Kiutendaji, Waziri Ridhwani Kikwete akiamua kutokomeza watekaji na wasiojulikana, anaweza....ila...

Footstep

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2026
Posts
383
Reaction score
594
Hili swalanla wasiojulikana kujiamulia watakavyo linalotuumiza vichwa, ni jambo dogo sana ikiwa Waziri Ridhwani Kikwete akiamulia kulivalia njuga.

Awamu ya pili ya mzee Mwinyi marehemu, Aliinuka Mtu mmoja tokea kule Kilimanjaro aliitwa Lyatonga Mrema, alikuwa akitamka Neno, ndani ya masaa kadhaa nchi mzima inazizima na kauli yake inatekelezwa, majambazi na polisi wanalijua hili.

Sasa Kwa Ridhwani Kikwete yeye hahitaji kufanya hivyo maana yeye ni smart, mpole, mnyenyekevu, akiamua kumwambia Shehe Mwaipopo, kwamba Rudisha hao Mbwa mwitu bandani, Shehe Mwaipopo atatii na huu ujinga utakoma mara moja.

Ndugu Kikwete junior, hili kiutendaji lipo mikononi mwako, nakushauri jipe ujasiri, wambie INATOSHA, uone kama Kuna hata mmoja atakayeguna.

Nimemaliza ushauri wangu kwako, sikulazimishi, nakusihi.
 
Usisubiri hadi watu wakusanyike kukuombea ndipo uamke kutimiza wajibu ulio ndani ya uwezo wako kiutendaji
 
Ridhiwani ni Waziri wa TISS ambaye technically ndiye anayefanya utekaji wote.
 
Akili yake inajaa hata kisoda kwani? Wanaoweza kudeal na mambo haya wana akili kubwa na falsafa za maisha yao, acha kumuonea kijana anakula siagi alizotafutiwa na babaye asijepaliwa bureee...
 
Atamteketeza bosi wake aliyemteua
 
Hujui km hujui na hutajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…