Kizungumkuti hifadhi ya Burigi

Walio wengi wanatetea bila kuwa na hoja za kuutetea huo uwanja.
Wanacho jua ni kutetea na kushangilia na kuwabeza wanao kosoa.
 
Kama haukuona nyani na ngedere naweka shilingi mfukoni.!!!!
 
Ndugu hebu tuwekee picha za leo basi.. maana zilizopo na zinazopatika na kuoneshwa ulimwenguni kote, Musoma airport bado haina Lami...
Hao ulimwengu wajue ili iweje?
We hujui msoma kiwanja kitajengwa mda si mrefu na pia kitajengwa kikubwa hapo hapo msoma na kuwa na viwanja viwili?
Kilicho chelewesha ilikuwa ni malipo ya fidia kwa maeneo ya watu.
 
Kabisa uwanja wa Omukajunguti ndio ungekuwa sehemu sahihi kujenga uwanja Chato ni matumizi mabaya ya rasilimali mali pesa
 
ingependeza zaidi kuona JPM anafuata watangulizi wake
Anafuata watangulizi wake kwa lipi: safari nyingi za ulaya?, Kwenda kupumzika lushoto?

Unaujua mradi wa maji wa chalinze, unajua mradi wa ujenzi wa bandari ya bagamoyo? Unakumbuka bia za bei nafuu za stela Artois?
 
Hao ulimwengu wajue ili iweje?
We hujui msoma kiwanja kitajengwa mda si mrefu na pia kitajengwa kikubwa hapo hapo msoma na kuwa na viwanja viwili?
Kilicho chelewesha ilikuwa ni malipo ya fidia kwa maeneo ya watu.

Ulisema lami ipo, sasa unasema ni mchakato- kwa nini una shift goal post ndugu...? hiyo hadithi ya ujenzi ni ya muda mrefu sana na mpaka sasa ni utamu kolea.. ni lini itakuwa kweli ? kumbuka, sipingi kiwanja cha chato kuwekewa lami, nacho taka ni usawa wa viwanja vyote nchini kuwa na lami ili kuwezesha private sectors zifanye ndege kuwa kama basi na affordable kwa raia wa kawaida kabisa...

Kwa sasa hakuna business case yoyote inayo -justify uwepo wa chato airport... ukipinga, hebu tuwekee ni watalii wangapi walitembelea hiyo burigi wiki jana... hawazidi hata mia moja kwa maoni yangu na kwa data zinazopatikana toka ICAO... je hao watalii mia moja ndio tuwawekee immigration officers 24/7, airport controlers, na ground operation staff?

Operational costs za Chato ni kubwa kama ukifanya Cost benefist analysis ...na sijui gharama za uendashaji analipa nani, tax payers au JPM mwenyewe au Tanzania airport authorities ? wasije kutuambia kwamba wanapata hasara bila mpango kazi...hasara nyingine ni za kujitakia tu...
Magufuli akiondoka tu, Chato itakuwa kama ile airport iliyojengwa na kuku wa zabanga- Mobutu...white elephant...
 
Kuna kipindi kina simba na Twiga walisafirishwa kwenda kwenye makaazi mapya huko
Watakuwepo ila pori lile ni kubwa mno linagusa Ngara, Karagwe, Biharamulo, Mleba, Chato na linapakana na Rwanda huenda wamepotelea msituni au twiga wameliwa na simba
 
Watakuwepo ila pori lile ni kubwa mno linagusa Ngara, Karagwe, Biharamulo, Mleba, Chato na linapakana na Rwanda huenda wamepotelea msituni au twiga wameliwa na simba
Hivi ni lile pori walipo kuwa wanajificha majambazi walio kuwa wanateka magari hasa mabasi?
 

Lisu nilidhani ni mwanasheria "Msomi" lakini amekuwa ni mtu wa porojo sana tangu alipoanza ubunge. Hizo mbuga za Burigi zipo siku nyingi sana wakati Magufuli bado yuko sekondari. Eneo hilo linazo mbuga kadhaa kama ulizotaja pamoja na kisiwa cha Lubondo ambazo ni za tangu miaka ya 70 na 80. Hizi kampeini za kueneza uwongo ni za kuogopa sana.
 
Hoja ni nzuri ila huku mwisho umeiingiza kwenye siasa tena ya chuki kabisa
 
Kama hilo pori lingeweza kuwa mbuga basi wanyama wangejipeleka wenyewe bila kusombwa kwenye magari kutokea serengeti!

Kwanza kitendo cha kuwa na Mbuga artificial kinafanya utalii upungue. Watalii wanataka vitu natural
 
Kulikuwa kuna ulazima gani wa kuweka Lami hapo Chato ilihali Serengeti baba lao hana lami wala Musoma airport lami hakuna mpaka leo... unajibuje hapo?
Hili swari akijibu accordingly basing on his assumption za kuinua sekta ya utalii Tanzania nitakubaliana nae moja kwa moja na alichokisema kuhusu Burigi.
 
Tiz
Ungeweka na idadi ya ndege za kibiashara au za kitalii zinazotua hapo tangu kumalizika kwa uwanja na uwepo wa hiyo hifadhi ya wanyama.

Kama hauna, alichosema TL kitabaki sahihi labda kama kinauma
Tizama hiyo mbuga imefunguliwa hivi karibuni na uwanja umejengwa hivi karibuni biashara ya Utalii siyo kama duka unafungua leo na leo hii unapata wateja inachukua muda baada ya kufanya matangazo na promosheni subiri kidogo utapewa takwimu unazohitaji sijui unafanya utafiti wa utalii, wanyama pori au viwanja vya ndege?
 
Mkuu tatizo letu ni kuwa hatupendi kukosolewa, ukifanya unaambiwa wewe umetumwa na beberu
Tatizo letu kubwa binadamu hasa wa Afrika tumejawa na ubinafsi. Hata hao wanaotetea ni kuwa wameridhika na kubadilisha mboga na viusafiri vyao na watoto wao wakiwa wanasoma shule za binafsi. Hawaangalii hawa binadamu wenzetu vijijini wanavyo shindwa mlo mmoja kwa siku na watoto wao wakiwa wanasoma chini ya miti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…