Ukweli ni kwamba hizo hifadhi zimeanzishwa kisiasa kwa maslahi ya watu au mtu kwa mitazamo yao au yake. Nia haikua mbaya ila uanzishwaji wake kwangu nauona una mashaka. Hayo mapori yalikua machafu toka miaka na miaka na uanzishwaji wake umekua niwaharaka sana ukilinganisha na hali halisi. Hadi sasa Tanapa ina hifadhi nyingi tegemezi sasa kuwaongezea hizo mbuga tena kwa haraka nikuwaongezea mzigo usio wa lazima.
Nakuhakikishia ata ilazimishwe vip hizo hifadhi hadi zifikie daraja la kati lakuingiza ata wageni 200 kwa mwaka sio chini ya miaka 20.Nakama lengo lilikua nikuongeza idadi ya wageni suluhisho la kwanza lisingekua kuanzisha hifadhi mpya bali kuboresha kwanza zilizopo kwa maana ya zile zinazozalisha vizuri(serenget, tarangire, kilimanjaro, ngorongoro, manyara n.k) zizalishe zaidi kisha kugeukia zisizozalisha vizuri(ruaha, mkomaz, kitulo, rubondo, mahale, gombe, odzungwa, mikumi n.k) zifikie kuzalisha vizuri kisha ndo wazo lakuanzisha hizo nyingine lingekuja, tena ilitakiwa zipande moja baada ya nyingine.