Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aisee wapo wengi sana Kasulu hao wanyoka haswa eneo la Makere. Anaruka kama ndege halafu anakupa ya utosi usioombee ukutane Naye. Pia huwa anawika kama jogoo, sehemu anayokaa huwa miti imekauka maana akiwa na hasira huigonga na sumu yake kukausha miti
kumuona kwake ni nadra sana ndio maana ukimuona ujue kuna tatizo litakutokea au atakua amejeruhiwa
huwa hataki vurugu
anaweza kusikia sauti au kishindo cha mtu akiwa umbali wa mita 500 kwa kuwa hataki vurugu hujificha na hutomuona lakin kama amejeruhiwa ni hatari sana kupita kwenye eneo lake
anaweza kufunga barabara kama amejeruhiwa
wengine waliokomaa huwa wanaota kucha mkiani ambayo hutumia kusimamia kuangalia hatari
akikasirika hupenda kuuma kichwani
anauwezo wa kuruka kufuata target
masika huishi juu ya miti na kiangazi kwenye vichuguu
hauwezi kumshika kichwa kama nyoka wengine yeye anauwezo wa kuuma vyovyote utavyokishika kichwa
sio mjinga kama nyoka wengine kichwa chake chepesi kupiga hesabu za nini afanye
Acheni hadithi za vijiweni....koboko anang'ata sehemu yeyote ile katika mwili wa binadamu na huishi popote si juu ya miti tu hata mapangoni na vichakani. Acheni ujinga wa hadithi za vijiweni kuna watu wamesoma humu.
Mkuu umenichekesha sanakuna hawa wachina watengeneza barabala alikula hiyo nyoka alijua ni zile za kichina mwili wake ulikua unatoa majivu tu kabla ya kufa.
Koboko ni hatari aisee, ila cobra nae usimchukulie poa ni habari nyingine.
Huyu mdudu ni hatari kama ni hivyo aiseecobra sumu yake inakuua ndani ya masaa 2,ukiwahi hospitali umepona,koboko sumu yake usipotibiwa ndani ya dakika 4 ushakuwa marehemu,halafu koboko ana uwezo wa kugonga hata watu 100 na akawaua wote kwa dkk chache wakati cobra akishakugonga mara moja anakuwa fala tu hana nguvu tena ya kugonga tena kwa kuwa jino lake hubakia kwa aliyemgonga wakati koboko jino lake hubakia kinywani mwake,baba huyu mdudu kiboko yake ni bundi na eagle na mdudu fulani hv wa porini anayependa sana kukaa majini ila sio mdudu mwingine wowote yule duniani
Huyu mdudu ni hatari kama ni hivyo aisee
Duh basi koboko hana mpinzanicobra sumu yake inakuua ndani ya masaa 2,ukiwahi hospitali umepona,koboko sumu yake usipotibiwa ndani ya dakika 4 ushakuwa marehemu,halafu koboko ana uwezo wa kugonga hata watu 100 na akawaua wote kwa dkk chache wakati cobra akishakugonga mara moja anakuwa fala tu hana nguvu tena ya kugonga tena kwa kuwa jino lake hubakia kwa aliyemgonga wakati koboko jino lake hubakia kinywani mwake,baba huyu mdudu kiboko yake ni bundi na eagle na mdudu fulani hv wa porini anayependa sana kukaa majini ila sio mdudu mwingine wowote yule duniani
Kijijini kwenu wapi?Nyoka huyu kaua sana kijijini kwetu.
Very nice analysis ingawa hujasema mazingira yapi anapenda kuishi(baridi, joto sana,misituni au katika mbuga) na je harufu au mavi ya ng'ombe yanathari kwake? Kisha naomba kufahamu kama wale nyoka wa majini nao ni aina ya koboko( black mambas)Habari wanaJF,
Leo nataka tufahamishane kuhusu nyoka huyu hatari kwa sisi waswahili tunamuita KOBOKO lakini kwa lugha ya kiingereza huitwa Black Mambas
Black mamba ni moja ya nyoka hatari sana katika dunia. Nyoka hawa hupatikana katika sehemu Mashariki na Kusini mwa Afrika. Black mamba anaweza kuishi katika aina mbalimbali za mazingira: savanna, mabwawa, misitu na maeneo ya miamba. Makazi yoyote ambayo hutoa joto na unyevunyevu ni sehemu nzuri ya kuishi Black Mamba. Kutokana na uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa kilimo, makutano kati ya Black Mamba na binadamu yameongezeka zaidi.
