umewahi kusikia Kenya wakizuia maandamano ki hivyo na kukusanya Polisi kutoka mikoa mingine kuja kuzuia maandamano?

Hujawahi kusikia Maandamano yakizuiwa Kenya?

Unadhani waandamanaji walipoifikisha serikali ya Kenya waliyapata kutokea mbinguni?

Au hujui kuwa vinavyoelewa viliundwa?
 
Hujawahi kusikia Maandamano yakizuiwa Kenya?

Unadhani waandamanaji walipoifikisha serikali ya Kenya waliyapata kutokea mbinguni?

Au hujui kuwa vinavyoelewa viliundwa?
Hapo ndipo mnapokosea, Kenya huwa hawazuii maandamano, wanazuia fujo wakati wa maandamano. Wakati maandamano kuna watu wanafanya looting au wizi na uharibifu mwingine kama walivyofanya juzi kuvamia jengo la bunge na kuharibu. Hapo ndipo Polisi wa Kenya hupambana na waandamanaji. Hapa kwetu hata kabla mtu hajaandamana akiwa kwenye ndege au nyumbani au anaongea na waandishi wa habari anakamatwa! Ni upuuzi mtupu!
 
Alishajiaibisha long time sana (2015)
 

Unaanza kuiangalia Kenya kuanzia wapi ndugu?

Kenya ilikuwa ya chama kimoja kama sisi. Imepita kwenye katiba mbovu kama sisi.

Kenya imejikwamua kutoka huko si kwa woga au dhana kama zako.

Ukionacho Kenya hawakupewa, Bali kimepiganiwa.

Nasi hatutapewa bila kuvipigania!
 
Sasa wewe unapigania nini hapa au pengine hujui unapaswa kusimamia nini manake unaonekana kulaumu Chadema kwa kushindwa kuandamana lakini hata hivyo unafikiri Polisi wa Tanzania wanafanya sawa kuzuia maandamano ya amani.
 
Mkuu positive criticism kama aliyoyafanya Mtiberi japo imeegemea upande ni nzuri.

Hata upinzani unapaswa kuambiwa ukweli kama ilivyo kwa chama tawala.

Kila mmoja anapokosea aambiwe kakosea hali kadhalika anapofanya vizuri apongezwe bila ushabiki.
 
Sasa wewe unapigania nini hapa au pengine hujui unapaswa kusimamia nini manake unaonekana kulaumu Chadema kwa kushindwa kuandamana lakini hata hivyo unafikiri Polisi wa Tanzania wanafanya sawa kuzuia maandamano ya amani.

Hakuna popote ninapolaumu lolote, ila ninasimamia hapa:

Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM

Wewe au wa aina yako hamuhitajiki kwenye maandamano popote.

Nikulaumu wewe au nani wa nini sasa?

Tukishatambuana wenye ujasiri tutakiwasha kwa wakati wetu bila ya kumlaumu asiyekuwa muumini kama sisi.

Wanalaumiwa vipi Simba au yanga au wasiohusika kwenye shughuli hii ndugu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…