Kiundwe chombo huru cha kusimamia Jeshi la Polisi

Kiundwe chombo huru cha kusimamia Jeshi la Polisi

Mishenyi

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2019
Posts
464
Reaction score
748
Polisi Tanzania limekuwa jeshi ambalo linaweza kubambika kesi kwa yeyote wamtakae na lisihojiwe na chombo chochote.

Wameenda mbali wanaua mtu yeyote hasa wafanyabishara endapo wataona ana mali za kumpora,wanamuua na wanamtupa na kuchukua mali zake kwa jeuri kabisa wakijua kabisa kwamba hakuna chombo kingine kinachoweza kupepeleleza jinai zaidi yao.

Polisi Tanzania ni janga kuu,serikali unda chombo kipya kilisimamie jeshi la polisi, hawawezi tena kujisimamia, wamegeuka laana kwa nchi

Serikali fanyeni haraka tuokoe wananchi dhidi ya Polisi. Kama mishahara midogo waongezeni.
 
Bila Kusahau chombo cha kusimamia chombo kinachosimamia chombo....

Kuweka mambo rahisi ingefahamika ikajulina na ikatekelezwa kwamba No One, absolutely No One is above the Law
 
Polisi tz limekuwa jeshi ambalo linaweza kubambika kesi kwa yeyote wamtakae na lisihojiwe na chombo chochote! Wameenda mbali wanaua mtu yeyote hasa wafanyabishara endapo wataona ana mali za kumpora...
Mgao wa uharifu wa polisi inamfikia igp na waziri ndio maana wananyamazia ushetani huu. Angalia jinsi maafisa waandamizi wanavyosimama mahakamani kutoa ushahidi wa uongo katika kesi ya mbowe. CCM inahitaji kupumzika hawa, imechakaa
 
Aise jamani jeshi la polisi limeoza na limeoza na limeoza lawama kutoka kwa wananchi wa Hali ya chini ni mengi sana.

Na jeshi Ili limeoza Zaid SI TU mijini vijijini ndo balaa


Siku kadhaaa zilizopita nilishuhudia wananchi wa wilaya ya Muleba kata ya Nshamba waliotaka kumtandika ocs makofi na tukio Ili lilisababishwa na ocs kutaka kuwaongopea kwenye mazishi ya kijana Alie pigwa risasi na kampuni ya ulinzi

Kama hiyo haitoshi ndugu zangu Kila mmoja wetu ajitafakari watu hawa tunapokutanaga nao huko mtaani Nini kina jili?

Kama haitoshi polisi wamemwongopea Mh Rais wa nchi yakuwa Mbowe ni Gaidi sijui walikua Rais ataitwa mahakamani akatoe ushaidi? Ona wanavyoumbuka Kila uchwao

Mh Rais Ili jeshi uanze upya.
 
Jeshi limeoza hilo hii ni habari ambayo tumeiskia hizo nyingine zinazoishia chini chini je?
 
Jeshi lililojaa matapeli na wakabaji.Hatuna cha kujisifia ndani ya jeshi hili.Subiri siku kikinuka kati raia na polisi watakuja kujuta kuzaliwa na kufanya kazi hiyo ipo siku.

Raia wa nchi hii wanateseka sana ndani ya mikono ya jeshi la polisi mauaji yanayofanywa na jeshi hili ni ya kutisha sana.Inasikitisha sana.
 
Bila Kusahau chombo cha kusimamia chombo kinachosimamia chombo....

Kuweka mambo rahisi ingefahamika ikajulina na ikatekelezwa kwamba No One, absolutely No One is above the Law
 
Nani ataacha kuamini kuwa Mosses Lingw'enya aliuwawa akiwa mikononi mwa polisi?

Nani ataacha kuamini kuwa wanachodai watuhumiwa wenzake na Mbowe ni kweli kuwa walipigwa na kuteswa?

Watuhumiwa wa makosa ya jinai wanatendea ndivyo sivyo na jeshi la polisi huku Igp hachukui hatua kujiuzulu.
Vituo vya polisi kuna uozo mkubwa sn
 
Back
Top Bottom