Kodi kwa 'watoto' wa miaka 18?

Kodi kwa 'watoto' wa miaka 18?

Ni hivi malipo yeyote ukifanya serikalini inabidi uwe na tin number,
Unaweza usiwe mlipa kodi lakini ukaagiza gari inje ya inchi na ukataka kuilipia ushuru na kuiregesta ni lazima uwe na tin number,
Au siku serikali ikisema leo tunagawa hela kwa wanachi woote inabidi uwe na tin? [emoji1787] naona zitagombewa
Kwahiyo tin (tax identification number), inaweza kufananishwa na social security number Kwa nchi za magharibi? Ila Kwa wao ni tangu mtoto anapozaliwa.
 
Punguza hasira bibie, TIN unakuwa nayo ikikutambulisha kama mlipa kodi, futa kwenye kichwa chako kuwa mtu mwenye miaka 18 ni mtoto. Huyu ni mtu mzima na ndiyo maana hupiga kura. Mbona hulalamiki hapa??
Ni mtu mzima sio? wakati ndio kwanza anamaliza Advance na bado ni tegemezi?!
 
Serikali ndiyo mlezi mkuu, kuna hekima kubwa sana kwenye hili jambo. Kwanza, litawafanya watoto wetu kujifunza their civic duty, kulipa kodi. Pili, litaharakisha watoto wetu kujitegemea, watoto wa kisasa hawajigusi na utakuta mtu ana miaka 40 bado yuko kwa wazazi kama mtegemezi. Haya ni matumizi mabaya ya rasilirasilimali watu kwani kila raia ana wajibu wa kutoa mchango wake katika ujenzi wa taifa kwa namna yake popote alipo. Tatu, sheria zetu zinatambua miaka 18 kuwa ni age of majority hivyo basi, siyo kulipa kodi tu, wanaweza kufungwa jela au kupelekwa vitani. Mwisho, kama nchi lazima iwe na misingi ya uwajibikaji, kila mtu awajibike.
Mkuu kungekuwa na Policy kwanza kuhakikisha vijana wana hizo kazi zipo ningewalewa...Ni kwa vile tu hamuelewi, kijana wa miaka 18 bado ni tegemezi, wachache sana ndio wanaingiza kipato nao ni circumstances zimewafanya wawe hivyo, sasa hii small segment ya population ndio ije kukufanya ufikirie kila kijana wa Kitanzania awe na Kitambulisho cha kodi ama alipe kodi ni kukosea, wajengee kwanza skills/knowledge wajitegemee ndio then ufikirie mambo ya kodi. I think kufanya shule kuwa free kuanzia Primary mpaka Advance free ni way foward lakini haya mambo ya kodi tunadanganyana.
 
TlN Ni utambulisho tu wa mlipa Kodi siyo shulutisho la kulipa Kodi nikama NIDA tu inakutambuliaha tu, ndivyo wanafanya duniani huko mf.india,us,uk etc,tax is legal compursory payment, lazima tulipe ipo kisheria
Labda India ila US na UK usiliznganishe na Tanzania, huko kuna ajira kibao hata mtu akiacha shule, sio Tanzania. NImewaelewa ni kitambulisho cha ulipaji kodi, ila ingekua kulazimisha watoto hawa kulipa kodi moto ungewaka leo..lol
 
Pole,
Ila miaka 18 siyo mtoto, ni mtu mzima.
Kama ni mtoto ni wa kwako tu.
Usiseme wa kwangu peke yangu, wakati Majority ya wazazi kibao tanzania wana watoto wenye miaka 18!, labda useme peke yako kuwa mtoto wa miaka 18 ni mtu mzima mwenzio
 
This is sad,

Miaka 18 hata Advance hajamaliza...au ndio anamaliza...

Haya ni maamuzi ya kukurupuka, una uhakika huyu 'mtoto' yuko kwenye 'ajira'rasmi?

Sana sana utawashawishi watoto wasifocus na shule waingie mtaani kutafuta ajira, unskilled jobs.

Huwezi ukafanya mambo( kodi) kama nchi zilizoendelea.

Wakati hujawawezesha ama hujaweka in place Mfumo utakaotoa ajira kwa vijana hawa.

Ukiangalia profile la kijana wa miaka 18, ni mdogo, hana skills zozote, bado yuko kwenye proccess ya kutafuta ana fit wapi in terms of career and his own identity.

Leo drastically unataka alipe kodi?

Profile la kijana huyu ni simply ' unemployable'.. sijui walifikiria nini.

Mbona ni simple logic, una create ajira, then ndio unataka watu walipe kodi.

Sio watu walipe kodi, wakati hamna ajira.

Unless nimeelewa tofauti,

Ila hii policy wamekurupuka,

Itakuwa very challenging kumuweka mtu mwenye profile la mtu wa miaka 18 ambalo ni unemployable awe employable.

