Klabu bingwa Afrika: As vita club 0-1 Simba dimba la Stade de Martyrs 12/2/2021

Klabu bingwa Afrika: As vita club 0-1 Simba dimba la Stade de Martyrs 12/2/2021

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
52,812
Reaction score
71,392
Naaaaam Barabara kabisa,

Ndugu wadau wa Michezo wa hapa Jamiiforums na kwingineko karibuni katika Live updates(Matukio Mubashara) kutokea hapa Kinshasa katika Dimba la Stade De Martyrs, uwanja wa nyumbani wa Timu ya AS VITA CLUB ambapo kuna "patashika nguo kuchanika" au unaweza kusema kipute cha ligi ya mabingwa hatua ya makundi katika Kundi A baina ya Wenyeji AS VITA ya hapa Congo na Simba Sports Ckub kutokea Tanzania.. Mechi hii itachezwa Saa Mbili usiku ( Kwa saa za hapa DR Congo na Saa 4 usiku kwa saa za Tanzania)

Kikosi cha Simba kilisafiri kutoka Tanzania jumanne kuja hapa DR Congo na kilitua salama, kikipokelewa salama na wenyeji na jopo la viongozi. Walikaribishwa na wakaendelea na mazoezi siku inayofuata.. Wapinzani wengine kwenye kundi hili A, ni Al Ahly ya Misri na El Mereikh ya Sudan ambao nao watapapatuana keshokutwa 16/2/2021

Kuelekea Mchezo huu Muhimu kwa timu zote, Timu ya Simba itawakosa nyota wake wanne kwa sababu mbalimbali ambao ni Erasto Nyoni/John Bocco (Majeruhi) David Kameta (Timu ya taifa U-20) Pamoja na Perfect Chikwende(Sheria za CAF hazimruhusu). Kocha wao Didier Gomes amesema kuwa wanahitaji kushinda magoli mengi kadiri wawezavyo kulingana na nafasi wapatazo ili kujiweka salama kwa mchezo ujao (Japo anajua Kutoka pale ni ngumu)

Kwa upande wa AS VITA kocha wao Florent Ibenge amesema kuwa itakuwa ni mechi ngumu baina ya timu hizo na amesema chochote kinaweza kutokea, ila amejizatiti kimbinu kushinda mechi hiyo muhimu

Kikosi cha As Vita kilichoibugiza Simba mabao matano kwa sufuri sio hiki kinachocheza leo kwa kuwa wachezaji wengi wameuzwa akiwemo Makusu, Tinombe Mukoko, Tuisila Kisinda, Ngoma n.k na Kile cha Simba sio hiki japo kuna baaadhi ya wachezaji walikuwepo wakiwemo Aishi Manula, Chama Cleotus, Kagere, Mkude, Wawa, Dilunga na wengineo

Kumbukumbu za Head to Head

Hii sio mara ya kwanza kwa timu hizo kucheza, huku Simba ikienda na 'kumbukumbu mbaya' ya kuchabangwa "Hamsa" yaani goli 5 bila majibu mnamo mwaka 2019.

2012 : Simba 1 : 1 As Vita Club

January 19 2019 AS VITA 5 : SIMBA 0
Machi 16, 2019 SIMBA 2 : AS VITA 1

Kwenye kundi lao Simba alifanikiwa kupita ila alitolewa hatua ya Robo fainali

Vikosi vya Timu zote mbili vitawekwa hapa kadiri muda utakavyokwenda......

--------------‐---‐-----------------------

Updates on starting XI (Huenda ikawa/Sio Rasmi)

AS VITA CLUB; Assie Koua, Ebunga Simbi, Makabi Lilepo, Masasi, Fiston Mayele, Medjo Simon Loti, Ouattara, Shabani Djuma, Tulengi Sindani, Wamba Merveille, Yacouba Sidi

SIMBA SPORTS CLUB; Manula, Kapombe, Zimbwe, Wawa, Mkude,Lwanga, Chama, Bwalya, Miquissone,
Mugalu, Kagere

Vikosi rasmi vitawekwa vikishatangazwa hapo baadae
----------------------------------------
Confirmed Mechi kwa watakaotizama itaoneshwa saa 4 usiku kupitia Channel ya ZBC2 inayopatikana kupitia Kisimbuzi cha Azam Tv
View attachment 1700848

