Kizungumkuti hifadhi ya Burigi

Sawa, Ngoja nikubaliane na wewe. Tunza post yako, Mungu akitujalia uhai, uje na takwimu ni watumiaji wangapi watakuwa wameutumia uwanja huo wa chato toka sasa hadi 2025. Hawatafika hata Milioni moja... mark my word.
Unajua hapa ndipo tunapofail.. kupanga kwa ajili ya Leo na kesho. Mkuu strategic planning inangalia mbali Sana.. na lengo nikueven out spending ya serikali kuleta harmony katika ukuaji wa Miji yote.

Miundombinu inao mchango mkubwa katika kuvutia uwekezaji na fursa za kibiashara. Pori la Burigi limepandishwa hadhi litatunzwa zaidi matokeo yake kutakuwa sio na wanyama wengi tu ila pia kutunza mfumo wa kiikolojia ambao unaharibika kwa kasi.

Lakini pia misitu itakuwa na kusaidia kuoffest carbon kutokana na uzalishaji mkubwa unaoendelea katika Miji ya Kanda ya Ziwa ambayo pia ndio ukanda populous zaidi nchini. Na kuboresha upatikanaji wa mvua

Sasa kuvutia uwekezaji lazima uwe na trigger projects ... Na Uwanja wa Chato Ni moja tu ya hizo trigger projects . Lakini maboresho ya barabara nyingine Muhimu Kama tabora Kahama Geita-chato. Geita Sengerema Mwanza(Ujenzi wa daraja Busisi) nk.

Sasa Hawa watu (milion kumi wa kushuka) wataanza kushuka lini Chato Ni swala la muda. Lakini biashara nyingi zitasogea sababu ya Uwanja. Na lazima ukumbuke kule tunapokea mvua nyingi pia, na udongo sio mzuri kuwa na njia ya lami Ni advantage.

Zaidi kilichojengwa ni runway tu ya lami, uwezo wa kupokea abiria ni pamoja na miundombinu mingine wezeshi.. ikiwemo jengo la abiria, maeneo ya kutunzia/kupaki ndege nk..na hivi vyote kwa chato bado.
 
Hivi bunge la Ndugai lilikuwa bunge au ili kuwa remote controlled?? Ni maamuzi gani ya bunge l Ndugai unaweza sema hayana dosari?? Cheni kundika vitu hapa kwa kumtetea mtu. Wote tuwe na uchungu na hii nchi. Kama na wewe ulitokea Burundi na mifugo tuweke wazi.
 
Wacha kujitafuna kwa kutaka kuigeuza nyeupe iwe nyekundu kisa kutetea madhaifu ya ccm.

Huo uwanja hata ipite miaka 20 hautafikisha abiria million moja.
 
Huyo ndiyo kwao huko huko Burundi na kwa wahaya wana waita ni washuuti. Na ndiyo wengi wao wamejazana humu jf wanaitwa MATAGA
 
Mikumi kuna uwanja wa kimataifa wa ndege?
Huo uwanja kajijengea JPM!
 

Sasa waTz wanaelewa hilo.....?.....Mimi wenyewe ndio nimesoma hapa na kujua sasa hivi.......
Elimu ni muhimu.......
 
Kila siku danadana za kujenga barabara ya serengeti au kuwalipa wananchi pale musoma ili wapishe kutanua uwanja wa ndege-musoma na kwa taarifa ndogo mmelipa watu wawili tu kati ya mia na pesa nyingine mnajua mlipopeka.

Sasa kutupa habari ya kumfurahisha mtu mmoja wakati kuna sehemu muhimu kuliko huko unapotaja ni sawa na kumdanganya mtoto kumletea pipi ili asilie 😢!
 
Unasema.watalii wanashukia KIA wanachukua hoteli kwanza ndipo wanaelekea Serengeti swali ni watalii wakishukia Chato wanachukua hoteli wapi? au yawezekana ata Chato kwenyewe hujawahi kufika.

Unaposema Uwanja wa ndege Chato imejengwa mjini na siyo kwenye hifandi unamaanisha nini? unajua umbali kutoka uwanja wa ndege Nyabirezi adi mjini ni mbali zaidi kuliko kutoka hapo Nyabirezi adi kwenye Mbuga?

Lakini uliona ile siku mkuu wa mkoa Kagera anakwenda kuzindua geti moja hapo Burigi Chato? Sijui upotoshaji inakusaidia nini.
Unaona busara sana kupotosha kuweka lami kwenye uwanja wa Chato yenye runway 3km na kuiacha viwanja vingine vinavyopanuliwa kwa kusuasua huku tukikosa pesa kutokana na idadi kubwa ya wageni?

Kwa mwaka jana adi leo wageni walioingia Chato ni Rais na ugeni wake kupitia uwanja wa Chato lakini pesa zote zililipwa ata kabla kazi kuanza. Kua mkweli ndugu.
 
