Chipukizi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 4,409
- 6,773
This is sad,
Miaka 18 hata Advance hajamaliza...au ndio anamaliza...
Haya ni maamuzi ya kukurupuka, una uhakika huyu 'mtoto' yuko kwenye 'ajira'rasmi?
Sana sana utawashawishi watoto wasifocus na shule waingie mtaani kutafuta ajira, unskilled jobs.
Huwezi ukafanya mambo( kodi) kama nchi zilizoendelea.
Wakati hujawawezesha ama hujaweka in place Mfumo utakaotoa ajira kwa vijana hawa.
Ukiangalia profile la kijana wa miaka 18, ni mdogo, hana skills zozote, bado yuko kwenye proccess ya kutafuta ana fit wapi in terms of career and his own identity.
Leo drastically unataka alipe kodi?
Profile la kijana huyu ni simply ' unemployable'.. sijui walifikiria nini.
Mbona ni simple logic, una create ajira, then ndio unataka watu walipe kodi.
Sio watu walipe kodi, wakati hamna ajira.
Unless nimeelewa tofauti,
Ila hii policy wamekurupuka,
Itakuwa very challenging kumuweka mtu mwenye profile la mtu wa miaka 18 ambalo ni unemployable awe employable.
Bora hata wangesema miaka 25 sababu mtu wa miaka 25 tayari ana ujuzi hata kama anaweza asiwe na uzoefu.
Wanaofanya decisions on our behalf simply ni useless...
Waste of space..
My honest opinion...
Rebecca.
Yes it can be done! Na kuwasaidia vijana zaiadi ya hao milioni 7. Na wakatengenezewa ajira endelevu. Kuna nchi tayari wanafanya hivyo na tax base yao imekuwa for 45% . Ukiiangalia unaweza ona aiwezekani na pia ni kituko- Lakini hii inaweza kuwa mkombozi wa Vijana wetu hapa nchini.View attachment 2261264
"Kila mtanzania mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 na mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi. Ili kutimiza amza hiyo, Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 au zaidi"
"Kwa kuwa utaratibu wa usajili wa namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA) unamtaka kila mwananchi mwenye umri wa miaka 18 au zaidi kujisajili NIDA, napendekeza kuwa wale wote wenye NIDA kwa sasa (wanaofikia milioni 19 nchi nzima) wapatiwe namba ya TIN na itumike kwenye miamala yote inayofanyika katika ununuzi na mauzo yanayofanyika ndani ya nchi"
"Kila mwenye namba ya mlipakodi atapata makadirio yake kwa njia ya simu na kulipa kodi husika kwa njia ya mtandao"
- @mwigulunchemba ,Waziri wa Fedha na Mipango
#BajetiKuu