Klabu ya Yanga imetangaza kumsajili kiungo mshambuliaji Clatous Chota Chama raia wa Zambia

Klabu ya Yanga imetangaza kumsajili kiungo mshambuliaji Clatous Chota Chama raia wa Zambia

Sasa wale mashabiki waliokuwa wanatokwa na mishipa ya shingo kumpigia kelele kocha kuwa kila mechi lzm chama acheze dkk 90, watasemaje sasa hv
Na waliokuwa wanasema kila Kocha anayekuja pale Msimbazi lazima aingie kwenye mfumo wa Chama watasemaje sasa?
 
Tutafanyaje ila viongozi wetu ndio wameamua, sijajua huu usajili ni wakiufundi au kumkomoa mtani.
Yanga sisi ni washindi kila sekta, kwenye boli, makombe, kumlaani mtani asicheze champions league aende akacheze loosers cup na ikawa, kamati ya ufundi, usajili wa maana, mashabiki lia lia tunaobweka, fitna za nje ya uwanja , gwaride la ubingwa dunia nzima hawatufikii, kukomoana na mtani na yoyote anaetaka ugomvi tuko tayari, pesa ya usajili ipo, ukileta ujuaji na kiburi kwa mwananchi tutakukomesha kwa jeuri ambayo ni next level, ona sasa Azam walimchukua Feitoto wakajisiiiiiifu kuwa wao wajaaaaanja, tumelipa kwa Dube, yani tumepiga Azam pale panapouma zaidi, sasa kwa hawa kolos aka simba mzee tumeamua tu tuwaonesha jeuri na kuwa mziki wao mdogo sana wa kitoto na haubambi, Yanga hii ina masifa mno kwasasa ni uonevu na vipigo tu kwa underdog wote kama my wetu Simba, Azam, Singida big stars, Ihefu , hatuangalii sura, hatucheki na kima!!
 
Yah:MWALIKO
Baada ya CHAMA kuondoka Simba Napenda kuwaalika wanaSimba woooote kujumuika pamoja leo Pale Tabata Kiwanja ni The Great kufurahia Chama kuondoka Klabuni na kwenda Uto.
Mpira ni burudani, Mpira ni furaha, Mpira ni ajira haina hajja kujengeana chuki wala kuwekeana mtima nyongo.
Chama aende tuuu na abebe na Nguruwe wake kabisaaaa maana huenda pia ndicho kitu pia wamekitamani Uttopolo.
 
Mpira wa bongo bwana 🤣🤣🤣

Washkaji hua wanashangaa kwanini hua inakua ngumu kwangu kuufuatilia.

Mahasimu wa jadi wanauziana wachezaji? 🤣🤣🤣 Hii ipo Tz tu. Na bado huyo mchezaji atasifiwa alipo na alipotoka. Hii ipo mpira wa Tz tu.
kaenda kama free agent
 
Yah:MWALIKO
Baada ya CHAMA kuondoka Simba Napenda kuwaalika wanaSimba woooote kujumuika pamoja leo Pale Tabata Kiwanja ni The Great kufurahia Chama kuondoka Klabuni na kwenda Uto.
Mpira ni burudani, Mpira ni furaha, Mpira ni ajira haina hajja kujengeana chuki wala kuwekeana mtima nyongo.
Chama aende tuuu na abebe na Nguruwe wake kabisaaaa maana huenda pia ndicho kitu pia wamekitamani Uttopolo.
Dah, nguruwe tena?!!! Yaani uto tunapenda kitimoto? You must be kidding me 👉!!

Tumeambiwa kuleni nguruwe ikiwa tu ng'ombe hamna!! Siku msosi ukikosekana ni kujipiga tu kitimoto, hiyo lini sasa??
 
Back
Top Bottom