Klabu ya Simba imefungiwa na CAF kucheza bila mashabiki na faini zaidi ya TSh. Milioni 100

Klabu ya Simba imefungiwa na CAF kucheza bila mashabiki na faini zaidi ya TSh. Milioni 100

Mechi zinazokuja Simba wasitumie ulinzi wa polisi, waingie mikataba na kampuni binafsi za ulinzi. Fujo zote zimefanywa na watu wachache wameshindwa kuwadhibiti na kuwakamata.
Halafu Azam badala ya kuchukua video za wafanya fujo wao ndio walihamisha kamera upande mwingine.
Wahuni wachache hawawezi kuachiwa kwa upuuzi waliofanya.
 
Hakuna namna mtu atawaza kung'oa viti vya uwanjani bila kufikiria kwanza matumizi na gharama ya viti hivyo. Mtu atafanya hivyo tu baada ya kuwa punguani au kutumia kitu kilichoharibu akili yake.

Viti hivi vilivyoharibiwa ni kodi ya watanzania wote, walioving'oa wanastahili adhabu kali ya kisheria kabla ya adhabu ya kimpira ya TFF na CAF. Uwanja ulikuwa na walinzi na camera za usalama kwanini watu hawa hawajakamatwa kama wahalifu kabla hata CAF kutoa adhabu ya ujumla ya kuwazuia wahuni na walevi kwenda uwanjani kuangalia timu yao?

Ahsante sana CAF kwa kutusaidia kuwaonya walevi na wahuni hawa.
 
Haya majitu yamelitia taifa aibu kubwa sana

Yanang'oa viti, yanajisaidia hovyo na kuharibu miundombinu ya vyooni, yaani ni majitu yasiyo na ustaarabu kabisa

Yaani kushabikia hiyo timu yaani Makolo Culture Troupe ni aibu tayari bado matendo yanayoambatana na mienendo yao isiyo ya kistaarabu

Natoa rai kwa watu wenye utImamu wa akili, bado wanayo nafasi ya kuachana na hilo timu bovu na kurudi kwenye timu yao ya asili, YANGA
 
I salute you kinsmen.
Wakuu mimi mshabiki wa simba kindaki ndaki nimeumia sana sana CAF kutufungia .

Yaani wametufanya wafungwa nchini kwetu? Sijapenda na ticket nimeshanunua mpaka simba mwenzangu ndugu Tate Mkuu ameahidi atakuja mjini kuwatazama simba na ticket nimemchukulia..!

Halafu vurugu walifanya waarabu sio sisi, kama haitoshi vielelezo vipo vya kutosha kuonesha kuwa waarabu ndiyo waling'oq viti sio sisi simb mfano huu hapa.
1736872522152.jpg

PICHANI HAPO JUU MWARABU AKING'OA VITI NA KUWARUSHIA MASHABIKI WA SIMBA, IJAPOKUWA NI MWARABU MWEUSI ..

CAF WANATUONEA SANA.
 
Uwanja ulikuwa na walinzi na camera za usalama kwanini watu hawa hawajakamatwa kama wahalifu kabla hata CAF kutoa adhabu ya ujumla
Walinzi ndio walin'goa viti wakan'goa na camera ili kupoteza ushahidi....

Uzuri ni kwamba mashabiki wa Simba hawanaga ubaya na mtu, hela wanayo akili pia wanazo so faini italipwa na robo fainali mashabiki tutajaa tele pale kwa Mkapa.
 
Baada ya kutoka kwa makolo au mbumbumbu fc
Unawaza kwa kutumia makalio bila shaka....

Ungewaza kwa kutumia ubongo ungebaini kuwa ni ngumu sana kumtenganisha huyo mzungu poli na vyura.

Nakushangaa leo unamkana msemaji wa utopoloz 😂😂
 
Unawaza kwa kutumia makalio bila shaka....

Ungewaza kwa kutumia ubongo ungebaini kuwa ni ngumu sana kumtenganisha huyo mzungu poli na vyura.

Nakushangaa leo unamkana msemaji wa utopoloz 😂😂
Matusi ya nini😀😀 c unaona mlivyokua hamna akili mnazani CAF ni TFF
 
Kufungiwa mashabiki ni pamoja na mechi ya ugenini?si uwanja wako wa nyumbani tu,nikiwa na maana michezo miwili ya nyumbani, hebu nisahihishe ukweli ni upi mana kama ni pamoja na mchezo wa ugenini basi afadhali
Adhabu tayari CAF wameipunguza. Simba Wamefungiwa mechi moja tu kucheza bila mashabiki.
Adhabu ya awali ni kweli ilihusisha mechi mbili za nyumbani, sio ya ugenini
 
Back
Top Bottom