Kodi mpya za miamala: Mahakama iweke zuio la haraka

Kodi mpya za miamala: Mahakama iweke zuio la haraka

Ngoja tuhamasishe mgomo kwa siku moja ili tuone. Je? yale malipo ya serikali ambazo tunayolipa kwa njia ya M-Pesa nayo yanakatiwa kodi?
Jamani hili jambo ni serious ebu vijana muhamasike ikibidi vipi ingieni mitaani kama wazulu hawa jamaa wanatuona minyumbu
 
Wakati haya yanapitishwa bungeni mlikuwa mko kwenye honeymoon ya "mama anaupiga mwingi sana" huku mdemkaji namba moja ni wapinzani na wanamtandao maarufu wakisifia budget akiwemo Edo Kumwembe.

Sasa hao wapinzani ndio walalamishi namba moja juu ya hili! Mlifanikiwa kuweka wananchi kwenye ajenda against JPM ila matokeo ya muda mrefu ni haya.

Chorus juu ya Mwendazake hazina nguvu tena na sasa tunaishi uhalisia! Let's go [emoji124]
 
leo asubuhi nimetoa elfu kumi kama kujaribisha zoezi wamekata 1125 kwa hiyo kilichozidi ni 125 tu KWA DHATI KABISA NIMEFURAHI SANA MAANA MAKATO HAYA YANAKWENDA MOJA KWA MOJA KATIKA KULIJENGA TAIFA LETU, # HONGERA KWA SEREKALI YETU.najaribu kutafakari endapo serekali itaamua kutumia debit card katika mfumo wetu wa kifedha jinsi gani serekali yetu itakuwa na fedha nyingi za kustaajabisha.
 
leo asubuhi nimetoa elfu kumi kama kujaribisha zoezi wamekata 1125 kwa hiyo kilichozidi ni 125 tu KWA DHATI KABISA NIMEFURAHI SANA MAANA MAKATO HAYA YANAKWENDA MOJA KWA MOJA KATIKA KULIJENGA TAIFA LETU, # HONGERA KWA SEREKALI YETU.najaribu kutafakari endapo serekali itaamua kutumia debit card katika mfumo wetu wa kifedha jinsi gani serekali yetu itakuwa na fedha nyingi za kustaajabisha.
Una uhakika gani imeenda kujenga taifa?
 
Wakati haya yanapitishwa bungeni mlikuwa mko kwenye honeymoon ya "mama anaupiga mwingi sana" huku mdemkaji namba moja ni wapinzani na wanamtandao maarufu wakisifia budget akiwemo Edo Kumwembe.

Sasa hao wapinzani ndio walalamishi namba moja juu ya hili! Mlifanikiwa kuweka wananchi kwenye ajenda against JPM ila matokeo ya muda mrefu ni haya.

Chorus juu ya Mwendazake hazina nguvu tena na sasa tunaishi uhalisia! Let's go [emoji124]
Fungate limeisha sasa wamerudi kwenye uhalisia. Acha upigwe mwingi
 
Kiukweli kama wanasheria wote nchi nzima hakuna hata aliyefungua case mpaka sasa kupinga huu uharamia, basi tupo nchi ya ajabu sana inayoenda enda tu watu wamekaa, hii na kwa hali ilivo mtaani ni kutaka kuwalaza watu njaa

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
wanaharakati wao kesi wanazofungua ni kesi za kisiasa tu na zakubumba zisizo na mashiko lakini katika hilo wala hutowaona
 
Huu uharamia wa kodi mpya za miamala ya simu unapaswa kusimama.

Wanasheria wetu mtusaidie hili. Hakuna kitu kinachoitwa sijui "kodi ya uzalendo" — Lazima Mahakama iweke ZUIO la hizi kodi za kitapeli.

Hauwezi ukakata kodi mara tatu kwenye muamala mmoja. Huo ni uhuni na wizi.

Hizi ndizo kodi za dhulma tulizokuwa tunazisema.

Badala ya kudhibiti madini na bandari pamoja na vitega uchumi vingine vikubwa, mmewaachia wazungu wanajichotea tu, halafu mnatengeneza vijikodi vya ajabu ajabu mnamtwika mwananchi mara tatu tatu?

HAPANA, Double taxation ni uhuni na dhuluma ambayo inapaswa kusimama.

Msituletee mambo ya kuupiga mwingi hapa. Kodi za kitapeli ni mwiko.

Wanasheria fanyeni kazi yenu, na tutaipima mahakama kama bado inajitambua kupitia hili.

unataka serikali itoe wap mapato kama hutaki kuchangia? wakikopa mnalalamika basi changieni bado mnalalamika sasa wafanye nn
 
wanaharakati wao kesi wanazofungua ni kesi za kisiasa tu na zakubumba zisizo na mashiko lakini katika hilo wala hutowaona
Wapingane na serikali ili wafungiwe leseni za taaluma yao.
Wachache wanadai katiba wanajua mapungufu yaliyomo.
Pia hakuna wakumshitaki kwa sababu wanakinga kisheria.
 
Wapingane na serikali ili wafungiwe leseni za taaluma yao.
Wachache wanadai katiba wanajua mapungufu yaliyomo.
Pia hakuna wakumshitaki kwa sababu wanakinga kisheria.
kwani kupingana na serikali watakua wameanza leo?siku zote wamekua wakipingana na serikali hawakuujua ubovu wa hiyo katiba?
 
Kama kuna mahali Mh. Rais alikosea ni kuendeleza baraza la yule mtangulizi wake.

Waziri wa Fedha sio Mbunifu.

