Kizungumkuti hifadhi ya Burigi

Kuna mbuga kibao kongwe na maarufu ila hazina miundombinu miaka na miaka. Kwenda zako. Kama lengo ndio hilo lako kwa nini asingeanza na kuboresha hifadhi zilizopo kabla ya kushughulika na mpya.
 
..mbuga ya wanyama na uwanja wa ndege ni kwa ajili ya hoteli yake aliyojenga huko.

..wako wanaodai pale alipoapishwa Mwigulu Nchemba ni hotelini kwa bwana mkubwa.
Unamaanisha wananchi wengine hawataruhusiwa kutua kwenye uwanja huo?? Naomba ufafanuzi Kiongozi.

Mimi nadhani badala ya kupiga majungu, tulipaswa tufurahie uwekezaji wa watanzania kwenye nchi yao. Sasa Kama Sugu na Mbowe wanahoteli zao? Mnashangaa nini Kwa Rais wa Nchi kuwa na Hoteli? (Hata kama ni Kweli)? Au Mhe. Rais hapaswi kumiliki Hotel? Haya Mambo mengine mnalalama naweza sema ni Wivu ila hakuna hoja za Msingi.
 
We tuliza domo. Kuna mbuga kibao kongwe na maarufu ila hazina miundombinu miaka na miaka. Kwenda zako. Kama lengo ndio hilo lako kwa nini asingeanza na kuboresha hifadhi zilizopo kabla ya kushughulika na mpya. Acha mahaba ya MATAGA
Hujajibu Maswali niliyokuuliza na usinifokee. Twende hoja Kwa hoja Hadi tutoane Kwa hoja sio kwa vihoja.

Kwa ujumla naweza sema mnatumika kisiasa. Tafuteni hoja zenye Mashiko. Kabla ya Hifadhi ya Mwl. Nyerere na Ruaha kuwa hifadhi kubwa, Hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania ilikuwa ni Serengeti. Je, Uliwahi kujiuliza ni Kwanini uwanja wa kimataifa unaohudumia watalii wa Serengeti upo Mkoani Kilimanjaro?? Ukijibu Hilo Akili inaweza ikazibuka ukaanza kufikiri wewe kama wewe.

Miundombinu mbalimbali nchini imejengwa kimkakati. Ni watu wa ajabu ndio wanaweza ainisha miundombinu na Ukabila. Kwamba Miundombinu huu umejengwa kuhudumia watu wa Kabila Fulani
 
Muelimisheni huyo ndugu muhisika kwani elimu ni bahati haina mwisho. Asante kwa kutuelewesha. Tusiporomoshe matusi si busara
 
Viwanja vya ndege vilivyopo vina hali mbaya na vinahitaji matengenezo makubwa kwanini kujenga uwanja wa kimataifa mahali ambapo hakuna shughuli za kimataifa zinaendelea?
 
Sio tu kimasikini, ni mawazo ya Kifukara.

Walipaswa wajadili baada ya Uwanja wa Chato kukamilika wanadhani ni mkoa gani mwingine uwe na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa.

Uwanja upo ndani ya nchi yao wenyewe, watakaotumia uwanja huo ni wao wenyewe bado wanalaumu. Nadhani wengi wao hawapandagi ndege ndo mana hawaoni umuhimu wa kuwa na hiyo facility ndani ya nchi yao. Wangekuwa ni frequent flyers wa maeneo ya huko wangeipongeza serikali Kwa kuwafikishia huduma hiyo hadi mlangoni.
 
Ndio wanajengewa mazingira Ili na wao wapate shughuli za kuwaingizia kipato kupitia sekta ya utalii Ili wale na wao milo mitatu.
 
Mleta mada, kipi kilianza, Chattle International Airport, au kupandishwa hadhi hayo mapori??
Kama umejichanganya vile??

Everyday is Saturday.......................... 😎
 
Unafahamu mapato yatokanayo na Mlima Kilimanjaro?? Nadhani huna taarifa za kutosha.

Kwa hiyo unamaanisha tufute Mbuga nyingine zote tubakishe Serengeti na Ngorongoro? Labda unachopaswa ufahamu ni kuwa hatuhifadhi Kwa ajili ya kuvutia watalii Tu.

Hifadhi na mapori yetu yana kazi nyingine muhimj zaidi ya utalii. Na huenda fedha zinazopatikana kutokana na huduma nyingine za kiikolojia no zaidi ya zile zitokanazo na utalii.

Unafahamu kuwa vyanzo vingi vya maji vipo kwenye hifadhi zetu? Pori linaweza lisitembelewe na watalii lakin uwepo wake Una umuhim mkubwa Sana Kwa maisha ya wananchi wanaozunguka Pori Hilo. Je likifutwa Kwa sababu hakuna mtalii anayekuja wananchi watapata wapi maji??

Unafadham faida inayochangiwa na hifadhi kwenye huduma ya uchavushaji (Pollination Service). Ukiona unakula tunda Huku mjini jua kuna Uchavushaji umetokea. Na bila mchavushaji kimsingi hakuna maisha hapa duniani. Hifadhi zetu zinasaidia Sana kwenye kuhifadhi viumbe wachavushaji kama nyuki, popo, bettles na vipepeo.

Itoshe kusema, faida za uwepo wa hizi hifadhi ni zaidi ya kuvutia watalii. Naweza kusema kuvutia watalii ni faida ndogo kabisa ya uwepo wa hizi hifadhi. Hivyo mnavyojadili mada hii ya uanzishwaji/upandishwaji hadhi wa hifadhi ni vyema mkawa na uelewa wa kutosha kuhusu faida zake.
 
