AL SHARPTON
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 2,797
- 953
Mkuu wakati niko porini kwa sababu black mamba ana uwezo wa kuruka tulikuwa hatusogei karibu. Akitokea ghafla ni mawe na Vipande vya magogo tu.
Kwahio tukielekea Porini tukakuta kichuguu humimina mafuta ya taa ndani yake na kukaa mbali.
Basi nyoka yyt aliomo humo ndani mbio atakayotoka humo si ya kawaida.
Koboko (black mamba) huwezi kumsogelea bila kuwa Mtaalamu wa Nyoka. Na sababu kuu ni ule Urefu wake. Anaruka ka bullet. Na sisi wengine Viazi na ugali kila siku tulikuwa Wazito sana kwa hio we never take a chance!
Na kingine hawa Koboko sumu yao ilivyo kali huwa inapanda Mwilini fasta sana na kusimamisha moyo faster than you think.
Kuna Bubu mmoja aligongwa na Huyu Koboko kaja mbio kambini anapiga kelele tumeshindwa kuelewa nini anasema amekufa chini ya dakika 10!
Sura yake na macho yake yalibadili rangi ajabu kabisa.
Huyu Nyoka ukikutana nae ni kurudi nyuma na Kumtazama mpaka apotee. Ukimpa mgongo tu umeondoka.
Hatari kuliko kupiga kofi Polisi wa bongo mwenye njaa!
Shukran kwa elimu ya hili joka. Nilikuwa nina safari ya kwenda porini Handeni kwenye madini lakini imebidi niiahirishe kidogo sababu ya hii story ya koboko manake nasikia huko Kwedikwazu wamejaa