Wale wa DSTV CHANNEL NAMBA 270 KBC 1

--------------------‐---------------------

Vikosi Rasmi ( CONFIRMED)

Simba XI: Manula Aishi, Kapombe Shomari, Mohamed Hussein (Nahodha), Onyango, Wawa Sergi, Lwanga Thadeo, Chama Cleotus, Mzamiru Yassin, Mugalu Kopa, Bwalya Larry na Miquissone Luis

Substitutes: Kakolanya, Gadiel, Kennedy, Ndemla, Kagere, Morisson, Kahata

AS VITA XI:

AS Vita Club [emoji1078] lineup:

Simon Omossola (GK) [emoji1062]
Djuma Shabani [emoji1078] (Captain)
Ousmane Ouattara [emoji1081]
Vivien Assié Koua [emoji1081]
Ernest Luzolo Sita [emoji1078]
Papy Tshishimbi [emoji1078]
Amedé Masasi [emoji1078]
Sidi Yacoub [emoji1163]
Jéremie Mbuyi [emoji1078]
Glody Mokabi Lilepo [emoji1078]
Fiston Mayele Kalala [emoji1078]

#TotalCAFCL #ASVSSC

_______________________________________
Mpira utaanza muda wowote kuanzia sasa, vikosi rasmi vinaingia dimbani, wanajipanga kwa picha na matukio mengine

Kickoff
00 + 1' Mpira umeanza rasmi na Simba ndio wanasukuma 'gozi la ng'ombe' kutokea kusini kuelekea Vita club waliopo lango la kaskazini

3' Simba wanalisakama lango la Vita ila mipango inakwama.. Vita wanarudi mchezoni... wanapata faulo inapigwa inaokolewa

7' Simba wanacheza vizuri, wanaonana vyema ila mipango yao inatibuliwa pale..aiseee

8' Vita wanapata faulo....inapigwa inaenda nje pale daaah

10' Kona fupi kwa Vita.. wanacheza vizuri ila inatoka nje Papy Tshishimbi anaitoa nje

13' Timu zote zashambuliana kwa Zamu kwa mashambulizi ya kushtukiza, Simba bado beki hazijatulia wakati huohuo Lwanga anafanyiwa faulo na Papy Kabamba, Papy anaonywa

17' Simva wanapata kona ya kwanza, wanaanzishiana fupi..inatolewa nje

20' luis Miquissone anashambulia lango la Vita, bahati mbaya anaushika mwamuzi anapuliza kipyenga..faulo

22' Miquison anatoa mpira inakuwa ni kona kwa Vita, mchezaji wa Vita anapiga kichwa mpira unatoka sentimeta chache langoni

25' Mpira umesimama Lwanga amechezewa faulu, anagangwa kidogo mpira unaendelea

30' Simba wanatengeneza mipango mizuri lakini namna gani pale Bwalya anajichanganya Vita wanaupata mpira

32' Djuma wa As Vita anadondoshwa na Lwanga ila refa anakataa mpira waendelea na kuwa kona ya kurusha kwa Vita

35' Vita wanapata faulo, mita kama 27 kutoka langoni, inapigwa moja kwa moja ila Manula anaidaka

40' Simba wanamiliki mpira ila wanakosa umakini Safu ya Kiungo Mzamiru Bwalya na Chama wanakosa mawasiliano sahihi, Vita wanapata faulo inapigwa lakini Manula anainyaka vyema

42' Bado ngoma Mbichi 0-0, Simba wanapiga counter attack lakini wanashindwa pale, daah nafasi nzuri

45' Dakika moja ya nyongeza kuelekea mapumziko, timu zimekamiana sana

45+1 Mpira ni mapumziko,

tukishuhudia matumizi makubwa ya nguvu, tunaweza kusema kuwa mechi imebalance ila Simba wanakosa umakini sana na Pia AS Vita wanashambulia sana lango la Simba ila hawajafanikiwa kwa kiasi kikubwa

