KKKT ni kanisa kubwa kuliko mtu, Kiburi kimemponza Mchungaji Kimaro

Please share na Matsai ni nani?
P
Mastai Ni Mchungaji Kiongozi Usharika wa Kimara Korogwe.. Kimaro ni mwanazuoni wa Mastai... Bora Kimaro Mch Mastai ni Mtu wa Kiroho na anaongea vile Roho anamuongoza na zaidi ukienda Kimara kusali hakuna mambo ya Liturujia...


Dayosisi ya Mashariki na Pwani ina Wachungaji Mahiri mo. Elimu Dunia ya kutosha na Theolojia ya kutosha...

Wachungaji watatu ndio naona wamekuwa mwiba sana..

Mchungaji Wilbroad Mastai

Mch Eliyona Kimaro

Mchungaji Ismael Mwipile

Wanaitwa (Mapacha watatu)

Hawa ni sampuli ya Martin Luther mwenyewe haijalishi we mkubwa kiasi gani wao wanakupa makavu tu...
 
Bila liturujia hilo ni Kanisa la kilokole
 
IIa lazima tukubaliane kuwa Doyasisi ya mashariki na Pwani chini ya Mwalasusa ina matatizo mengi sana miaka yote!

'Saa ya ukombozi ni sasa': By Mch. Hananje
Na hii ni kwa sababu Malasusa mwenyewe ndiye mzizi wa tatizo.
 
Hii ndio tofauti kubwa ya ma padri wa Katoliki, Katoliki ni utii na nidhamu kwanza ndipo ije ibada, sisi Katoliki tuna mpaka jela za kiaina!, kama alivyo fungwa Archbishop Milingo wa Zambia, aliitwa Vatican akatulizwa!. Ukikatazwa kitu na askofu wako usipotii unafukuzwa kama Padri Dr. Wilbroad Slaa, Felician Nkwera na Kalugendo. Wengi wa wachungaji wenye makanisa yao ni Walutheri, Wakatoliki ni wa kuhesabu!.
P
 

Kanisa la wachagga hilo... migogoro huwa haiishi. Subiri ukifika wakati wa uchaguzi ndo utaona muziki wake.

Kiufupi KKKT ni kama CCM tu. Uongozi unapatikana kwa kupiga kampeni na kupigiwa kura. Unategemea migogoro itaisha? Ina maana masuala ya kupanga safu huko yapo kwa sana tu.

Wanaokwenda kiimla (Wakatoliki) ni nadra kusikia wanagombana. Mi nimeshuhudia ugomvi wao mmoja tu ule wa Father Nkwera na wanamaombi wake. Ila Katoliki kiongozi wao wa kitaifa hapa Tanzania anateuliwa na Papa. Hapigiwi kura na wakatoliki walioko hapa Tanzania. Wanaambiwa tu, fulani ndo Papa amemteua kuwa Kiongozi wenu Tanzania.

Hapo ugomvi utaanzia wapi? Nani atayeweka kutoka Tanzania akalipate sikio la Papa amuume na umbea na majungu dhidi ya fulani na fulani.
 
Wengi wa wachungaji wenye makanisa yao ni Walutheri, Wakatoliki ni wa kuhesabu!.

Wengi ni walokole. Ni kizazi kipya ambacho hakitokani na hayo makanisa makongwe ya Katoliki na Lutheran. Pili Ukatoliki ni wa kuzaliwa nao. Ndo maana kanisa katoliki halifanyagi mikutano ya injili. Hawana shida ya kutafuta wafuasi, wao wanaamini wafuasi wapya watazaliwa katika familia za kikatoliki. Wakatoliki huwa ni wale waliopikwa kutoka utotoni, na huwa haitakiwi wajue mafundisho mengine zaidi ya ukatoliki.

Kwa hiyo utagundua kuwa ni ngumu sana kwa Padre wa Katoliki kuanzisha kanisa lake. Hawezi kushindana katika ulimwengu wa ulokole. Mapadre wa kikatoliki wakichepuka huwa wanachepuka na wakatoliki wenzao. Mfano Nkwera kaondoka na wakatoliki. Pale kituo cha EMAUS Ubungo napo wanaokwenda sana ni wakatoliki.

Walokole hawawezi kupata mzuka katika ibada za kikatoliki. Ndo maana utakuwa wakatoliki wanakwenda kwenye ulokole, lakini ni ngumu kukuta Mlokole kahamia kwenye ukatoliki.

Ukatoliki umepooza.
 
Mithali-16:18-19
18.Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.
19 Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi.
 
Shida inaanzia kwenye utawala wenyewe. Umempa mtu likizo ya siku 60 na kumwelekeza akirudi aripoti kwako ilitakiwa iishie hapo hapo mengine yaende kimya kimya kama mmeamua hivyo.
Ila anatoka Askofu anasema baadhi ya wachungaji wanakuwa na kiburi,waumini wanawaamini wachungaji kuliko Yesu,hapo naona kuna tatizo.
Kama waliamua kuliendesha kimya kimya ilipaswa liende kimya kimya.
Askofu kutoka kuongea maneno yale pasipo kuelezea hicho kiburi ni kipi ! Hilo ni tatizo kubwa sana.
 
Kanisa likifikia viwango hivi, halina tofauti na chama cha Siasa au genge la sheitwani mwenyewe. Watu wanacheza na roho za watu aisee.
Ukijua tu walioko kanisani ni hawa hawa binadamu tulio nao kwenye maswala mengine sipati tabu kuhusu hilo la migogoro makanisani

Jamini maaskofu na wachungaji hawajatoka mbinguni, ni hawa hawa waliopo kwenye maswala mengine
 
... ingawa mara nyingi viongozi wasio na maono wala karama yoyote wanakuwa na wivu sana ingawa sikatai ukweli kwamba baadhi ya wenye karama nao sometimes wanakuwa na viburi.
Umekata kote kote...nakazia...wasio na karama wana wivu na chuki sana
 
Unamaanisha Mchungaji Mwangomola

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Unajua kwanini watu wanaenda Shule kuondoa some of vumbi kichwani ili kujua useme nini wapi na wakati Gani na kwanini useme unaweza kuwa na hoja lkn ukikosea hizo Principal unaumia

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Nahii pia ni miongoni mwa shutuma wanazomtuhumu jamaa zake muajiriwa wa Kanisa unahubiri kupitia YouTube channel binafsi Usharika una benefits nini

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Unajua kwanini watu wanaenda Shule kuondoa some of vumbi kichwani ili kujua useme nini wapi na wakati Gani na kwanini useme unaweza kuwa na hoja lkn ukikosea hizo Principal unaumia

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
Kwahiyo mchungaji akiwa madhabahuni haruhusiwi kuongea mapungufu au uovu wa dini yake ?? Haruhusiwi kuongea ukweli wa dunia inakoelekea ¿?? Ni kweli hakuna wachungaji matapeli??! Vp kuhusu waumuni????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…