Mhe. Waziri, kwanza tunashukuru umeshiriki nasi hapa. Binafsi nina jambo moja ambalo ni nje ya mada hii ila wewe kama Waziri mwenye dhamana linakuhusu.
Mhe, kuna hii mikopo ya online ambayo licha ya kutoza riba kubwa, lakiini wanakiuka mikataba baina yao na wateja wao mfano ni kuanza kudai marejesho siku ya 5 badala ya siku ya 7 tena kwa vitisho na lugha za hovyo. Kibaya zaidi ni kusambaza taarifa zla watu wanaowadai mitandaoni kisa tu mu amechelewa kulipa kwa siku 1 au 2 wakati utaratibu ukichelewa ni kulipa faini sio kumdhhalilisha mteja.
Jambo moja la kushangaza ni nyie kama serikali kushindwa kuyabaini haya makampuni yanayokopesha mitandaoni wakati transactions zao zote za kutoa mikopo na kulipwa/kupokea fedha zao(lmarejesho) hufanyika kwa kutumia mitandao ya simu ya humu nchini(Mpesa, tigo pesa, Airtel money, n.k). Hii ina maana wamesajliwa katika hii mitandao wanatumia Lipa namba na hiki ndio kinachofanyika.
Sasa swali wangu ni hili:
Kama kweli haya makampuni hayana vibali (leseni kutoka BOT), kwanini serikali isiagize mara moja haya makampuni ya simu yaache kushirikiana kibiashara na haya makampuni ya kitapeli?
Au kama kweli mna lengo la kubaini haya makampuni, kwanini Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na BOT, wasiyabane makampuni ya simu yawasaidie kuwapata wenye haya makampuni maana wameyasajili kwenye mitandao yao ya simu.
Ili upate "Lipa namba" ya kampuni kwenye mitandao ya simu, si ni shariti usajiliwe? Na ili usajiliwe, si ni shariti kampuni iwasilishe vielelezo muhimu kama leseni ya biashara, anuani ya makazi, n.k?
Katika hili, Mhe. Waziri, binafsi naona hakuna dhamira ya dhoti ya kupambania na haya makampuni na ndio maana kila siku yanaongezeka wakati serikali na vyombo vyake kama Jeshi la Polisi, TCRA na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi(PDPC) vipo.
Pathetic!