.....Tukutane kipindi cha pili

____________________________________________________________________________

Naaam Kipindi cha pili kimeanza Vita 0 Simba 0

45-46' Mpira umeanzishwa na Vita wakiwa Lango la Kusini la uwanja wa Martyrs wakipeleka mashambulizi kunako lango la Simba lililopo Kaskazini

Tuendelee......huku timu zote hakuna mabadiliko

47' Djuma anamuona kipa wake pale baada ya Simba kushambulia.. Anakwenda chama ila anapoteza mpira

50' J. MBUYI wa Vita anatoa mpira baada ya kubambikiziwa na Chama

52' Simba wanashambulia kupitia chama, wanaanza haraka haraka ila Miquison anapiga shuti dhaifu linazuiwa na ukuta wa vita

54' Kona AS vita wanapata inapigwa ndefu inawahiwa kwa kichwa ila Goal kick mpira unatoka nje

56' Mabadiliko kwa Vita, Mumbere In Papy shishimbi out... mukokyani in Mayele out

58' Simba wanapata penalti baada ya mchezaji wa AS Vita kuunawa/Kuushika katika harakati za kuokoa mpira ule... Naona Mugalu kaushika mpira bila shaka ndie mpigaji

Wakati huo Simba wanafanya mabadiliko

Bwalya Rally nje , Kahata Francis ndani

59 ' Penalti inapigwa pale..... Goooooooaal Mugalu anapata penalt

AS Vita 0 Simba 1

62' Simba wanakosa goal kupitia Mzamiru baada ya kutengeneza chance moja nzuri ila bahati haiko kwao

Sub kwa vita Tulenge Sindani In, Glody Out

65' AS vita wanapoteza nafasi za wazi hapa huku wakisakama lango la Simba kwa udi na uvumba

68' Lwanga anapata kadi ya njano baada ya kumchezea rafu jezi namba 6 wa Vita

70' AS vita 0 Simba 1 , As vita wanasakama lango la Simba , Simba kama wamerudi nyuma hivi kulinda ushindi

Sub kwa vita (double)

Moloko D, Zemanga Soze in

Yacoub and Kalenda J. out

75' Bado 0 kwa vita na 1 kwa Simba

Juma shaban anapenya ngome ya Simba ila anakowa bahati pale daah

77' Mugalu anakamatwa na misuli sijui kama ataendelea... Anaingia Medie Kagere

80' Kona kwa Vita, inaokolewa Simba wanapiga counter attack wanashindwa kuelewana hapa

83' Vivien anapewa kadi ya njano kwa kumchezea rafu kagere

84' AS VITA wanaliandama sana Lango la Simba, huyu beki Djuma Shabani analeta mushkeli kidogo kwa mabeki wa Simba

86' Kona kwa Simba, inapigwa ndeefu Simba wanaokoa hatari ile
Wawa kapewa kadi ya njano kwa kupoteza muda

87' Sub kwa Simba Chama out, Kennedy Juma In

90' Dakika 4 za nyongeza As vita 0 Simba 1

91' Mchezaji wa As Vita - Mayamba anapiga tik taka inaenda nje

90+2' Kennedy Juma anatoa nuksi golini kwao na kuwaweka salama Simba

90+3' AS VITA Wanasakama goli la Simba ila Simba wanasimama imara na kuzuia mashambulizi japo wanachezewa nusu uwanja

90+4' Full time AS VITA 0 SIMBA 1

Simba wanapata ushindi wa kwanza wa hatua ya makundi kwa kuifunga AS Vita bao 1 sifuri kupitia Penalti ya Mugalu Chris Kope ya dakika 59 kuelekea 60

Ahsanteni kwa kunifatilia kuanzia mwanzo hadi mwisho!
 
12 February 2021
Kinshasa, DR Congo

Tazama Mubashara mchezo toka Uwanja wa Mashahidi

HIGHLIGHTS | AS Vita Club 0-1 Simba SC | MD 1 | TotalCAFCL

Source : CAF TV

Kipindi cha pili kinaanza sasa na Simba yaongoza kwa bao la penati dakika 59' mfungaji Chris 'Prince' Mugalu

.............................................................................

