JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Akizungumza katika mahojiano na Mtangazaji Robert Marawa ambayo yamerushwa na 947 Joburg, kocha huyo amesema:
Baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kesho yake tulikaa kikaoni na uongozi wa Klabu kikiongozwa na Waziri wa Fedha ambaye ndiye bosi wa Klabu, akaeleza kutofurahishwa na uwezo wa timu na jinsi kikosi kilivyopangwa, alivuka mipaka ya majukumu yake.
Licha ya kwamba yeye ni Waziri wa Fedha lakini ilikuwa 'too much', nina taaluma najua ninachokifanya, ndio maana mtu akiingilia majukumu yangu namuachia afanye yeye hiyo kazi.
Ndio, kulikuwa na hoja hizo, mchezaji hapangwi kwa kuangaliwa anapendwa na mmiliki au historia, kikosi kinatokana na mazoezi ya wakati husika.
Hapana sikupigiwa simu, ingetokea hivyo ningeondoka muda huohuo.
Niliondoka kikaoni baada ya kuona wanazidi kuvuka mipaka, walinihoji mambo ambayo waliingilia taaluma yangu na nikaweka wazi mbele ya viongozi wote kuwa sitaendelea na majukumu, sikuandika barua ya kujiuzulu na niliona hakuna umuhimu wa kufanya hivyo kwa kuwa nilitamka mbele yao.
Sikutaka kudai fedha na wala uwepo wangu haukuwa umeshawishiwa na fedha, wanaweza kuzitumia katika miradi mingine.
Makocha wengine wanafanya kazi kwa mtindo huo wa kupangiwa timu na kuingiliwa majukumu ya taaluma zao lakini kwangu mimi hilo haliwezekani
Makocha Wasaidizi
Kocha huyo wa zamani wa Kaizer Chiefs na Moroka Swallows amesema makocha wasaidizi ambao alikuwa akifanya nao kazi “Bado wana mikataba na ni juu yao kuamua kama waendelee kubaki au wataondoka.”
Afisa Habari wa Singida
Hussein Masanza alipoulizwa amesema “Tumeona taarifa zake lakini kama klabu hatujapata taarifa rasmi kuhusu maelezo yake, bado ni kocha wa klabu yetu na tunajua yupo Afrika Kusini, kama kukiwa na lolote atatupatia taarifa ya maandishi.”