Kivuli cha Hayati Magufuli kinataka kumtingisha Rais Samia

Utata tu wa sukari ulioibuka Kwa utawala wake JPM, ufumbuzi haikuwa ni kwenda ulaya kuomba misaada, Bali Kwa kauri yake njema, alitumia vema watu waliopo,

Bakhlesa akampa shamba bagamoyo, basi mambo ya sukari yamepoa,

Uongozi ni ubunifu bhana, embu fikilia kwamba mvua hazitanyesha, tutakaa kusubiri miujiza ya Mungu.?
 
Pamoja nakuorodhesha hayo, raisi pia ni mfariji mkuu kwa watu wake.

Na sifa ya kuu ya kiongozi duniani ni kuaminika na watu wako; ndio science ya siasa za uchaguzi ilipo unataka wananchi wakikusikiliza na kuona matendo yako wanapata imani na wewe. Sasa kwetu kukaripia uzembe ni sehemu ya kuonyesha unajali.

Ukienda nchi zilizoendelea kama wako vitani nchi imevamiwa mwanajeshi aliekwenye chama ndio watataka awaongoze, uchumi mmbaya chaguzi zinazofuata ni economists watatawala.

Sisi tunaufisadi na uzembe uliokithiri tunataka raisi mpole asiekaripia watu; binafsi sikuwa na afiki kila kitu cha Magufuli ila alikuwa mtu sahihi kwa mazingira ya Tanzania.
 
Mwadera mwanambate!!
 
Kazi ya SSH ni kubwa kuliko unavyodhania. Kurudisha mahusiano na mataifa makubwa ya nje ambao ulipotea kabisa awamu ya tano sio shughuli ndogo.

Kusaidia upatikanaji wa masoko ya bidhaa zetu kimataifa ni kazi inayotaka ubunifu mkubwa na kujua namna ya kujichanganya.

Ukame ni kweli unaleta matatizo makubwa ya maji na umeme pia, hiyo video ya afande sele ni sehemu ndogo tu ya tatizo lililoanza miaka zaidi ya thelathini la majiji kama Dar kukaisha miti ya mkoa wa Pwani kwa kukata mikaa miezi yote kumi na mbili ya mwaka.
 
Kazi kweli kweli !!
 
Tatizo la ukame wataalam wanasema ni kila baada ya miaka kumi huwa linajirudia.

Je wataalam wetu wa wizara husika chini ya mbunge wa kisarawe wanalo suluhisho la tatizo hili?.
 
Hizo porojo bakini nazo huko huko serikalini, na chawa mnaowatumia.

Tanzania aijawahi kutengwa kimataifa, raia wake na raisi wao ajawahi kuzuiwa kwenda nchi yeyote na wala aijawahi kuwa na mgogoro na nchi yeyote wenye kuathiri deplomatic relations.

Hakuna nchi mvua zinanyesha miezi 12 ni uzembe tu wa wizara ya maji na TANESCO ndio ulioleta shida.
 
Kwani Tanzania ilivunja uhusiano na Nchi ngapi katika kipindi cha JPM !! Maana umesema kurudisha mahusiano !! Au Rais kutokwenda nje ya Nchi maana yake mahusiano hayapo tena. ? Kwani hao mabalozi huwa wanawakilisha nini huko walipo ?!!
 
pole inakuhusu wewe unaeteseka na kivuli cha marehemu na kujifanya ulikua unamuelewa huku ukiandika gazeti refu kujustify incompetence ya bibi wa unguja
Uelewa wangu ni tofauti kabisa. Rais kutolazimika kuwa karibu na media kwa nia ya kutaka kuitawala hakumfanyi akawa dhaifu.

Ni sawa sawa na JK tulivyomuona kama vile hafai kumbe hali ni tofauti kabisa, kukubali kukosolewa na kupokea maoni tofauti na kila upande hakumfanyi rais akawa na sifa ya kuitwa dhaifu,
 
kwenye "chadomo" mm nikafikiri umemaanisha Chadema!
 
JK sio ulimuona hafai. Ni hafai.
 
Mtazamo na kutengwa ni vitu viwili tofauti. Tunauongelea mtazamo wa awamu ya tano na huu wa awamu ya sita.
 
Kwani Tanzania ilivunja uhusiano na Nchi ngapi katika kipindi cha JPM !! Maana umesema kurudisha mahusiano !! Au Rais kutokwenda nje ya Nchi maana yake mahusiano hayapo tena. ? Kwani hao mabalozi huwa wanawakilisha nini huko walipo ?!!
Kuna mikutano ya kusimamiwa na balozi na kuna inayomhitaji rais mwenyewe awepo ili aonyeshe uzito wa hicho ambacho taifa lake linakihitaji.

Kuna masuala kama ya vibali vya kazi, zipo zinazoweza kufanywa kwa umahiri na wataalam kutoka nje, akaanzisha utaratibu kuwa kibali kikimaliza muda wake huyo mgeni aondoke amuachie kazi mzalendo.

Yale yale ya Mugabe na uporaji wa mashamba ya wazungu, waafrika walioachiwa yamewafia mikononi huku wazungu wakiwacheka tu.

Labda nia ilikuwa nzuri lakini inapokosewa katika utekelezaji wake inaleta picha ya serikali nzima kuwa na hulka za kibaguzi.
 
Hapa ndio nimekuelewa ulianza kumsifia marehemu kumbe kinafiki, kumbe ni mlamba asali.

Leta maji na umeme, wacheni propaganda za kishamba. Kuongoza nchi sio kama kucheza mdako
 
Mtazamo na kutengwa ni vitu viwili tofauti. Tunauongelea mtazamo wa awamu ya tano na huu wa awamu ya sita.
Diplomatic relations ni factual sio mtazamo. Either upo au aupo.

Shida hapo ni story za social media mlizokuwa mnajiambia na kujiaminisha wenyewe; lakini Tanzania aijawahi kuwa na diplomatic issues na nchi yeyote.

Labda kama kuweka msimamo kwenye mambo yako ya kujiamulia kinyume na mabeberu wanavyotaka, panapo tokea majibizano ya hapa na pale ndio tafsiri yako kuharibika kwa diplomatic relations.
 
Until that day...,
When we the people will know its not who is up there who makes things happen, but rather we the people down here who can make a change...., And not through voting but through demanding day to day what is right, and what should be done, and make our voices heard now and not waiting 5 more years for the chance to vote

Until that day....,
When we will know its us who decides what the person up there should do and not her / his favor to do what's supposed to be done...

Until that day...,
When we will know individuals won't make a dent of change but having strong institutions and knowledgeable citizens who are patriotic...

Before then we will continue writing and commenting on such threads with nothing to show for it....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…