Bora hata wangesema miaka 25 sababu mtu wa miaka 25 tayari ana ujuzi hata kama anaweza asiwe na uzoefu.

Wanaofanya decisions on our behalf simply ni useless...

Waste of space..

My honest opinion...

Rebecca.
Msizae mizigo kwa serikali, zaeni walipa kodi.
Jitu zima linazaa watoto 10, halafu elimu bure, hospitali bure.
Mkue kiakili.
 
Msize mizigo kwa serikali, zaeni walipa kodi.
Jitu zima linazaa watoto 10, halafu elimu bure, hospitali bure.
Mkue kiakili.
Kila mtoto anakuja na baraka yake yakheee

Unadhania watoto 10 ukiwajengea uwezo wakazalisha hawataleta Maendeleo Tanzania?
 
"Haiuzwi kwa wenye umri chini ya miaka 18"
Hapo unaelewa nini??

Miaka 18 ni Mtu Mzima tayari sio Mtoto kisheria ila kwa Mzazi bado atakua Mtoto hata akifika miaka 70.

Mnhhh sijui unapinga nini na unakubali nini, mtoto wa miaka 18 ni mtoto sawa na huyo asiye chini ya miaka 18 period!
 
IMG_7493.jpg
 
Mkuu kungekuwa na Policy kwanza kuhakikisha vijana wana hizo kazi zipo ningewalewa...Ni kwa vile tu hamuelewi, kijana wa miaka 18 bado ni tegemezi, wachache sana ndio wanaingiza kipato nao ni circumstances zimewafanya wawe hivyo, sasa hii small segment ya population ndio ije kukufanya ufikirie kila kijana wa Kitanzania awe na Kitambulisho cha kodi ama alipe kodi ni kukosea, wajengee kwanza skills/knowledge wajitegemee ndio then ufikirie mambo ya kodi. I think kufanya shule kuwa free kuanzia Primary mpaka Advance free ni way foward lakini haya mambo ya kodi tunadanganyana.
Japo sio mjuzi wa haya mambo lakini wacha nitoe maoni yangu, kuwa na TIN namba ni sawa na ww kuwa na namba ya simu mfno huwez kumtumia mtu pesa kama hana namba ya simu, kifupi kama hana simu, so kwa kuwa kila mtu anapaswa kulipa kodi itakuwa hivi, kuliko makampuni ya simu ndo yalipe kodi badala yake ww ndo utakAtwa kodi moja kwa moja, kwa hiyo mfno unataka kutuma pesa kwa MPESA utalazimika kuingiza TIN no yako piaa ili ulipe kodi, unataka kulipa pesa serikalini kwa control namba utaweka pia TIN namba yako, unatakaa kulipia BIMA,utaweka TIN namba yako, kika mtumishi wa Umma ana TIN namba yake tutazitumia kulipia ving'amuzi, miamala ya Benki, kuweka Vocha, kulipia majengo, kupangisha nyumba, kulipia umeme, Maji, kulipia huduma hospitalini, mashuleni, viwandani, yaan walipaji wataanza kulipia benki au mpesa ili ukatwe kodi sio kupeana mkononi pesa, nenda kwenye miradi ya SGR hadi vibarua hela inalipwa benki sasa tutawapa TIN namba ili wakienda kuchukua malipo yao wakatwe kodi.....

Pole kwa mwandiko Mbaya
 
Mnhhhh sasa ukatwe Tax kwenye maji,umeme,hospitalini,Mashuleni, na huduma nyingine utabaki na kitu??? au nimekuelewa sivyo Mkuu???
 
Serikali yetu haina ubunifu kabisa kutwa kujaziana mavitambulisho. Ilitakiwa ID ya nida ibebe kila kitu hata mtu akienda hosp medical records ziwepo humo,akiwa na criminal records ziwepo humo. Sasa wao kutwa kuibua project mpya moya wasizozimalizia kutwa kujichotea pesa tu na kutapanya
 
what for? mapambo?
Happy uelewe mtoto tin take itaonesha manunuzi tu na sio mauzo au mapato. Sasa analipaje hiyo Kodi?
Kodi ni tofauti Kati ya manunuzi na mauzo,
Kwa lugha nyingine hutaweza kununua bila tin , sasa hapo hamna atakayeweza kuficha mauzo kwani mnunuaji anaitaji manunuzi kwenye tin yawe mengi kupunguza Kodi
Pia ikiwa hutotoa risiti yamauzo stock kwako itaonekana kubwa sana Jambo ambalo haliingii akilini hence utachunguzwa!
Ujue kupunguza Kodi ni pamoja na kuficha manunuzi halisi, ikiwa manunuzi yatakuwa reflected in your tin huwezi kwepa
 
Back
Top Bottom