Klabu bingwa Afrika: As vita club 0-1 Simba dimba la Stade de Martyrs 12/2/2021

Klabu bingwa Afrika: As vita club 0-1 Simba dimba la Stade de Martyrs 12/2/2021

12 February 2021
Stade des Martyrs De La Pentecòte
Kinshasa, DR Congo

Hamasa na mori mkubwa miongoni mwa wachezaji na mashabiki wa AS Vita Club kuikabili Simba SC


12 Feb 2021
Vita club vs Simba SC: dernier entraînement de Vclub, danse. Quelle ambiance!

L'Association Sportive #Vita Club de la République Démocratique du #Congo joue son premier match comptant pour la phase de groupes de la Ligue des Champions de la Confédération Africaine de Footbal, ce vendredi 12 Février 2021.
Ce sera face au Sporting Club Simba de la Tanzanie dans les heures vesperales au stade des Martyrs de la Pentecôte, à #Kinshasa.
En marge de cette opposition, le coach de Vclub Florent #Ibenge Ikwenge s'est fait accompagner de son défenseur central Ivoirien, Vivien Assié nouvellement acquis pour répondre aux questions des journalistes en conférence de presse veille de match.
Source: afroinfos 243

Tazama uhamashishaji wa super kochee Florent Ibenge kuandaa kisaikolojia timu, Ubao kupanga mashambulizi, ukabaji, umiliki wa uwanja unatumika kupanga mchezo bila kusahau muziki wa kuliwaza bongo


Source : VClub Tèlèvision Officiel
 
Kuwatoa hofu[emoji23]
IMG-20210212-WA0001.jpeg
 
Kama nawaona vile wanavyojipanga kuingia na MAPAKA [emoji192][emoji191][emoji194][emoji193] ya kutosha kwenye mechi yao ya marudio!!
 
MSIKIE IBENGE KUELEKEA MCHEZO WA SIMBA NA AS VITA

“Nawakumbuka wachezaji wengi wazuri ndani ya kikosi cha Simba kama Clatous Chama na Jonas Mkude, kwenye mchezo wetu wa mwisho dhidi yao ambao tulipoteza, nakumbuka Chama ndiye alitufunga bao lililotutoa kwenye mashindano.“

"Lakini pia namkumbuka Mkude alicheza vizuri, nadhani wachezaji hao wanahitaji ulinzi zaidi ili wasitupe madhara kuelekea mchezo huu ambao tutakuwa nyumbani.“

"Mchezo huu ni tafsiri halisi ya mpira, lazima ukutane na mpinzani ambaye unahisi kuwa atakupa changamoto, na unatakiwa uwe tayari kuzikabili changamoto hizo.“

"Nadhani wapinzani wetu hawatakuwa tayari kufungwa mabao mengi kama ilivyotokea awali walipokuja Congo,” ameeleza Frolent Ibenge, Kocha Mkuu wa AS Vita.
 
Dooh!! Nimejikuta naukumbuka ule usemi wa mtani wangu Ghazwat "mwana kulitaka mwana kulipewa"

Mnalo hilo watani na tumeamua kuwaamshia dude la uzi mapeeema kabisa. Mshindwe wenyewe. 😅😅😅😅

#Ukinunauwenasababu.
hii match Simba asiposhinda, atajijengea mlima wa kuukwea.
#SimbaNguvuMoja
 
Naaaaam Barabara kabisa,

Ndugu wadau wa Michezo wa hapa Jamiiforums na kwingineko karibuni katika Live updates(Matukio Mubashara) kutokea hapa Kinshasa katika Dimba la Stade De Martyrs, uwanja wa nyumbani wa Timu ya AS VITA CLUB ambapo kuna "patashika nguo kuchanika" au unaweza kusema kipute cha ligi ya mabingwa hatua ya makundi katika Kundi A baina ya Wenyeji AS VITA ya hapa Congo na Simba Sports Ckub kutokea Tanzania.. Mechi hii itachezwa Saa Mbili usiku ( Kwa saa za hapa DR Congo na Saa 4 usiku kwa saa za Tanzania)

Kikosi cha Simba kilisafiri kutoka Tanzania jumanne kuja hapa DR Congo na kilitua salama, kikipokelewa salama na wenyeji na jopo la viongozi. Walikaribishwa na wakaendelea na mazoezi siku inayofuata.. Wapinzani wengine kwenye kundi hili A, ni Al Ahly ya Misri na El Mereikh ya Sudan ambao nao watapapatuana keshokutwa 16/2/2021

Kuelekea Mchezo huu Muhimu kwa timu zote, Timu ya Simba itawakosa nyota wake wanne kwa sababu mbalimbali ambao ni Erasto Nyoni/John Bocco (Majeruhi) David Kameta (Timu ya taifa U-20) Pamoja na Perfect Chikwende(Sheria za CAF hazimruhusu). Kocha wao Didier Gomes amesema kuwa wanahitaji kushinda magoli mengi kadiri wawezavyo kulingana na nafasi wapatazo ili kujiweka salama kwa mchezo ujao (Japo anajua Kutoka pale ni ngumu)

Kwa upande wa AS VITA kocha wao Florent Ibenge amesema kuwa itakuwa ni mechi ngumu baina ya timu hizo na amesema chochote kinaweza kutokea, ila amejizatiti kimbinu kushinda mechi hiyo muhimu

Kikosi cha As Vita kilichoibugiza Simba mabao matano kwa sufuri sio hiki kinachocheza leo kwa kuwa wachezaji wengi wameuzwa akiwemo Makusu, Tinombe Mukoko, Tuisila Kisinda, Ngoma n.k na Kile cha Simba sio hiki japo kuna baaadhi ya wachezaji walikuwepo wakiwemo Aishi Manula, Chama Cleotus, Kagere, Mkude, Wawa, Dilunga na wengineo


Kumbukumbu za Head to Head

Hii sio mara ya kwanza kwa timu hizo kucheza, huku Simba ikienda na 'kumbukumbu mbaya' ya kuchabangwa "Hamsa" yaani goli 5 bila majibu mnamo mwaka 2019.

2012 : Simba 1 : 1 As Vita Club

January 19 2019 AS VITA 5 : SIMBA 0
Machi 16, 2019 SIMBA 2 : AS VITA 1

Kwenye kundi lao Simba alifanikiwa kupita ila alitolewa hatua ya Robo fainali

Vikosi vya Timu zote mbili vitawekwa hapa kadiri muda utakavyokwenda......

--------------‐---‐-----------------------

Updates on starting XI (Huenda ikawa/Sio Rasmi)

AS VITA CLUB; Assie Koua, Ebunga Simbi, Makabi Lilepo, Masasi, Fiston Mayele, Medjo Simon Loti, Ouattara, Shabani Djuma, Tulengi Sindani, Wamba Merveille, Yacouba Sidi

SIMBA SPORTS CLUB; Manula, Kapombe, Zimbwe, Wawa, Mkude,Lwanga, Chama, Bwalya, Miquissone,
Mugalu, Kagere

Vikosi rasmi vitawekwa vikishatangazwa hapo baadae
----------------------------------------
Confirmed Mechi kwa watakaotizama itaoneshwa saa 4 usiku kupitia Channel ya ZBC2 inayopatikana kupitia Kisimbuzi cha Azam Tv
View attachment 1700848

Wale wa DSTV CHANNEL NAMBA 270 KBC 1
nikajua upo live kumbe ndo kutest mitambo
 
Back
Top Bottom