Dhidi ya Mbabane Dar kabla ya mechi
Leo mnapigwa hapa hapa nyumbani
Baada ya mechi
Simba 4
Mbabane 1
Mnaenda kufa kwao
Marudiano kwao
Mbabane 0
Simba 4
Mmekutana na vibonde hapo ndio mwisho wenu
Dhidi ya Nkana Dar
Mlikufa 2-1 kwao leo mnakufa tena safari ishaisha hiyo
Baada ya mechi
Simba 3
Nkana 1
Kimyaaaaaa [emoji1787]
Makundi
Al Ahly
Simba
As Vita
Js Saoura
Waarabu wawili na m-Congo mmoja hapo Simba anashika mkia na yule jamaa ndio akapigilia msumari kabisa kwa kutuita Under Dog wa kundi
Dar Simba dhidi ya Js Saoura
Waarabu wamekuja kuwapiga hapa hapa nymbn
Baada ya mechi
Simba 3
Saoura 0
Hawa sio waarabu ni wapemba ngoja waje Ahly [emoji1787]
Simba dhidi ya Ahly Dar (kabla)
Sasa leo ndio wamekuja waarabu wenyewe Taifa linaingia ktk aibu nyingine Cairo hamsa na leo hamsa tena
Ramadan Subhi wamemchukua kwa mkopo wa paun billion 10 thamani yake kikosi kizima cha Simba hakifikii thamani hiyo
Baada ya mechi
Simba 1
Ahly 0
Mmebahatisha tu lkn hampiti shughuli mtaiona ktk mechi ya mwisho dhidi ya As Vita hamsa zingine hapa hapa
Simba dhidi ya As Vita Dar
Leo sasa ndio mwisho wa safari mnakufa tena nyingi
Baada ya mechi
Simba 2
As Vita 1
Hamna lolote nyie mnawapulizia dawa wapinzani ndio mnashinda [emoji1787]
Yani kutoa hongera kwao imekua ngumu sana wanageuka vinyonga kila leo kwa kauli zao
Dhidi ya Plateau (Nigeria)
Kabla ya mechi leo Taifa linaingia kwenye aibu kubwa mnaenda kufa nyingi jamaa kila game wanashinda tano tano Enyimba kafa 5 na wengine kibao ni hamsa au 4G
Baada ya mechi
Plateau 0
Simba 1
Wanakuja kupindua matokeo Dar
Leo sasa mnakufa hapa hapa (kabla)
Baada ya mechi Dar
Simba 0
Plateau 0
Mmeshindwa kuwafunga kwenu hata hao wabovu ngoja muone Platinum
Dhidi ya Platinum Bulawayo,Zimbabwe.
Mnakufa nyingi leo
Platinum 1
Simba 0
Chikwende,Chikwende..na kelele kibao na huo ndio mwisho wa safari mnakufa tena Dar
Mechi ya marudiano Dar
Kabla ya mechi
Chikwende leo atakuepo tena
Kwa beki zenu hizo wazee Wawa na Onyango hapo Chikwende na wenzake wanakuja kufanya mauaji tena
Baada ya mechi
Simba 4
Platinum 1
Simba hawashindi mpk mapaka [emoji1787]
Hongera ni ngumu sana kutoa na maneno kila siku yanabadilika
Makundi
Al Ahly
Simba
As Vita
El Merreck
Daaah aibu imerudi tena kwa Taifa zile hamsa hamsa zinarudi tena
As Vita dhidi ya Simba (Congo)
Leo ndio zile hamsa zinajirudia aibu kwa Taifa kila baada ya dkk kadhaa goli,As Vita hatari sana kwao,mara watapakiwa mkongo n.k
Baada ya mechi
As Vita 0
Simba 1
Sasa hivi As Vita hamna timu wameuza sana wachezaji wao [emoji1787]
Hivi ndivyo ambavyo kila siku maneno yanabadilika wanakua vinyonga na wepesi kukana maneno yao ya awali
Simba mnawatesa sana watani mana sio wapinzani,kila wakichagua waume nyie mnaua wanatafuta mwingine mnaua wanapata sana shida hawa wajane
Na nyie wajane fc mjifunze kutoa hongera hata mara moja moja mtabadilisha mabwana mpk lini? mafanikio ya Simba ni mafanikio ya Taifa pia sbb tunawabeba nyie mwende kutembea na kurudi lkn hamna shukrani aibu yenu wenyewe
Tuliwakera sana 2018/19
Msimu huu 2020/21 kero zitaongezeka sbb hatuna nyumbani wala ugenini pagumu kwetu ni Cairo tu na tunauhakika wa kuvuka na kucheza hatua ijayo
Kila siku vitu vizuri tunafanya sisi,wanaume ni sisi,watu wa historia nzuri ni sisi,watu wa ushindi ni sisi,watu wa kulitangaza taifa ni sisi,watu wa kuleta heshima kwa Taifa ni sisi ila watu wa kuharibu ni nyie,watu wa kutia aibu ni nyie,watu wa kushindwa ni nyie,watu wa kuumia (maumivu) kila siku ni nyie,watu wa wivu ni nyinyi yani mnateseka sana..
Poleni sana
Simba Nguvu Moja