Kodi mpya za miamala: Mahakama iweke zuio la haraka

Kodi mpya za miamala: Mahakama iweke zuio la haraka

Hata hivyo kesi itakuwa haina mashiko kwamba unaishitaki Jamhuri kwa Kuanzisha kodi au tozo au? Kwani kodi ni dhambi au ni kinyume na sheria?

Mwambie jamaa alipe kodi hakuna maendeleo ya mkato mkato, Serikali haiwezi kupunguza hili na miamala inaendelea kama kawaida
Mjinga wewe, kodi ama tozo inapaswa kutozwa kwenye faida ama mapato (income) na sio kwenye mitaji.

Zaidi ya yote, huwezi kutoza kodi mbili kwenye muamala mmoja. Hiyo ni kinyume na kanuni za utozaji kodi.

Hakuna kodi inayoitwa kodi ya uzalendo. Huu ni WIZI na UTAPELI.

Ni UHUNI abi initio. Hakuna kitu kama hicho duniani.
 
[QUOTE="Omusolopogasi, post: 39729660, member: 451552]Kumbuka corona ipo na inaua...[/QUOTE]

Hiyo corona iko wapi mbona siioni?
 
Huu uharamia wa kodi mpya za miamala ya simu unapaswa kusimama.

Wanasheria wetu mtusaidie hili. Hakuna kitu kinachoitwa sijui "kodi ya uzalendo" — Lazima Mahakama iweke ZUIO la hizi kodi za kitapeli.

Hauwezi ukakata kodi mara tatu kwenye muamala mmoja. Huo ni uhuni na wizi.

Hizi ndizo kodi za dhulma tulizokuwa tunazisema.

Badala ya kudhibiti madini na bandari pamoja na vitega uchumi vingine vikubwa, mmewaachia wazungu wanajichotea tu, halafu mnatengeneza vijikodi vya ajabu ajabu mnamtwika mwananchi mara tatu tatu?

HAPANA, Double taxation ni uhuni na dhuluma ambayo inapaswa kusimama.

Msituletee mambo ya kuupiga mwingi hapa. Kodi za kitapeli ni mwiko.

Wanasheria fanyeni kazi yenu, na tutaipima mahakama kama bado inajitambua kupitia hili.
Hili kwa kinyakyusa tunaita Regime uncertainty
 
Yani wewe jamaa una akili Sana.Nashangaa Yani watu tupo kama wendawazimu hata kesi tu mahakamani tumeshindwa kufungua hivi Watanzania tuna akili kweli?Tunaumizwa tunakaa kama makondoo . Nimeamini serikali ya Tanzania haipo kwa ajili ya kuwainua Wananchi wake .Wlichikifanya ni zaidi ya uhuni.
watu wanashinda twitter kupiga porojo badala ya kufatilia mambo ya msingi.
 
Hakuna kodi ya uzalendo wewe, usilete ujinga wako hapa.

Tunalipa kodi stahiki na halali, sio kodi uchwara za kitapeli.

Uzalendo ndo nini yaani?
Afu huu uzalendo ni kwa wananchi wa kawaida kwann wao viongozi hawawi wazalendo? Nilitegemea Mwigulu kama waziri wa fedha azuie yale ma viette watumie land Cruiser kupunguza garama za uwendeshaji serikali, then aje kwa mishahara ya wabunge ilimwe kodi, alafu ahamie kwenye madini na bandari atulie
 
watanzania hawana tatizo na makato ila tunacho kitaka ni fedha hizi zisichezewe, isitokee watu kuzidokoa.
serikali iwe makini tu kwenye malengo.
watanzania tuko tayari na tunaendelea kutoa kodi.
kamwe serikali isipumbazwe na kelele za wapinga maendeleo ambao wana dhamiri ya kusumbua awamu hii ya 6.
serikali iwe imara isikubali kuyumba wala kuyumbishwa.

wabunge wetu ambao ndio wawakilishi wetu bungeni wamejadili na kuona umuhimu na faida tutakayo ipata kutokana na kodi hizi.
mjenge nchi ni mwananchi maenyewe.
tusikilize maneneo wanasiasa wasaka tonge.
Acha unafiki mkuu wangu
 
Afu huu uzalendo ni kwa wananchi wa kawaida kwann wao viongozi hawawi wazalendo? Nilitegemea Mwigulu kama waziri wa fedha azuie yale ma viette watumie land Cruiser kupunguza garama za uwendeshaji serikali, then aje kwa mishahara ya wabunge ilimwe kodi, alafu ahamie kwenye madini na bandari atulie
Hawajitambui.
 
Huu uharamia wa kodi mpya za miamala ya simu unapaswa kusimama.

Wanasheria wetu mtusaidie hili. Hakuna kitu kinachoitwa sijui "kodi ya uzalendo" — Lazima Mahakama iweke ZUIO la hizi kodi za kitapeli.

Hauwezi ukakata kodi mara tatu kwenye muamala mmoja. Huo ni uhuni na wizi.

Hizi ndizo kodi za dhulma tulizokuwa tunazisema.

Badala ya kudhibiti madini na bandari pamoja na vitega uchumi vingine vikubwa, mmewaachia wazungu wanajichotea tu, halafu mnatengeneza vijikodi vya ajabu ajabu mnamtwika mwananchi mara tatu tatu?

HAPANA, Double taxation ni uhuni na dhuluma ambayo inapaswa kusimama.

Msituletee mambo ya kuupiga mwingi hapa. Kodi za kitapeli ni mwiko.

Wanasheria fanyeni kazi yenu, na tutaipima mahakama kama bado inajitambua kupitia hili.
Kwenye mahakama ipi? Hatuna mahakama huru Tanzania. Uhuru upi uliopo mahakamani kwa watuhumiwa kukaa mahabusu miaka kwa madai kuwa upelelezi haujakamilika? Uhuru upi wa mahakama kuteuliwa majaji wasio na sifa ?
 
Jamani tunafungua nchi tulieni tumewapa demokrasia pigeni story mitandaoni

Maskini wamerudi kuwa mashetani mamaeeeee

Matajiri piga keleleeee[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Dah inachekesha ila ndo ukweli
 
Mwigulu inatakiwa afukuzwe kazi ,amefeli sana!

Wafanyabiashara wa Xpesa wanasema kamisheni imepungua sana means watu wamepungua waliokuwa wanafanya miamala....Kuna mmoja alikuwa anapata commision hadi laki 6 ila kwasasa ana laki na ushee.
 
Back
Top Bottom