Hapo awali kabla mechi super kochee Ibenge alisema haya :

Press Conference : Coach Florent Ibenge Ikwenge wa Club AS Vita akiwa na beki mpya Vivien Assié, kuelekea mechi na Simba SC

Kutoka Kiwanja cha Mashahidi wa Pentecost chenye uwezo wa kuingiza mashabiki zaidi ya 80,000 mjini Kinshasa, coach mkuu Flirent Ibenge Ikwenge wa Club AS Vita azungumza huku akimtambulisha beki mpya kisiki mu-Ivory Coast, Vivien Assié na kuondoa tetesi juu ya kama kweli beki huyo ataichezea Club AS Vita.

AS Vita Club vs Simba S.C, coach IBENGE dub the match as between doubt and caution

The AS Vita Club Sports of the Democratic Republic of Congo is playing its first match for the group stage of the Champions League of the African Footbal Confederation (CAF), on Friday, February 12, 2021.

It (match) will be against Simba SC of Tanzania in the early evening hours at the famous Martyrs of Pentecost stadium in Kinshasa.

On the sidelines of Pentecost stadium pitch in Kinshasa, AS Vita Club coach Florent Ibenge Ikwenge was accompanied by his newly signed Ivorian central defender, Vivien Assié, to answer questions from journalists at a press conference the day before the match.

C1/CAF: Vclub vs Simba S.C, IBENGE entre doute et prudence

L'Association Sportive #Vita Club de la République Démocratique du #Congo joue son premier match comptant pour la phase de groupes de la Ligue des Champions de la Confédération Africaine de Footbal, ce vendredi 12 Février 2021. Ce sera face au Sporting Club #Simba de la Tanzanie dans les heures vesperales au stade des Martyrs de la Pentecôte, à Kinshasa. En marge de cette opposition, le coach de Vclub Florent #Ibenge Ikwenge s'est fait accompagner de son défenseur central Ivoirien, Vivien Assié nouvellement acquis pour répondre aux questions des journalistes en conférence de presse veille de match.
source : Afroinfos 243
 
12 February 2021
Kinshasa, DR Congo

Kocha Didier Gomes wa Simba SC na mchezaji wake Chris Mugalu wakizungumzia maandalizi ya mchezo dhidi ya AS Vita Club, ijumaa 12 February 2021

Coach Didier Gomes awahakikishia wapenzi na mashabiki kuwa timu ipo tayari kimwili na kifikra huku wachezaji wa Simba SC wameelekeza kukusanya point hapa Kinshasa.

Didier Gomes pia anabainisha wanatambua Club AS Vita ni timu nzuri lakini Simba imejitayarisha kufanya vizuri. Simba itamkosa nahodha John Bocco huku mchezaji mpya Perfect Chikwende mzimbabwe hataweza kuichezea Simba SC kufuatana na taratibu za Champion league za CAF kuhusu mchezaji aliyesajiliwa hivi karibuni.
Source : Simba SC Tanzania
 
12 February 2021
Stade des Martyrs de la Pentecòte
Kinshasa, DR Congo

WIMBO WA MASHABIKI WA CLUB AS VITA
Wimbo aliotungiwa Kocha mkuu Florent Ibenge Ikwenge, utakuwa chachu kwa mashabiki wa Club AS Vita kushangilia mwanzo-mwisho bila kuchoka na wao kuwa kama "mchezaji" wa 12 wa AS Vita Club ktk mechi hiyo ya CAF Ligi ya Mabingwa dhidi ya Simba SC.

IBENGE COACHEE SONG - BY TREJAKON

Source : Trejakon TV
 
AC VITA nao naona wamejipanga, Cha msingi Simba icheze mpira wa kuelewana na kujiamini counter attacks nyingi na mashambulizi ya kupitia pembeni yakipandishwa na mabeki wa Kushoto na kulia.
 
Naaaaam Barabara kabisa....

