Kiwanda cha biskuti za bangi chagunduliwa Kawe

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imekamata watu wanaojihusisha na shughuli za utengenezaji wa biskuti kwa kuchanganya na bangi aina ya skanka katika eneo la Kawe Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas James Lyimo amesema watuhumiwa hao wamekutwa wakiendelea na uzalishaji wa biskuti hizo kwa kutumia mtambo mdogo wa kusaga skanka na vifaa vya kutengenezea biskuti hizo za bangi ya skanka.

Kutokana na operersheni hiyo watu 16 wamekamatwa na Kilogramu 423.54 za bangi iliyosindikwa ya skanka yenye kiwango kikubwa cha sumu ya TetraHydroCannabinol THC ambapo asilimia 75 ikizalishwa kutokana na bangi aina ya Sativa na asilimia 45 bangi ya Indica ikiwa na sumu zaidi ya asilimia 45 ikilinganishwa na asilimia 3 hadi 10 zilizo katika bangi ya kawaida.

Chanzo: Clouds TV
Mpaka kiwanda kianaanzishwa na kufanya production, vyombo vyetu walikikuwa wapi

Waendelee kuagiza mitambo ya kudukua huku wakiacha milango wazi
 
Kwahiyo mamlaka zinasemaje kiwanda kitaendelea kuzalisha au vipi? Na kama kitaendelea wanampango gani na sisi ambao si wenyeji wa daslamu tupate hizo biskuti?je,kama kitazuiwa kosa lao ni lipi?(kwani kuna watumiaji walitoa malalamiko kwenye mamlaka au ni utashi tu wa mamlaka?)
 
hatari sana hiii haiko sawa kwa hawa watoto wetu naipongeza sana mamlaka
Sio biscuits za dukani kwa jinsi zinavyotengenezwa ndio maana wanaziita Biscuit ila ni Bangi zile zile na wateja ni wale wale wameboresha kwa kuchanganya aina tofauti ili watumiaji wapate radha kali zaidi...ni mchanganyiko wa aina tofauti za bang kutoka sehemu tofauti...
 
Hizo biscuits inaonekana zinatengenezwa in small scale sio production kubwa kutokana na maelezo ..na walengwa watakuwa special market. Serikali ifanye uchunguzi pia kwa watengenezaji wa keki maana zinaweza zikawepo keki za madawa ya kulevya kama cocaine etc..
 
Sio biscuits za dukani kwa jinsi zinavyotengenezwa ndio maana wanaziita Biscuit ila ni Bangi zile zile na wateja ni wale wale wameboresha kwa kuchanganya aina tofauti ili watumiaji wapate radha kali zaidi...ni mchanganyiko wa aina tofauti za bang kutoka sehemu tofauti...
aisee umewahi kuziona kwa macho ya nyama ndugu
 
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imekamata watu wanaojihusisha na shughuli za utengenezaji wa biskuti kwa kuchanganya na bangi aina ya skanka katika eneo la Kawe Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas James Lyimo amesema watuhumiwa hao wamekutwa wakiendelea na uzalishaji wa biskuti hizo kwa kutumia mtambo mdogo wa kusaga skanka na vifaa vya kutengenezea biskuti hizo za bangi ya skanka.

Kutokana na operersheni hiyo watu 16 wamekamatwa na Kilogramu 423.54 za bangi iliyosindikwa ya skanka yenye kiwango kikubwa cha sumu ya TetraHydroCannabinol THC ambapo asilimia 75 ikizalishwa kutokana na bangi aina ya Sativa na asilimia 45 bangi ya Indica ikiwa na sumu zaidi ya asilimia 45 ikilinganishwa na asilimia 3 hadi 10 zilizo katika bangi ya kawaida.

Chanzo: Clouds TV
Nawapongeza.hao.wanasayansi coz Wana kitu!mi kama mkemia kama kijana wa kitz anaweza ku extract chemical ya bangi na kuichanganya na unga mzuri wa biscuits na kuuza products kongole kwao!

Na huko ndio kujiajiri kunakotamkwa na wanasiasa Kila siku Wana shauri!!
 
Pana watu wanadhani ni Biscuit hizo za madukani hapana kwa jinsi hizo Skanka zinavyogandamizwa zinakua kama biscuits ili kurahisisha kusafirisha na package yake ila ni bangi tuu hiyo na wateja wake wengi ni wageni kwenye Club na hao wadada wa Mjini...Kilo moja ya Skanka inaweza kufika laki nane harafu ndio uzikute hizo biscuits kwenye maduka ya Mangi hakuna kitu kama hicho...
Ni kweli kabisa mkuu. Ni drug dealer gani mjinga atauza hizo ''biskuti'' kwa watoto wakati bei yake ni ya juu? Ni kama kusema unga wa cocaine utauzwa duka la mangi kwa kupima kama unga wa sembe.
 
Watanzania wengi ni Malaika hatuna dhambi hatujui hata Dunia inaendaje Skanka wanasema wataikuta duka la Mangi harafu ukakope daah kisa imeitwa Biscuit..
 
Back
Top Bottom