Tanzania bila mfumo bora wa uongozi hatuwezi kutoboa bila serikali kuwaibia wananchi wengi na kunufaisha wachache.

Wengi wataumia sana kama Farasi dume wa mkoloni. Mkoloni alikua na Farasi dume lisilo na jike wala msaidizi. Muda wote mzungu yupo mgongoni mpaka alipowapata waafrika wa kumbeba mgongoni.
Watawala wasio na mbinu mbadala wanawatumia wananchi kujinufaisha wao kwa madaraka tuu huku wananchi wakiumia.

Kwa sasa ni vikao na semina elekezi kila sehemu.
Utasikia pesa za Tasaf lakini ukijiuliza hiyo Tasafu kwa nini isingekua na ubunifu tu wa kuwatafutia hao maskini ardhi kule Bagamoyo ,Chato, Mkuranga, Mtwara ,Lindi Arusha ,Namanga, Manyara, Dodoma , Mwanza n.k. ikawamilikishia viwanja kama rasilimali zao na familia zao maskini ?
Au kumwapa Hati za umiliki wa maeneo yao bure ili wazitumie kuwekeza badala ya kufanya ujanja ujanja wa kuwapa watu elfu kumi za kununulia kuku mmoja wa kienyeji ambao zamani tulikua tunakwenda kwa mjomba na babu na bibi unapewa kuku unaenda kufuga unapata vifaranga unarudisha kuku wa watu.

Ujanja ujanja ni mwingi unalenga kujinufaisha tu.

Chunguzeni hao wanatumia madaraka yao kuwaumiza wanyonge kwa kujifanya wazalendo ,wao ni mabilionea, wanalindana ,wanaogopa maisha magumu kwenye familia zao. Wanamatumizi makubwa kwa kodi za umma.

Hivi ni nchi gani maskini inaweza kuendelea kwa serikali kuwa na matumizi makubwa kwa kodi ya maskini?
Nchi inaendelea kwa kupunguza matumizi na kuongeza mapato kwenye rasilimali za asili sio kukusanya vipesa vya madafu.

Leo tulitakiwa tuwe Taifa linalouza gesi mpaka Afrika kusini .
Gesi isiyo na suala la Korona kama wanavyofanya Urusi kwa nchi za ulaya.
Badala yake tunawekeza kwenye usafri wa ndani kwa gharama za wanyonge wenyewe huku Rasilali zao za asili zikiwa zimeshikiliwa na watawala wanaosubiri wawekezaji watakaowatumia kuweka hisa zao zinazotokana na mapesa wanayowaibia wanyonge.
Ndio maana Watawala wa awamu ya tano walikua wanaua mitaji ya wafanyabiashara ili baadae wao ndio wawe wawekezaji kwa fedha walizokwapua kwenye maofisi na tenda za kupeana kwenye miradi mikubwa.


Tanzania tumekua na mamlaka nyingi za kukaa ofisini huku zikilipwa mamilioni ya Pesa kwa kodi za kuwaumiza wananchi. Hizi kazi yake ni kuongeza tozo ili wao waishi maisha mazuri na kuwaumiza walaji wa mwisho.
Ewura wakati TBS ipo.
Tozo za miamala wakati VAT ipo.
Sumatra wakati Jeshi la polisi lipo.
Suma JKT wakati JKT na JKU iliundwa kwa ajili ya kujenga nchi na uchumi wa nchi bara na visiwani.
REA wakati Tanesco ipo.
Tarura wakati Halmashauri zipo na Tanroad.
Sijui Tanapa ,Sijui Mamlaka ya Bandari,Sijui ,mawakala wa kukusanya ushuru ,Sijui .
Kila sehemu ni Mamlaka Mamlaka na ukiangalia wao wanajilipa Mishahara mikubwa kuliko wazalishaji na watendaji wanaowajibika moja kwa moja.
Sumatra mfano wapo mikoani tu na hawana uwezo wa kufanya kazi bila Polisi lakini polisi wana mishahara duni kuliko wao. Polisi wana magari Duni kuliko wao. Faini za polisi ni ndogo kuliko zao. Yote ni kuongeza wigo wa rushwa na kujinufaisha na kundi dogo huku kundi kubwa likiumizwa.


Nchi hii inahitaji mjadala mpana na Katiba Mpya ili tupate wawakilishi wa wananchi kwenye Bunge badala ya Bunge la wawakilishi wa kulinda maslahi ya watawala na familia zao.
Bunge la marafiki na familia zao.
Bunge la sasa lipo kwa ajili ya kukutana na kula hata kwa kodi za watanzania huku likipitisha maumivu kwa watanzania.

Tunataka katiba itakayoweka bayana maslahi ya wanyonge ni yapi na haki zao ni zipi na miiko ya uongozi. Utawala bora unaotokana na kura za wananchi ni nguzo kubwa sana.

Watu wanatozwa kodi na tozo nyingi lakini wanaambiwa wajenge shule ,hospitali, wachimbe mitaro ya mabomba ya maji kwa nguvu zao tena ,yani waache kwenda shambani kujitafutia riziki waende kujenga shule lakini shule ikiisha ni mtaji wa mkuu wa wilaya ,mkurugenzi mbunge wa kuteuliwa na diwani wa kuteuliwa. !!
Katiba katiba katiba.
 
hii sasa ndio kampeni mpya ya chadema baada ya kuona katiba mpya imekuwa ndoto za mchana.
ila chadema inazidi kujichafua zaidi kisiasa kwa kuhamasisha mambo ambayo ni kinyume na uzalendo, hakuna anaye shawishika na uhuni huu .
Lione hili nalo lilivyo lijinga, hapa chadema imekujaje?.
 
Back
Top Bottom