Kizungumkuti hifadhi ya Burigi

Toa mfano wa upendeleo uliofanywa na watangulizi wake kuupa nguvu hoja ya "kiongozi" kupendelea kwao.NYERERE,MWINYI,MKAPA na KIKWETE WALIFANYA NINI KWAO CHENYE SURA HII?
 
Toa mfano wa upendeleo uliofanywa na watangulizi wake kuupa nguvu hoja ya "kiongozi" kupendelea kwao.NYERERE,MWINYI,MKAPA na KIKWETE WALIFANYA NINI KWAO CHENYE SURA HII?

Mimi kwangu sioni kama ni upendeleo as long kilichofanyika ni kitu cha kuwaletea watu maendeleo. Ningeona ni upendeleo iwapo angekuwa amegawa pesa bure au huduma zote za kijamii zinapatikana bure au hata kodi hawalipi. Sasa kujenga uwanja wa ndege Chato ni upendeleo? Au kuipa Burigi hadhi ya mbuga imekuwa upendeleo kweli?
Mbona viwanja vya ndege vipo Mbeya, Mtwara, Bukoba, Iringa, n.k huko hawajapendelewa? Kuna mbuga nyingi tu zilipandishwa hadhi kuwa hifadhi za Taifa, hizo je?
Mi ndio maana nasema haya ni mawazo ya kimasikini na kupandikiza chuki tu kusiko na sababu.
 
Okay, tufanye chato international airport imejengwa mahususi kwa ajiri ya kuchochea utalii hapo burigi, nijibu maswali haya.
1. Kwa nini hakuna scheduled flights za kwenda huo uwanja japo na air tanzania? au hamna watalii wanaokwenda huko?
2. kama ni kweli bunge lilipitisha hiyo burigi kuwa hifadhi rasmi ya taifa miaka hiyo, lilielekeza kupeleka wanyama huko buligi?
yaani kwa nini waliiona burigi kama hifadhi ya taifa ya wanyama wakati haikuwa na hao wanyama?

acheni kutetea upuuzi.
 
Aisee ukifuatilia haya mambo yanayo fanyika kienyeji unaweza kupata blood pressure bure!
 

Ndugu sehemu kutokuwa na scheduled flights haimaanishi kwamba hakuna abiria. Swali dogo kwako, je airtanzania inaenda kila mahali penye kiwanja hapa nchini? Au precision air au hata hizi charter flights, zina scheduled flights kila sehemu penye uwanja wa ndege hapa nchini?

Pili, maisha ya wanyama hayako kama binadamu kwamba kila mahali unaweza ishi. Jamii za wanyama zina tabia na ecolojia inayoweza kuwapa maisha katika eneo hilo. Na ndio maana ukienda ngorongoro hukuti sokwe mtu au kima wekundu au serengeti hukuti simba wanaopanda miti, n.k

Kupelekwa kwa wanyama Burigi inaweza kuwa ni sehemu ya majaribio kuona iwapo wanyama hao wanaweza ishi katika hiyo mbuga na si kwamba haikuwa na wanyama kabisa. Sidhani kama umewahi itembelea yote na kuona kuwa haina wanyama kabisa, otherwise unaleta maneno ya uzushi tu humu
 
MAWAZO YA KIMASKINI UNAYO WEWE. UNGEKUWA NA MTAZAMO CHANYA UNGETUPA SABABU "KWA NINI HAYO YAFANYIKE HUKO NA SI KWINGINE?"
Hoja za upendeleo zinapata nguvu kwa kuangalia mengi kama teuzi za nafasi muhimu kuwapa jamaa zake ili kufanikisha azma zake "ovu". Angalia Hazina,Wizara,Jeshini n.k. Tunapoongea tuna ushahidi na kauli zake zinadhihirisha.Hawezi kujipaka kinyesi kisha alaumu wanaohisi harufu mbaya!
 

Tatizo unauliza maswali ukiwa na mihemko. Rudia kusoma nilichokujibu hapo juu. Ukiniuliza kwanini yamefanyika Chato na si kwingine nami nimekuuliza kwani kwingine hakujafanyika hayo ya Chato, unabaki kuruka ruka tu na sasa umehamia kwenye teuzi.
Wacha kuwa na akili za kimasikini nakwambia tena.
 

Nadhani uwanja huo ungenengwa Mwanza angalau isingekuwa ngumu sana kuutetea.
 
mimi sijaongea ongea tu, namjibu huyo mwenzako aliyeleta justification za kitoto kabisa za kujenga uwanja wa kimataifa wa ndege chato, sasa kwa sababu kutetea upuuzi kunahitaji degree kadhaa za ujinga.


mwenzako anasema uwanja ulijengwa kwa ajiri ya kuvutia utalii, KIA ilijengwa kwa sababu hizi pia, maana ake Chato airport ilijengwa on commercial basis, kama hiyo ni kweli tungeanza kuona ndege zinatua chato za kimataifa, hasa kutokea Nairobi, japo moja kwa mwezi basi jamani.

ama sivyo kila mkoa na wilaya nchi hii kwa sababu za kiusalama na kiserikali kuna uwanja wa ndege, na ni kweli hakuna flight schedules hata kutoka air Tanzania, Geita, Shinyanga,Musoma,Tabora,Singida,Iringa, etc kote kuna viwanja vya ndege na sijauliza kwa nini hakuna flight schedules kwa sababu najua havina viwango vya business based flights, lakini sio kama chato, uwanja wa ndege wa chato ni bora kuliko wa mwanza, sasa kwa nini zinatua ndege ambazo magufuri pekee ?
 
