Kodi ya majengo kuanza kukatwa kwenye Luku kuanzia Agosti 20, 2021. Je, Serikali imekosa Dira, mbinu zimewaishia?

Kodi ya majengo kuanza kukatwa kwenye Luku kuanzia Agosti 20, 2021. Je, Serikali imekosa Dira, mbinu zimewaishia?

View attachment 1897744

Naomba kuuliza maswali machache...

Ni sababu ipi hasa ya msingi iliyopelekea kutoka mfumo wa malipo wa zamani kuleta mfumo wa sasa?.....
Naomba kujibu

1. Serikali imeondoa mfumo wa zamani sababu ulikuwa rahisi watu kukwepa kulipa na ngumu kukamatwa. Hivyo serikali ilikuwa inapoteza sana mapato. Mfumo mpya ni ngumu kukwepa.

2. Mpangaji halipi Kodi ya nyumba. Hapo ni makubaliano na mwenye nyumba akisema utalupa mwenyewe hama nyumba usikae kulalamika kitu kipo ndani ya uwezo wako

3. Kila chumba kuwa na Mita hayo ni maamuzi binafsi ya mwenye nyumba anaweza kuondoa au akaacha au akanunua sub meters ambazo bill yake haitoki direct TANESCO bali inatokana na mgao unaotoka kwenye main meter.

4. Mpangaji aliyepanga nyumba mbili hapo narudi kwenye jibu langu la pili kuwa mpangaji atabaki kulipa kodi ya pango akilipa kodi ya TRA ni makubaliano yake na mwenye nyumba.

5. Unauliza usiponunua Umeme. Hapo weka vizuri swali lako maana usiponunua Umeme si unalala giza? Au unamaanisha unanunua Umeme labda wa 200k wanakukata 1,000 yao alafu unautumia huo mwaka Mzima? Kama ndivyo utakuwa umewakomoa.
 

Naomba kuuliza maswali machache...

Ni sababu ipi hasa ya msingi iliyopelekea kutoka mfumo wa malipo wa zamani kuleta mfumo wa sasa?...
Hata Kama Ni kutafuta noti kwa nguvu sio hvyo!

Na hayo ndo madhara ya serikali iliyojiingiza madarakani, hawana uchung kabisa na wananchi wao!

Ajira hawatoi, watu kitaa wako hoi, bado unataka umkwapue Hadi sh mbili anazoziangaikia!

CCM mmelaaniwa kwa kweli,!
 
Mbaya zaidi wameongeza hiyo Kodi kutoka 10k Hadi 12k
Huyu bibi hakuna anachojua
Hizo hela kuna watu walikuwa wananufaika nazo sema Magu alikata huo mrija ina maana ni kama maboss wamejirudishia system yao ya kupiga hela 😂!!! Tuna nchi ya ajabu sana
 
Kama Mwanaume nikichangia 12000 Kwa mwaka ili serikali ilete maendelo sioni tatizo ,tuache kulia lia Kama watoto, 12000 ni kitu gani
Yaani nashangaa mtu anapopinga kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yake mwenyewe.
 
Sisiemu wanaturudisha nyuma mpangaji anabeba kodi ya mwenye jengo
Serikali inapiga ndege wawili kwa jiwe moja. Kwanza, kupunguza kusukumana na watu katika kulipa kodi ya majengo. Pia ukusanyaji wake hautakuwa na gharama kubwa. Asante tekinolojia ya mawasiliano.

Pili, kupanua wigo wa walipa kodi kwa vile kila mwenye luku lazima atalipa hiyo kodi. Zimekuwepo hoja kwamba hapa bongo watu wachache wanatwishwa mzigo wa kulipa kodi. Serikali nimejaribu kupata ufumbuzi wa hoja hiyo. Kama kodi ni kubwa (kama inavyosemekana kwenye miamala) au ni ndogo hilo ni suala lingine na linazungumzika.

Kimsingi, serikali (iwe ya CCM, Chadema, act-wazalendo, chauma n.k.) haiwezi kuchochos maendeleo bila kukusanya kodi. Vyanzo gani vya kodi, Wabunge wetu wanatuwakilisha katika kufikia maamuzi hayo (wamepatikanaje hiyo ni hoja tofauti ambayo haihusiani na vyanzo na viwango vya kodi).

Kuhusu mpangaji kulipishwa kodi badala la mwenye nyumba ni suala la maelewano kati ya hao wawili. Kiwango cha kodi kinaeleweka. Hivyo mwenye nyumba anawajibika kumrejeshea mpangaji wake kwa utaratibu watakaokubaliana. Hili siyo jukumu la serikali.
 

Naomba kuuliza maswali machache.

Ni sababu ipi hasa ya msingi iliyopelekea kutoka mfumo wa malipo wa zamani kuleta mfumo wa sasa?...
Hii ni hatari sana. Akili za watawala sasa zinakaribia kufika mwisho wa kufikiri!

Umeme ni huduma ya msingi kwa maisha haipaswi kubeneshwa vikodikodi kama hivi visivyokuwa vya msingi, VAT unakata hata pa kulala mnatoza kosa !! Basi tumekwisha.

Wakoloni weusi wabaya sana kuliko weupe , wacha twende tutafika!

Maana uchokozi imunazidi tutakuja kuelewana mbeleni
 
Ninavyowajua Wapangaji wangu watakaa giza sana sijui itakuwaje ikipitiliza miezi,
 

Naomba kuuliza maswali machache.

Ni sababu ipi hasa ya msingi iliyopelekea kutoka mfumo wa malipo wa zamani kuleta mfumo wa sasa?...
Lengo lao lilikuwa kujikwamua kulipia mighorofa wanayoipangisha na kututwisha sisi mzigo, Mwigulu na wenzake wao umeme wanalipiwa na serikali hivyo kodi haitawahusu kwenye LUKU, kuna watumishi wa vyeo vya juu wanaolipiwa umeme nao pia hawatshusika japo wanamijengo wanapangisha! Hii haikubaliki.
 
Tunavyosema kuwa hii serikali ni inept na imechoka huwa siyo siasa.We mean a business!Imagine mimi naanza kulipa kodi za majengo wakati similiki jengo lolote lile.
 
Itafika kipindi hata ukilala na mkeo nyumbani itabidi ukatwe kodi ya uzalendo
 
natamani nimjue aliyetoa ilo wazo
Hii kitu ni mwigulu nchemba written all over it. Yule jamaa MUNGU amfunike na mabawa ya malaika wake asione tena nafasi za uongozi abakie tu kuwa mwanachama mfu wa ccm.
 
Hii ina maana kuanzia kesho, na itakuwa ni kwa wale wenye majengo tu au hata ukiwa na kiwanja chenye hati unachangia?
wapo lumumba wana tafutia jina kodi yako na njia ya kulipia!
pengine itaitwa kodi ya mazingira!
 
Back
Top Bottom