Kodi zetu ndio Maendeleo ya Taifa letu.
Mwaka 2021/22- Trillions 22.2.
Mwaka 2022/23- Trillions 24.1.
Mwaka 2023/24- Trillions 27.6
View attachment 3033852
Mh waziri wa fedha @ Mwigulu, Wananchi wanasema
Hakuna maana yoyote kama mwananchi wa kawaida maisha yake yanaendelea kuwa magumu kila kukicha (bidhaa kupanda bei bila nidhamu, gharama za maisha kupaa, uwezo wa mwananchi kujipatia kipato ama kwa njia mshahara, biashara, kilimo nk ni duni sana) huku ninyi mkinufaika na kodi hizo wanazotoa wananchi.
Watumishi wa serikali na umma wakilipwa mishahara ya anasa, wabunge mishahara na posho juu, kununua magari ya kifahari kwa pesa nyingi, viongozi kusafiri sana nje ya nchi bila uwiano wa kile wanachokileta kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Kodi na tozo nyingi wakati mnapokea mikopo na misaadi lukuki isiyo na impact yoyote kwenye maisha halisi ya Mtanzania.
Kulipa madeni kiwango kikubwa nje tena kwa thamani ya dola huku maendeleo yakichechemea bila matumaini ya kukaa sawa.
Makusanyo hayana manufaa yoyote kwa mwananchi wa kawaida zaidi ya kujinufaisha ninyi wenyewe mlioko kwenye dhamana ya uongozi.
Kikokotoo cha wastaafu au kuacha kazi kisimtese mchangiaji michango kwenye mfuko wa jamii maana ni pesa zake kwanini muwapangie namna ya kupata na kiwango gani wakati ninyi wabunge na viongozi wa kisiasa mnalipwa kwa mkupuo na hamlipi kodi yoyote kwenye vipato vyenu?
Kadri makusanyo ya mapato yanavyoongezeka ndivyo wizi, rushwa, ufujaji na ufisadi unavyoongezeka kupitia watumishi wengi wasio waadilifu kazini ambao mnawafahamu lakini hakuna hatua stahiki zinazochukuliwa dhidi yao zaidi ya kulindana.
1. Kodi kero ziondolewe kwenye vipato vya mishahara na biashara
2. Mishahara watumishi wa serikali, umma na sekata binafsi ziboreshwe kulingana na kupanda kwa gharama za maisha
3. Bidhaa zipunguzwe bei kwa serikali kuweka ruzuku kutoka kwenye kodi za wananchi wanazochanga
4. Kikokotoo kilichopo na kilichorekebishwa bila kushirikisha wachangiaji wenyewe kiondoshwe na kupandishwa hadi asilimia 75% na naksi ya kuishi baada ya kustaafu irekebishwe hadi miaka 18 badala ya 12.5
5. Wanafunzi wanaojiunga chuo kikuu kwa shahada katika fani yoyote wapewe mkopo na sharti ya kwamba mwanafunzi aliyesoma shule ya binafsi kidato cha nne kwamba hana sifa ya mkopo iondoshwe ni ubaguzi
nk...................