Kodi zetu ndio Maendeleo ya Taifa letu

Kuna haja gani kwa nchi masikini kama hii kuwa na mtumishi wa umma analipwa zaidi milioni mbili kwa mwezi kama siyo ubinafisi na ufisadi? matumizi ya anasa na makubwa ya hovyo pamoja na wizi wa mali za umma.
 
Kuna haja gani kwa nchi masikini kama hii kuwa na mtumishi wa umma analipwa zaidi milioni mbili kwa mwezi kama siyo ubinafisi na ufisadi? matumizi ya anasa na makubwa ya hovyo pamoja na wizi wa mali za umma.
Wewe unaona TShs. 2milioni ni mshahara mkubwa??? Watu wanakusanya mamilioni ya fedha kila mwezi, halafu wewe unazungumzia Milioni mbili!!?
Wapo baadhi ya maafisa wa Serikali kila mwezi wanakusanya zaidi ya Tshs. 24milioni zikiwa kama ni Malipo ya posho tu ya mwezi mmoja, mbali na mshahara wake wa kila mwezi.
 
~~~Ongezeni taratibu nzuri zaidi katika mikopo ya wanafunzi wa vyuo, kwani fedha nyingi zinapotea kwa kushindwa kuajiri wahitimu aidha wengi kutokomea, zidisheni conditions, kwa ajili ya kupata mikopo hiyo, ikiwemo udhamini wa mashamba, mali mbalimbali na vinginevyo visivyohamishika ili kulazimisha wahitimu hao kurejesha fedha za umma. ~~~~
 
Ndiyo hayo mkuu sasa tunaongea hiyo milioni 24 ingeweza kuajiri watanzania 48@500,000 badala ya kulipa mtu mmoja na badala lake tungepunguza tatizo la ajira kwa ndugu zetu sehemu kubwa sn, tena hawa wangejituma kupita kiasi, huyo anayelipwa milioni 24 unaweza kukuta kazi yake kubwa ni kuzunguka kwenye vikao badala ya kuzalisha. Shame on us
 
Kodi zetu ndio Maendeleo ya Taifa letu.

Mwaka 2021/22- Trillions 22.2.
Mwaka 2022/23- Trillions 24.1.
Mwaka 2023/24- Trillions 27.6

Mhe. Dr. (Ph.D), binafsi nimefarijika sana na rejeo lako JF. You might be the highest GOT high rank official, to appear humu jf in person, this is the type of boldness we need it up there!. Kuna kitu niliwahi kusema kukuhusu wewe, Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa! kitu hicho bado unacho and the room is still there, and the door wide open.
Thanks for being who you are.
P
 
Hapa umeleta takwimu za makusanyo. Kesho tunaomba za matumizi ya hovyo na zinazoibwa wakati wa kutumia. Au bado unasimamia kauli yako hakuna wizi serikalini?
Matumizi ya Hovyo ndio yakoje hayo? Serikali si Ina matumizi ya Fedha clear kabisa kwenye Bajeti Kuu inaonesha na Bajeti za Kila Wizara.
 
Kwani Kila ongezeko la watu manake ni ongezeko la walipa Kodi? Poor reasoning 😁😁
 
Hawezi kuja kujibu Kila mtu hapa ila Mimi naweza kujibu Baadhi ya sababu .
1.Mama amefungua Nchi,ishu ya kwanza kabisa ilikuwa kurejesha Imani ya wawekezaji na wafanyabiashara Kwa Serikali na mnakumbuka hatua mbalimbali zilifanyika ikiwemo ziara za Nje,kurudisha pesa za walioporwa na kuacha kutumia task force au kufungua accounts.Waliofungiwa accounts Kwa Sasa ni wale wanaodaiwa.

2.Utalii.Ishu ya Royal tour imeirejesha Tzn kwenye ramani ya Utalii,ni sekta imefanya vizuri Sana na kuweka rekodi kubwa kuwahi tokea.

3.Sekya ya Madini.Sekta ya Madini imekua sana awamu hii ya sita Kwa sababu ya uratibu mzuri,udhibiti na kuwajali wawekezaji wadogo na wakubwa.Mfano wawekezaji wadogo wamepewa Mitaji,umeme na mitambo Baadhi ya maeneo.

4.Sekta ya Ujenzi,viwanda na Uchukuzi imeimarika sana awamu ya 6.

5.Kekta ya Kilimo.Licha ya kwamba Bado inachangia kiwango ambacho sio kikubwa sana ila imechangia zaidi ya hapo awali.

Mazao kama ufuta,avocado,mazao ya nafaka na ya biashara hasa tumbaku yameleta pesa nyingi sana Nchini Kwa sababu ya sera na uwekezaji wa Serikali kwenye kilomo.Kumbuka mama ameweka pesa mara dufu kwenye Kilimo.

Kwa maoni yangu nilivyofuatilia nimebaini sekta hizo ndio maana mabenki na bima wamepata mabilioni Kwa mabilioni ya faida kushinda wakati mwingine wowote.
 
Umejitahidi kujibu swali la kwanza Mkuu, japo hujawasilisha jibu la swali la pili.

Kwamba pamoja na makusanyo hayo makubwa ya Kodi, kwanini tunaendelea kukopa?
 
Mkuu Mwigulu hebu hizi kodi ziweke kwa dola katika miaka yake jinsi rate ya dola ilivyokuwa. Unaweza ukute hakuna kilichoongezeka isipokuwa shilingi imeshuka thamani tu na tena unaweza kuta mwaka 2021 tulikusanya zaidi kuliko 2023......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…