Tuwekane sawa kidogo kuhusu mambo ya uongo ambayo ameongea ndugu TUNDU LISU mgombea uraisi kwa nafasi kupitia chama Cha demokrasia na maendeleo.
HIFADHI YA TAIFA YA BURIGI
Mwanzo kabisa hi hifadhi ya taifa ya burigi kabla kupandisha hadhi kuwa hifadhi ya taifa ya wanyama pori, Lili kuwa ni pori moja wapo ya mapori ya hifadhi ya serekali ambalo linapatikana mkoa wa Geita, Hili pori lilianzishwa mwaka 1980 Kama pori la hifadhi la akiba.
Katika ukanda huo kwa maana ya mikoa ya Geita na Kagera yalikuwa yanapatikana mapori Kama vile:
Burigi
Kimisi
Biaramulo
Kibanda na
Rumanyika.
Mwaka 2018-2019 kwenye bunge la bajeti,wizara ya utali walipeleka hoja bungeni ya kuomba kupandishwa hadhi baadhi ya mapori ya akiba na kuwa hifadhi za taifa,mapori hayo ni Burigi,Biaramulo,kibanda na rumanyika.
Haya mapori yote yapo katika ukanda muhimu Sana wa ki ikorojia.
Lengo la wizara ya utali kupeleka hiyo hoja ni kwa sababu ya kupanua utali na kuongeza mapato ya taifa ndani ya miaka Saba ili yafikie bill.16 USD yani maana yake wastani wa watali kufikia mil.8 kwa miaka hiyo Saba.
Wa bunge wote wa bunge la Tanzania walipitisha na wakiwemo na wabunge wa Chadema na yule mtoa vimemo vya uongo kwa mgombea wao bwana Mnyika alikuwepo kwenye kupitisha maamuzi hayo.
Lakini wabunge walikubaliana hayo kwa hoja nyingine ya msingi.
Biharamulo,Burigi na Kimisi haya yote yaliunganishwa na kuwa hifadhi ya taifa kwa jina la BURIGI na mapori haya yote yamezungukwa na kata 18 na vijiji 48.
UWANJA WA NDEGE WA CHATO
Kutokana na kupandishwa hadhi mapori hayo na kuwa hifadhi ya taifa kwa namna moja au nyingine ni lazima kuwepo kwa uwanja wa ndege ili uraisishe utali na kupanua wigo wa utali.
Sasa ndio unaona uongo wa huyu mgombea wa Chadema bwana TUNDU LISU kwamba uwanja wa ndege raisi MAGUFULI kajenga kwa ajiri yake.
RAI YANGU KWA WATANZANIA
Tumpinge vikali Sana huyu muongo wa taifa na mchonganishi wa taifa letu kwa huu upotoshaji anaoufanya kipindi cha kuelekea kwenye kampeni za uchaguzi mkuu
Tatizo la Lissu kila kitu anajua yeye na hao wafuasi wake wanaamini kila anachosema kama vile wanaamini dini; yaani hawajipi hata muda kidogo kujiuliza na kulinganisha. Rais anapokuwa anatoka eneo fulani la nchi haina maana kuwa ni marufuku shughuli yeyote ya marndeleo isifanywe anakotoka Rais huyo. Jiulize tu yeye Lissu akiwa rais Ikungi au Singida hakutafanyika chochote?
Mipango ya maendeleo huwa inaandaliwa kwa muda mrefu kulingana na mahitaji au matakwa tarajiwa ya nyakati fulani; hivyo rais anaweza akaingia madarakani na ikaonekana kuwa anafanya jambo fulani kumbe yeye anatekeleza tu kilichoamuliwa kabla yake.
Nakumbuka tangu miaka ya themanini mapori ya akiba yamekuwa yakupandishwa hadhi na kuwa hifadhi kutegemeana na mipango ya kupanua utalii.
Wakati pori la Burigi na hayo mengine yanaunganishwa na kupandishwa hadhi kuwa hifadhi vilevile pori la Selous lilimegwa na kuanzishwa mbuga ya Nyerere. Hii inaonyesha mambo yanafanywa kiutaalam.
Lissu anapaswa aelewe kuwa hiyo hifadhi inaingiza mapato, pia kupitia forward na backward linkage mapato mengine kupitia sekta ndogo ndogo kama mahoteli, maduka ya kuuza zawadi, vyakula, huduma za usafiri!, ajira za kudumu na vibarua nk yanazalishwa kwa mwaka na hivyo kukuza GDP.
Lissu kama anataka kuwa mjuzi wa uchumi atenge muda akasome uchumi au atafute mtaalam wa uchumi afundishwe.
Watu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Kwa somo dogo tu jinsi nchi inavyoendelea mchango wa sekta ya huduma (service sector) ambayo ni pamoja na utalii huongezeka na kuwa mkubwa kuliko sekta zingine. Mfano nchi ya Ubelgiji ambayo yeye Lissu anaitajataja, mchango wa sekta ya huduma katika GDP kwa mwaka 2019 ulikuwa asilimia 69.9. Kwa hiyo jinsi Tanzania tunavyozidi kuendelea ndivyo sekta ya huduma ikiwemo utalii itazidi kupanuka.
Lissu hamuwezi wala kumfikia Rais Magufuli katika menejimenti ya uchumi.