Kocha Fadlu umefedhehesha brand ya Simba, hukupaswa kusema Yale kwenye vyombo vya habari pengine na wewe umechangia kutuangusha

Hivi Fadlu huwaga ni mhindi au Mchina?
 
Ongeza na ile mechi ya Namungo
 
Amesema ukweli mtupu Simba hatuna wachezaji wa viwango, ila viongozi wetu Sasa Wana mdomo wa viwango. Wanatupiga lugha Kila siku Ili tuwaone Bora kumbe mbuzi tu ,yaani inauma Sana unajua. Hawajali hisia za mashabiki wao
 
Siku Simba ikianza kusajili wachezaji na kuacha kuokoteza ndiyo siku itaanza kuleta ushindani kwa Yanga.

Kwa mpira wa msimu huu ushindi 60% ulikuwa mbinde mno, simba imetawala michezo katika mechi chache na mbaya zaidi wachezaji ni kama wanalazimushwa kucheza mfumo ambao hawautaki na hawauwezi.

Mpira wa Jana hata kama angechezesha Mangungu Simba tusingetoboa.
 
Duh!!
 
Mimi ni mnyama ingawa sijamsikia kocha akisema hivyo

Lakini si haki kusema kwamba Fadlu hajafanya chochote,tusimuone kocha mbaya kwa matokeo ya dabi

Tangu aje amekuwa akijenga timu na matokeo tumeyaona

Nguvu moja daima
Oya jamaa

Yule jamaa wa MLIPUKO MKUBWA SANA bado yupo?
 
hii ndo ile tunaita ukweli mchungu...POLE KOLO
 
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
 
Na Mpanzu ameshasinya miaka miwili. Anaenda kucheza na mafundi, huwezi kumchezesha Mpanzu na Mukwala na Mutale timu moja. Amejionea dharau kubwa.
 
Daah Simba hawawezi kupiga pasi kumi mbele wanaruka ruka wanamrudishia kipa daah huyo Kagoma alipotezwa mbaya hapo kati na huyo Duke Abuya mapafu ya mbwa wa polisi.
 
Wazungu ni wa kweli na wapo straight sana mkuu.
 
Sasa kwani uongo simba
 
Ulitaka akayasemee wapi kumbuka lazima na yeye alinde CV yake

Swali je yule mchezaji bora wa mashindano ya shirikisho 24/25 alicheza dabi ya namba 184 tarehe 25-06-2025
 
Kwa ubishi wenu wa kutokubali kwamba mna kikosi kibovu natamani Mendeleev na ubishi huo huo tuwakande 10 times back to back
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…