Maelezo mazuri kiasi lakini ingefaa utuambie unayatoa wapi maelezo hayo ili tujue kama yanatokana na uzoefu au siyo ili tuweze kujua thamani yake. Mie ni mmojawapo niliyechunga ng'ombe wakati wa udogo wangu na nilikutana mara nyingi na nyoka huyo. Kwa uzoefu wangu nyoka huyo ni wa aina nyingi; wengine wafupi na wengine warefu lakini wote ni machachari. Rangi yake ni ya kijivu zaidi lakini alama yake kubwa ni huo mdomo mweusi. Maelezo nilikuwa nikipata kwa wazazi wangu kabla sijafungulia ng'ombe kwenda porini yalikuwa: nikikutana na simba au koboko (huyu naye ndiye simba wa nyoka) anashambulia ng'ombe niwaache ng'ombe nirudi nyumbani niwaeleze wakubwa. Hii ilikuwa ina maana nikikutana na dharura nyingine nishughulikie kadri nitakavyoona inafaa. Na kweli nikikutana na wengine kama nyoka mweusi, cobra, pamoja na makeke yake hakunitisha; akipanua mdomo nilikuwa namtupia jiwe la manati na likimpata kwenye domo alilopanua nyoka anakuwa hoi. Black mamba yuko sehemu nyngi mno hapa Tanzania. Anapenda sehemu yenye mvua ya kadri, isizidi inchi 40 za mvua kwa mwaka au sehemu kavu yenye mito au visima vya maji. Kwa hiyo Iringa kavu ya Ilula, Ismani, Pawaga, Idodi; Dodoma, Singida, Tabora, Chunya ni halali yao. Game Park ya Ruaha wako wengi.
Black mamba ni nyoka anayehodhi eneo lake, (territorial snake) hivyo husiamamia mkia na kuchunguza mgeni nayeingia kwenye eneo lake; anaishi zaidi ya miaka 12. Pia bila shaka mnajua nyoka wote hawasikii. Macho, harufu na mtikisiko wa ardhi ndiyo kinga yao.