Ndugu wadau wa Michezo wa hapa Jamiiforums na kwingineko karibuni katika Live updates(Matukio Mubashara) kutokea hapa Kinshasa katika Dimba la Stade De Martyrs, uwanja wa nyumbani wa Timu ya AS VITA CLUB ambapo kuna "patashika nguo kuchanika" au unaweza kusema kipute cha ligi ya mabingwa hatua ya makundi katika Kundi A baina ya Wenyeji AS VITA ya hapa Congo na Simba Sports Ckub kutokea Tanzania.. Mechi hii itachezwa Saa Mbili usiku ( Kwa saa za hapa DR Congo na Saa 4 usiku kwa saa za Tanzania)

Kikosi cha Simba kilisafiri kutoka Tanzania jumanne kuja hapa DR Congo na kilitua salama, kikipokelewa salama na wenyeji na jopo la viongozi. Walikaribishwa na wakaendelea na mazoezi siku inayofuata.. Wapinzani wengine kwenye kundi hili A, ni Al Ahly ya Misri na El Mereikh ya Sudan ambao nao watapapatuana keshokutwa 16/2/2021

Kuelekea Mchezo huu Muhimu kwa timu zote, Timu ya Simba itawakosa nyota wake wanne kwa sababu mbalimbali ambao ni Erasto Nyoni/John Bocco (Majeruhi) David Kameta (Timu ya taifa U-20) Pamoja na Perfect Chikwende(Sheria za CAF hazimruhusu). Kocha wao Didier Gomes amesema kuwa wanahitaji kushinda magoli mengi kadiri wawezavyo kulingana na nafasi wapatazo ili kujiweka salama kwa mchezo ujao (Japo anajua Kutoka pale ni ngumu)

Kwa upande wa AS VITA kocha wao Florent Ibenge amesema kuwa itakuwa ni mechi ngumu baina ya timu hizo na amesema chochote kinaweza kutokea, ila amejizatiti kimbinu kushinda mechi hiyo muhimu

Kikosi cha As Vita kilichoibugiza Simba mabao matano kwa sufuri sio hiki kinachocheza leo kwa kuwa wachezaji wengi wameuzwa akiwemo Makusu, Tinombe Mukoko, Tuisila Kisinda, Ngoma n.k na Kile cha Simba sio hiki japo kuna baaadhi ya wachezaji walikuwepo wakiwemo Aishi Manula, Chama Cleotus, Kagere, Mkude, Wawa, Dilunga na wengineo

Kumbukumbu za Head to Head

Hii sio mara ya kwanza kwa timu hizo kucheza, huku Simba ikienda na 'kumbukumbu mbaya' ya kuchabangwa "Hamsa" yaani goli 5 bila majibu mnamo mwaka 2019.

2012 : Simba 1 : 1 As Vita Club

January 19 2019 AS VITA 5 : SIMBA 0
Machi 16, 2019 SIMBA 2 : AS VITA 1

Kwenye kundi lao Simba alifanikiwa kupita ila alitolewa hatua ya Robo fainali

Vikosi vya Timu zote mbili vitawekwa hapa kadiri muda utakavyokwenda......

--------------‐---‐-----------------------

Updates on starting XI (Huenda ikawa/Sio Rasmi)

AS VITA CLUB; Assie Koua, Ebunga Simbi, Makabi Lilepo, Masasi, Fiston Mayele, Medjo Simon Loti, Ouattara, Shabani Djuma, Tulengi Sindani, Wamba Merveille, Yacouba Sidi

SIMBA SPORTS CLUB; Manula, Kapombe, Zimbwe, Wawa, Ame, Lwanga, Chama, Bwalya, Miquissone,
Mugalu, Kagere

Vikosi rasmi vitawekwa vikishatangazwa hapo baadae
.
IMG-20200718-WA0002.jpg
 
Utopolo hii mechi haiwahusu subirini mechi yenu na mbeya city. Simba tuna watu wengi watatupa live update sijui mna kiherehere cha nini mechi zenu tu mnashindwa kutoa update mnaonekana baada ya kupata goli .
 
Nachukua nafasi hii kuwatakia As Vita ushindi wa kishindo kabisa yaani wamalize mpira dakika 45 za mwanzo tu, hizo 45 za pili ziwe ni kufanya mazoezi ya pamoja nao
 
Simba ana 75% ya kushinda hii mechi kama watatumia kila nafasi vizuri,tabia ya kukosakosa magoli mengi kwenye mechi zake za ligi kwenye klabu bingwa zisiwepo.
Ghazwat
 
Back
Top Bottom