Ni sawa kodi ni maendeleo ya nchi,bila kupunguza matumizi ya anasa hakika tutapiga hatua mwendo wa konokono.
Manunuzi ya magari mengi ya gharama kubwa L/C V8,Nissan.... ni kaburi la kodi za walipa kodi.
Mikutano,Makongamano,Warsha na safari za hovyo hovyo hakika ni matumizi ya hovyo ya fedha za umma.
Kuuziana Magari ya thamani kubwa ya serekali kwa bei ya nyanya kunawakatisha tamaa walipa kodi.
Serekali ni lazima ibane matumizi si kuongeza na kubuni kila uchao vya kodi.
Kuhusu makusanyo ya kodi naomba kutofautiana na wewe.
Ongezeko la kodi pia linatokana na makusanyo ya TANAPA,TAWA,Ngorongoro kuingizwa kama kodi wakati hizi taasisi zilitakiwa kuachiwa fedha zake na kuilipa gaiwo kama ilivyo bandari,CRDB,NMB,NHC......
Kifupi hesabu za TRA hazina ukweli kwakuwa fedha za TANAPA &Ngorongoro si kodi bali ni mapato ya hizo taasisi.
Nashangaa CAG alishalitolea ufafanuzi suala hili lakini bado serekali inaendelea kuwadanganya wananchi na kuirundukia sifa TRA bila sababu za msingi.
Nina uhakika high season inayoanza mwezi 7 hadi 10 TRA itabebeshwa sifa za uongo kupitia mgongo wa TANAPA & Ngorongoro.
Ngongo kwa sasa Kibanda maiti.