Kwa nini useme Burigi ipo Geita ingali ina-cover maeneo ya Biharamulo?
Kwa ufupi hifadhi ya taifa ya burigi iliunganisha mapori matatu: Burigi ambayo ipo Mleba, Biharamulo lililopo biharamulo na kimisi lililopo karagwe, kwa muunganiko huo wakalipatia jina Burigi kutoka na ziwa burigi. Pori la Biharamulo lilijumuisha maeneo yote ya pori hilo kabla Biharamulo haijagawanywa na kuzaa wilaya mpya ya chato. Baada ya kugawanywa kipande cha pori la biharamulo kilienda wilaya ya chato hasa maeneo ya katete.

Hivyo burigi kipekeee ni eneo la mleba isipokuwa imebeba jina la muunganiko kutokana na ziwa. Ofisi kuu zipo biharamulo na mlango mkuu upo Nyungwe/ Nyakahura wilayani biharamulo na kambi kuu ipo Nkonji.
 
Hizi hifadhi hazijaanzishwa, zilikuwepo over 40 years now. Kilichofanyika ni kuzipandisha hadhi, kuziongezwa ulinzi na kuongeza fursa Kwa wazawa. Huko nyuma zilipokuwa Mapori ya Akiba, wazawa hawakuwa na uwezo kisheria kutumia rasilimali ya humo ndani mana ni Uwindaji wa Kitalii tu ndio uliokuwa unaruhusiwa.

Kuhusu suala la kuboresha zilizopo Kwanza. Nakubaliana na wewe, lakini unadhan ni Bora watu wa Burigi wasubirie kwanza had Tarangire itengamae? Itachukua miaka mingapi?? Kama haya ndo mawazo yako, basi ni Bora kilichofanyika mana Kwa utaratibu huo watanzania wa maeneo mengine hawataona maendeleo had wanaingia kaburini. Yaani watakufa wkt wanasubiria kwingine kukamilike kwanza kimaendeleo.
 
Hakuna pori linaitwa biharamuro..
Pori linaitwa Kasindaga game reserve
Ila lipo biharamuro..
 
Kwani Daraja la Mkapa halisaidii kuboresha utalii kusini mwa Tanzania? Naimani wakati Mkapa anajenga Daraja lile wapo waliobeza juhudi hizo. Leo hii mnasifu na kusahau masimango aliyoyapata miaka hiyo Daraja lile linajengwa.

Mimi naomba tuweke kumbukumbu vzr, zitasaidia Sana huko mbeleni.

Uwanja ule ukishindwa kutumika uzembe ni wetu Sisi watanzania mana ndio tunapaswa kuchangamkia fursa hiyo. Tunapiga porojo na kubeza huku badala ya kutangaza vivutio vya Burigi na kuleta watalii nchini.

Watalii huenda Mbuga za Kaskazini Kwa vile zinauzwa/zinatangazwa zaidi. Watalii hawasemi Tu wenyewe wanataka kwenda sehem flan. So tupambane tupeleke watalii Burigi.
 
Kuna mbuga kibao kongwe na maarufu ila hazina miundombinu miaka na miaka. Kwenda zako. Kama lengo ndio hilo lako kwa nini asingeanza na kuboresha hifadhi zilizopo kabla ya kushughulika na mpya.
Zitaje,
 
Sawa, Ngoja nikubaliane na wewe. Tunza post yako, Mungu akitujalia uhai, uje na takwimu ni watumiaji wangapi watakuwa wameutumia uwanja huo wa chato toka sasa hadi 2025. Hawatafika hata Milioni moja... mark my word.
Kiongozi inaonekana hata hujui kinachoendelea kwenye hii sekta ya Utalii. Kwahiyo unategemea Hifadhi ya Burigi itapokea watalii million moja ndani ya miaka mitano?? Ni vyema ukafahamu kuwa toka Tanzania upate Uhuru ni mwaka Jana ndio tumepokea watalii 1.5m Kwa Mwaka Kwa mara ya Kwanza. So watalii wanaotembelea nchini mwetu sio wengi kihivyo. So tuna kazi kubwa mbele yetu ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu kama hivi ilivyofanyika kwenye Ujenzi uwanja wa ndege Chato.
 
Sifa pekee ya hifadhi ya Burigi Ina Twiga weupe ambao huonekana kwa nadra na hawapatikani kokote duniani zaidi ya Burigi
 
[emoji16][emoji119]
 
Duuh! Ukisikia mtu kajibiwa kwa hoja ndiyo hivi Sasa. Huyu mleta mada hawezi kupangua hoja hizi.
Hakuna hoja ya maana hapo. Hivi anajua ukanda ule wa Kaskazin Magharibi kuna hifadhi ngapi ambazo watalii wake watahudumiwa na kiwanja kile? Angelijua Hilo asingelinganisha na Iringa, Mara, Kigoma, Katavi na kwingineko.

Lakini afahamu kuwa ukanda wa nyanda za juu kusini tayari kuna Songwe International Airport. Ukanda wa Mashariki kuna JNIA, Ukanda wa Kaskazini kuna KIA. Hivyo si busara kuongeza uwanja mwingine wa kimataifa katika kanda hizi.
 
Haya mafua ya mara kwa mara tunayopataga, nahisi kuna watu huwa wanapenga ubongo badala ya kamasi.
 
Sifa pekee ya hifadhi ya Burigi Ina Twiga weupe ambao huonekana kwa nadra na hawapatikani kokote duniani zaidi ya Burigi
Hivi una taarifa za kutosha kusema hayo eddy? Acha uvivu tafuta taarifa sahihi. Neno kivutio Lina maana pana Sana. Inawezekana Burigi kuwa Chato ni kivutio pia mana ndo Nyumban Kwa Mhe. Rais. Kitu kuwa kivutio inategemea namna tunavyokipackage.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…