Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Na mbwembwe zake zote koboko hana ujanja kwa bundi. Ndiyo sababu usiku hatembei.
 
Hivi kati ya black mamba na Greena mamba nani hatar zaidi?
Nakumbuka kipind flan nilitembelea mbuga ya mikumi sehem moja inaitwa Genesis nilipata kuoana viumbe mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyoka lakn niliambiwa Green mamba ni nyoka mpole na hana kawaida ya kung'ata hovyo ila ndio nyoka mwenye sumu kuliko nyoka wote.

Niliambiwa Green mamba huwa anaogopwa na nyoka wengne kwan hata kama akijichanganya na nyoka wengne anaweza kuwazuru wote na wakafa.

Unasemaje juu ya hili Dola Iddy
 
Last edited by a moderator:
Akikutana na nyegere(honey burger) hizo sifa zoote anaweka mfukoni.ila binadamu ukifanikiwa kumuua utakuwa umeacha kazi umefanya kazi..hatari aloo.
 
K 4 LIFE njoo umuone shoga yako yule aliekukimbiza masaa mawili.
 
Last edited by a moderator:
Maelezo mazuri kiasi lakini ingefaa utuambie unayatoa wapi maelezo hayo ili tujue kama yanatokana na uzoefu au siyo ili tuweze kujua thamani yake. Mie ni mmojawapo niliyechunga ng'ombe wakati wa udogo wangu na nilikutana mara nyingi na nyoka huyo. Kwa uzoefu wangu nyoka huyo ni wa aina nyingi; wengine wafupi na wengine warefu lakini wote ni machachari. Rangi yake ni ya kijivu zaidi lakini alama yake kubwa ni huo mdomo mweusi. Maelezo nilikuwa nikipata kwa wazazi wangu kabla sijafungulia ng'ombe kwenda porini yalikuwa: nikikutana na simba au koboko (huyu naye ndiye simba wa nyoka) anashambulia ng'ombe niwaache ng'ombe nirudi nyumbani niwaeleze wakubwa. Hii ilikuwa ina maana nikikutana na dharura nyingine nishughulikie kadri nitakavyoona inafaa. Na kweli nikikutana na wengine kama nyoka mweusi, cobra, pamoja na makeke yake hakunitisha; akipanua mdomo nilikuwa namtupia jiwe la manati na likimpata kwenye domo alilopanua nyoka anakuwa hoi. Black mamba yuko sehemu nyngi mno hapa Tanzania. Anapenda sehemu yenye mvua ya kadri, isizidi inchi 40 za mvua kwa mwaka au sehemu kavu yenye mito au visima vya maji. Kwa hiyo Iringa kavu ya Ilula, Ismani, Pawaga, Idodi; Dodoma, Singida, Tabora, Chunya ni halali yao. Game Park ya Ruaha wako wengi.
Black mamba ni nyoka anayehodhi eneo lake, (territorial snake) hivyo husiamamia mkia na kuchunguza mgeni nayeingia kwenye eneo lake; anaishi zaidi ya miaka 12. Pia bila shaka mnajua nyoka wote hawasikii. Macho, harufu na mtikisiko wa ardhi ndiyo kinga yao.
 
Mtoa mada umechanganya madesa,black mamba sio koboko.hawa ni nyoka wawili tofauti,hebu jaribu kutafti tena
 
kumuona kwake ni nadra sana ndio maana ukimuona ujue kuna tatizo litakutokea au atakua amejeruhiwa

huwa hataki vurugu

anaweza kusikia sauti au kishindo cha mtu akiwa umbali wa mita 500 kwa kuwa hataki vurugu hujificha na hutomuona lakin kama amejeruhiwa ni hatari sana kupita kwenye eneo lake

anaweza kufunga barabara kama amejeruhiwa

wengine waliokomaa huwa wanaota kucha mkiani ambayo hutumia kusimamia kuangalia hatari

akikasirika hupenda kuuma kichwani

anauwezo wa kuruka kufuata target

masika huishi juu ya miti na kiangazi kwenye vichuguu

hauwezi kumshika kichwa kama nyoka wengine yeye anauwezo wa kuuma vyovyote utavyokishika kichwa

sio mjinga kama nyoka wengine kichwa chake chepesi kupiga hesabu za nini afanye
 
Naogopa Nyoka, nahisi nikikutana nae ntalia kama mtoto
 
Naogopa Nyoka, nahisi nikikutana nae ntalia kama mtoto


haha haa
umenikumbusha siku nilienda na beibe shamba kuna michungwa mingii...wakati yeye busy na watu wa shamba mie uhindi ukaniingia kuchkuch hotae mpaka kwenye miti nimchumie mpenzi, gafla mti wa jirani akadondoka nyoka akakimbia na mie mbio nalia kama mtoto mdogo
 
Asante kwa elimu nzuri ulete na elimu kuhusu chatu maana mie nimelikimbia shamba wiki iliyopita baada kukuta vijana wameua chatu shambani kwangu.[l/IMG]
 

Attachments

  • 1451159458492.jpg
    1451159458492.jpg
    85.1 KB · Views: 863
Pia haujatupa mbinu za kupambana na nyoka huyu au angalau kumuepuka.

Nyoka inasemekana huwa anapafu moja. So hiyo speed anaweza kwenda um bali gani
 
Back
Top Bottom