Kabla hatujampinga kwa "uongo"wake,Kwanza mtuambie Nani aliweza kumshambulia Mbunge,kwa risasi 18!mchana kweupeee,mpaka leo hajurikani!!maana uongo mliokwisha sema,hata shetani,anaona aibu!
Lisasi za PT yetu,ikipigwa juu,inaendaaa,inarudi chini,inakata Kona,mara paaap!ikampiga mwanafunzi wa ustawi wa jamii,akafa!kesi wakapewa Chadema ya mauaji!!!
Hata nyie ni waongo balaa!
 
Jifunze kuandika kwanza.
 
Duuh! Ukisikia mtu kajibiwa kwa hoja ndiyo hivi Sasa. Huyu mleta mada hawezi kupangua hoja hizi.
 
Kulikuwa kuna ulazima gani wa kuweka Lami hapo Chato ilihali Serengeti baba lao hana lami wala Musoma airport lami hakuna mpaka leo... unajibuje hapo?
Muongozo kidogo.
Musoma Airport lami ipo, sahihisha sentensi yako
 
Ndio kwanza kampeni hazijaanza 😂😂😂mna vingi vyakujibia
 
KIA iko km 40+ toka Moshi,
Songwe km 20+ toka Mbeya City.

Nasioni kwann usijengwe Chato wakati ni sehemu Sahihi kabisa kwa mkoa wa Geita. Usafiri wa Anga, Unakutana na Barabara na Maji pia sehemu gani nyingine kwa Mkoa wa Geita!?

Uwanja umejengwa kwa kuzingatia provisions za sera ya usafiri wa Anga. Ambayo inataka kila mkoa kuwa na uwanja wa kimataifa. Siku ya ufunguzi wa Ujenzi Mh. Mbalawa alisema Ni Uwanja wa Daraja la 4-C na akafafanua Uwanja utapokelewa ndege zenye uwezo wa kubeba abiria 100-200

Kuhusu Mahala pengine labda tuangazie.. maana uchumi unabadilika.. mfano, Kahama Inawateja wengi wa ndege kuliko Shinyanga, ila kwa sababu ya ukongwe tukajenge Shinyanga!? Sasa huwezi jua huko mamlaka za anga wanalitazamaje Hili..labda wako katika kujipanga upya kutoa Huduma kule inakohitajika.

Sioni ninapokuongopea sema ulichoamua kuamini kinakinzana na kile Mimi ninaamini. Hilo tu
 
taifa ya burigi kabla kupandisha hadhi kuwa hifadhi ya taifa ya wanyama pori, Lili kuwa ni pori moja wapo ya mapori ya hifadhi ya serekali ambalo linapatikana mkoa wa Geita,Hili pori lilianzishwa mwaka 1980 Kama pori la hifadhi la akiba.
Tangu lini Burigi ikawa sehemu ya mkoa wa Geita? Burugo iko Biharamulo, mkoa wa Kagera. Kuna na ziwa Burigi pia.
Kwa uongo huu ume-disqualify defense yako yote.
 

1) Watalii wa Serengeti hutua KIA na Arusha na miundombinu wezeshi kwa Hifadhi hii iko Arusha(the Safari capital) na Moshi. Kwann sio Musoma Sijui lakini Kama hauna viongozi wakulipigania sioni haja ya kulaumu.

2) Hapa Iringa tunao Uwanja decent kabisa pale Nduli na ulifanyiwa ukarabati mkubwa tu, mpaka sasa hakuna anayelaumu kwa lolote... Na Kama ujuavyo miundombinu hii ni ghali haijengwi kwa hisia.

3) Kigoma mpaka Sasa wanao Uwanja, na Ni katika viwanja vinavyoenda kupanuliwa sio tu ili watalii waende Gombe lakini pia wafanya biashara na baadae kuwa kitovu Cha usafirishaji ukifuatia maboresho ya reli, barabara na bandari. Ila mpaka Sasa wale wa gombe wanakwenda vizuri na ATCL

4)Mpanda Kahama Geita ndizo Manispaa zinazofuata, na tunataraji viwanja vya ndege kwa Shinyanga na Katavi kujengwa Kahama na Mpanda respectively. Je vitakuwa vya kimataifa!? Hatujui, je Ni lazima viwe vya kimataifa!? Hapana.

5)Ngorongoro &Manyara wanatimia KIA na Arusha, Nyerere National Park na Mikumi wanatumia Dar es salaam.

MUHIMU: Viwanja hivi havijajengwa ndani ya Hifadhi, vinajengwa kwenye Miji ambapo watu wanaweza kupata Huduma nyingine pia.. Kama malazi, chakula, usafiri mwingine, Afya, starehe na burudani. Lakini pia havijengwi kwa ajili watalii tu kuna mahitaji mengine pia ya kiusafirishaji.
 
Mikumi, Serengeti wana airport Na Wao?
 
[emoji1][emoji1][emoji1]hata wale twiga hukuwaona boss?
 
Mambo hata hajayaanzisha Lissu, yeye ameyakuta watanzania wanayahoji na wewe ulikuwepo hapa JF kwanini haukuyajibu muda wote huo? Asalaamalekum.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…