View attachment 344401
1- Black mambas ni nyoka mwenye sifa ya urefu anaweza kufikia miguu 14 urefu na 1.58757 katika uzito.
2- Black mamba ana mwili mwembamba kufunikwa na ngozi yenye magamba kama ilivyo kwa nyoka wa jamii nyingine, Pamoja na wao kujulikana kwa kiingereza kama Black mambas lakini hawana rangi nyeusi katika ngozi na rangi ya mwili inategemea makazi yao na inaweza kuwa ya kijani, kijivu au njano.
3- Black mambas ni jina lake kwa sababu sehemu ya ndani ya vinywa vyao ni nyeusi kabisa. Black mamba kuonyesha kinywa chake cheusi wakati anakabiliwa na hatari.
4- Nyoka huyu huanza kutanua shingo yake lakini sio kama afanyavyo COBRA na hutoa sauti kama ile ya tairi likiwa inatoka upepo na hii ni ishara nyingine kwamba kiumbe hutayari shambulio. Ukiona amena moja ya hizo ishara unashauri wa usifanye chochote kwasababu kwa kasi aliyonayo hutaweza kumuwai kifupi tulia mpaka hasira zishuke na ajiondokee narudia usithubutu kujifanya unafurukuta matendo yako hayatawahi tendo lake.
5- Ingawa nyoka huyu amebeba sifa ya kuwa nyoka mjeuri na mkali sana, lakini nayeye hujaribu kutoroka kabla mashambulizi lakini hushambulia kwa ukatiri sana ikibidi. Kumbuka kwa mtulivu ukikutana nae
6- Sasa upande wa sumu hapa ndipo patamu Black mamba ana aina mbili ya sumu zinazozalishwa katika mwili wake moja ni huitwa Neuro – hii huathiri mfumo wa neva na nyingine ni Cardio-toxin hii huathiri mfumo wa moyo na sumu hizi zinaweza kuua binadamu chini ya dakika 20. Pia imethibitika kuwa matone mawili ya sumu yake inaweza kuua.
7-Black mamba anatumia sumu kuwinda aina mbalimbali za ndege na wanyama wadogo. Na hutumia kama kitoweo chake
8- Black mamba anaishi katika mashimo ya miti na katika mashimo ya miamba. Pamoja na kiasi kikubwa cha sumu kali sana aliyonayo, lakini hana ujanja mbele ya Nguchiro na Mbweha, na Nyegere.
9- Black mamba hutembea haraka sana akiwa juu ya ardhi. Anaweza kusafiri umbali mrefu kwa kasi ya maili hadi 12 kwa saa. Hivyo usijaribu kukimbia atakufukuza mpaka akugonge sehemu ya mwili wako.
10- Jike hutaga mayai kati ya 10 na 25 katika kiota juu ya ardhi. Joto ni muhimu kwa ajili ya incubation ya mayai. Na mayai hujitotoa baada ya miezi 3. Na vijinyoka hivyo vichanga huanza kujihudumia kwa kila kitu na huwa na sumu ile ile kama ya nyoka mkongwe hivyo usije ukadharau.
View attachment 344402
11- Black mamba anaweza kuishi hadi miaka 11 katika pori na hadi miaka 12 katika kama atafugwa.
Kuna documentary moja ninayo mwanzo mtangazajia anasema kama ukikutana na huyu nyoka usithubutu kufanya chochote hatari sanaHuyu nyoka ni hatari sana. Kama wewe ni mtu wa miraba minne ni bora upambane na chatu ambaye kwa kawaida hana sumu kuliko kukabiliana na nyoka huyu.