Kodi kwa 'watoto' wa miaka 18?

Kodi kwa 'watoto' wa miaka 18?

Ni hivi
Kila huduma ufanyayo unakatwa kodi ila hautambuliki kama mlipa kodi. VAT hulipwa na mtumiaji wa mwisho ambao ni sisi.
Hivyo basi ili tuonekane ni walipaji, kila mtu itambidi awe na TIN ambayo itasajiliwa kwenye Number za Simu na Bank, kwamba ikitokea umefanya malipo kwa njia tajwa basi ile VAT itaenda kwenye acc yako kule TRA na utajulikana kama mlipakodi
Exactly
 
TIN ni namba ya kulipia KODI mpaka pale utakapofanya MIAMALA... Digital Currency nayo mbioni, mbona kazi ipo.
 
Kama 18 hakupaswa kuwa twgemezi, niambie ni kazi gani huyu 18yr old anaweza kufanya na kuhitegemea.

Kwa mfumo wa elimu yetu, huyu kama hayupo o level basi ni a level, ni tegemezi100%, na ndio maana hata nhif waliona waongeze kidogo umri wa mtu tegemezi hadi 21yrs coz 18yrs kiuhalisia bado ni mtu tegemezi kabisa licha ya kutambulika kama mtu mzima.

Mimi ningeshauri hata kama hiyo taxpayers id watatoa kuanzia 18yrs old, lakini kodi wanayotaka kumkamua mtu iwe kuanzia 25yrs, hapo walau mtu anachakarika mtaani jamani.

Wengine hawaelewi ninachoongelea mkuu,18 ni mtoto moja, mbili kuandaa mlipaji kodi wa badae ni upuuzi. nani anajua Rais mwingine atakuja na Policies zake na kazi kwa vijana hawa itakua hamna kabisa😁😁😁😁, hayo madude watakaa nayo yawasaidie nini?
 
Usikute huu ni mpango-mkakati wa ma- CCM kurudisha ile kodi ya kichwa kwa watu wote wanao anzia miaka 18!
 
utataka tu maana kodi tayari - TIN number si hiari tena ni lazima kila mtanzania mwenye 18 awe nayo. Hukawii kufika kwenye huduma yoyote wakakuomba TIN number kwanza !! 🙂🙂

Mkuu nipe kazi basi,lol
 
Siyo kila mwenye miaka 18 yupo kidato Cha nne!!..na wanesema mwenye kipato,mna shida gani vichwani!!?
mwenye shida kichwani ni wewe. Tanzania ya leo over 90% ya watoto wanaomaliza darasa la saba wanamwagwa katika shule za secondary za kata wakiwa na miaka 14 au 15. come 18 bado wako secondary..

Hao unaosema wana miaka 18 na wana kipato ni watoto wako au wadogo zako? Jifunze kushughulisha ubongo wako
 
mwenye shida kichwani ni wewe. Tanzania ya leo over 90% ya watoto wanaomaliza darasa la saba wanamwagwa katika shule za secondary za kata wakiwa na miaka 14 au 15. come 18 bado wako secondary..

Hao unaosema wana miaka 18 na wana kipato ni watoto wako au wadogo zako? Jifunze kushughulisha ubongo wako
Turudi kwenye takwimu tuone vijana umri huo ni wangapi Tanzania,ili tuamini kweli wote wapo sekondari
 
Back
Top Bottom