Kodi zetu ndio Maendeleo ya Taifa letu

Mna uliza maswali ambayo huyu jamaa hawezi kuwajibu kamwe. Muhimu ni nyie Watanganyika mjitambue mfanye jambo.
 
Gen Z ya Bongo bado ina options kwahio bongo bado hatujafikia point of no return ila Generation ambayo italeta huku shida ni generation Alpha... sababu kizazi hicho kitakuwa hakina sehemu ya kuita kwao, hakina pension, hakina ujira hivyo they will have nothing to lose..., Ufukara huo tayari ushawakumba vijana wa wengi wa Kenya (neither hope, nor future prospects)
 
Hii ndiyo inasababisha hata moyo wa kulipa hizo kodi ututoke,sijawahi kuelewa kwanini waliojipachika uongozi ktk nchi hii wanabadili magari kila mwaka tena ya thamani kubwa.

Wewe Mwigulu kwanini mnajikuta nyie ni special sana kiasi mema yote ya nchi mnakula nyie na familia zenu hamuwezi mkaamua kuwa tofauti na wengine mkagawa neema kwa wengine?
 
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kama hayo maswali ya members yatajibiwa na huyo jamaa mnayemuita waziri
 
Tatizo mwigulu wewe unaamini unajua kila kitu, jambo baya sana. kuna shule kisha kula uzoefu na akili.
 
Dr. Mwigulu Nchemba trends inavutia na ni kazi zuri... Lakini;

Kuweni na kiasi katika kuamua kodi sio tunakua tunafurahia ongezeko kubwa linalovunja rekodi ya mapato, kumbe huku nyuma tunaacha wadau wanasaga meno(inakua self sabotage).

Kwa afya ya ukuaji wa uchumi jumuishi baina ya Taasi za kiselikari na za binafsi, AZAKI na startups za wajasiliamali wachanga, inapaswa muwe na taarifa sahihi kwa wakati na mahali sahihi zinazo ainisha matabaka mbalimbali ya jamii na hali zao halisi kiuchumi, kutokea hapo sasa kodi ikusanywe kwa fairness.

Hii migogoro na minong'ono ni dalili kwamba kundi hilo limeshindwa kustahimili mzigo uliojuu yao.

Ukipata muda wa spare pitia na huku Kiongozi.
 
Tatizo mwigulu wewe unaamini unajua kila kitu, jambo baya sana. kuna shule kisha kula uzoefu na akili.
Unfortunately vyote hana na aliyemuweka kwenye hiyo nafasi naye hana anachokijua.

Wanapuyanga tu.
 
Wanapoteza muda kuuliza maswali ambayo hayato jibiwa na huyo jamaa. Kifupi hao jamaa wana waona Watanganyika ni wajinga wajinga ndio maana wanafanya watavyo na hamna kitu watafanywa.

Umewahi jiuliza mabilioni ya mikopo wanayo pokea kila uchwao dhamana ni nini na huwa inafanya kazi gani?
Kuna aliyejibiwa swali lake?
 
Huna tofauti ba Waandishi wa habari, wanao pewa muda wa kuuliza maswali Rais wanaanza kumuambia amependeza


Uchawa tu hakuna kingine.

Hapo anajikuta watofauti na mitazamo ya watu ilihali ni vitu ambavyo vipo wazi kuwa Mwigulu ameshindwa kuwa na tija kwa wananchi katika nafasi aliyopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…