Kulikuwa kuna ulazima gani wa kuweka Lami hapo Chato ilihali Serengeti baba lao hana lami wala Musoma airport lami hakuna mpaka leo... unajibuje hapo?
Serengeti kueka lami sio rahis kivile ,maana ile heritage na iko kwa UNESCO list ,kwaiyo itapoteza ubora wake ,na walisha jaribu ilo ,ila serikal ya Tanzania ilishitakiwa na ikashindwa kesi
 
Uchaguzi wa mwaka huu mtakuwa na kazi ngumu sana ya kumtetea mgombea wenu.
 
Kulikuwa kuna ulazima gani wa kuweka Lami hapo Chato ilihali Serengeti baba lao hana lami wala Musoma airport lami hakuna mpaka leo... unajibuje hapo?
Ile ni mbuga very special ina wanyama adimu Mkuu.
 
..mbuga ya wanyama na uwanja wa ndege ni kwa ajili ya hoteli yake aliyojenga huko.

..wako wanaodai pale alipoapishwa Mwigulu Nchemba ni hotelini kwa bwana mkubwa.
 
Mimi nachojua hifadhi hii ipo Biharamulo na muleba huko kagera. Hivyo watalii watatumia uwanja wa ndege wa bukoba
 
Hiyo miaka unayosema kulikuwa na wanyama gañi?
 
Ungeweka na idadi ya ndege za kibiashara au za kitalii zinazotua hapo tangu kumalizika kwa uwanja na uwepo wa hiyo hifadhi ya wanyama.

Kama hauna, alichosema TL kitabaki sahihi labda kama kinauma
Labda ungetufafanulia unadhani kipi kinapaswa kuanza?? Kujengea uwanja ndio ndege zitue au ndege zitue Kwanza afu ndo uwanja ujengwe??

Uwanja huu na hifadhi hizi bado ni mpya. Tunahitaji muda wa kuboresha miundombinu ya kuhudumia watalii ndio utaona wanatua hapo. Miundombinu hiyo ni pamoja na Mahoteli, viwanja vya ndege na barabara ndani ya hifadhi. Hivyo, ndugu zangu haya Mambo hayatokei overnight. Ni busara Kabla mtu hajaanza kuongea hovyo kwa maneno yakulishwa, tutumie akili zetu kufikiri.
 
Nashukuru kwa bandiko lako. Naomba unambie

Muswada wa kununua ndege na kujenga uwanja wa ndege chato ulipelekwa bungeni ?

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Ndugu yangu, hiyo sasa ndio moja ya sababu kuu za kupandisha hadhi pori hilo. Unapopandisha hadhi pori la akiba, pamoja na Mambo mengine, unaliongezea ulinzi pori husika.

Hifadhi ya Taifa ya Burigi kimazingira na ki-ikologia inao uwezo wa kuhifadhi wanyama wa Aina tofautitofauti (species diversity kubwa) kuliko hata Serengeti. Ila lilikosa ulinzi madhubuti.

Baada ya kupandishwa hadhi, wanyamapori wote ambao bado hawajatoweka watarudi na wengine watahamishiwa hapo ili kuboresha mfumo wa kiikolojia wa hifadhi hiyo mpya.

Ukisoma historia ya hifadhi za Taifa, hata Serengeti haikuwaga na wanyama wengi kama ilivyo leo hii baada ya kupandishwa hadhi. Hivyo, unafurahia wanyama wengi wapo kwenye hifadhi hizo ulizozitaja ni Kwa vile mapori hayo yalipandishwa hadhi siku nyingi na kuongezewa ulinzi. Hivyo, tuipe Muda Burigi, itakuwa hifadhi Bora kama nyingine ulizozitaja.

Hata hivyo, kitendo cha wewe kuona Mbweha ilipaswa ujue kuwa wanyamapori wanaoliwa na Mbweha pia wapo mana Mbweha Hali majani. Vilevile, huwezi kuwaona wanyama woooote waliopo Burigi Kwa siku moja hata kama ungekuwa mtalii achilia mbali mtumia barabara. Ukitaka kujua wanyamapori waliopo Burigi, tafuta taarifa sahihi Tanzania Wildlife Research Institute (TAWIRI). Hao ndio wasemaji eneo Hilo.
 
Nadhani unapotosha. Tafuta taarifa. Lilipokuwa Pori la Akiba la Burigi, mle ndani kulikuwa kunaruhusiwa Uwindaji wa Kitalii tu ambao unafanywa na watalii toka nje ya nchi. Hivyo, fahamu kuwa wazawa walikuwa hawaruhisiwi kisheria kuwinda ndani ya Pori Hilo. Aidha, hakukuwa na miundombinu ya kuhudumia watalii wa ndani. Kwa kupandishwa hadhi, sasa watalii wa ndani wataruhisiwa kisheria kuingia Hifadhi ya Taifa ya Burigi.

Je unaposema wananchi walikuwa wanapata riziki na sasa wamenyimwa, unamaanisha nini?Au unaongelea Ujangili?

Vile vile huwezi kuona wanyamapori wote waliopo hapo kwa kupita tu barabarani. Kwani kuna makazi tofautitofauti mle ndani yanayokaliwa na wanyama tofautitofauti. Ni vyema ufahamu Kitaalam, idadi na aina ya wanyamapori waliopo kwenye Pori fulani hubainishwa Kwa kufanya Sensa. Wewe unapaswa usome taarifa ya Sensa ya Burigi au Hifadhi fulani kama wataka kujua humo ndani kuna wanyama gani. Vilevile inapaswa uende ukatalii humo ndani sio utegemee kukatiza ukiwa kwenye Basi ndio utegemee utaona wanyama wote. Huwezi kujua Aina na idadi ya wanyamapori waliopo kwenye Pori au Hifadhi fulani Kwa kupita Barabarani ukiwa kwenye Basi au Daladala, Hilo ni suala la Kitaalam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…