Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo unatudhalilisha watanzania, mada hii ungeleta bila ushabiki wa kijinga watu wangechangia kwa kujenga ila unaboa. Nina hakika unasimuliwa tu kuhusu Kenya hujawahi fika laiti ungefika usingekuwa unaandika upuuzi kulinganisha na wao. Kushindana na Kenya ni sawa na kufukuza upepo mwishoe utapotea sababu hujui upepo unapoelekea. Nimebahatika kutembea nchi mbali mbali za Africa na kuishi Kenya kwa muda nakuhakikishia sio wenzetu maana tz nako nimetembea karibu mikoa yote kasoro mtwara na Lindi ninachoongea nakifahamu. Tujitahidi kujadili maendeleo yetu bila kujisifu Bali kuongeza bidii katika kuinua uchumi sio SIFA za kijinga. Serikali inajitahidi kuona tunasonga mbele