Kofi Annan, Luis Ocampo na Thabo Mbeki waombwe kusuluhisha vyama vya siasa Tanzania

TIASSA,

..Mzee Thabo Mbeki ni mzima wa afya.

..hapa anatoa ushauri wake kwa Raisi mpya wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.

Una akili finyu wewe! Mimi na huyo fisadi lowassa wapi na wapi!? Usilazimishe vitu ambavyo haviko. UZWAZWA wako mwisho lumumba siyo humu.

Ile pesa aliyopewa Mbowe ili CCM wasimamishe mgombea kupitia chama chetu haikutoka kwenye kodi zetu?
Mbona kuna mamburula humu ndani yanaona sawa tu?
 
too low
 
Una akili finyu wewe! Mimi na huyo fisadi lowassa wapi na wapi!? Usilazimishe vitu ambavyo haviko. UZWAZWA wako mwisho lumumba siyo humu.
Kwa hiyo una maana mwenyekiti alikuwa anapiga hela tu.
 
..hivi kwa hapa tulipofika bado kuna watu hawaamini kwamba tunahitaji msaada toka watu ambao ni NEUTRAL watusaidie kurejesha masikilizano nchini?
 
Hakuna cha kusuluhisha hapa Tz kwa sababu hakuna mgogoro wowote unaohitaji suluhu. Ni suala la wapinzani kubadilisha namna ya kufanya siasa na serikali iliyopo na watambue kwamba kwa vyovyote vile utawala wa JK hauwezi kuwa sawa na wa JPM kwa namna yoyote iwavyo.
 
..sawa.

..wapinzani wanatakiwa wabadilike.

..lakini naamini watawala, na haswa Raisi Magufuli, wanatakiwa wabadilike.

..katika mazingira hayo anatakiwa msuluhishi au wasuluhishi ku-facilitate hizo pande mbili kubadilika.
 
Kusuluhisha ili iweje?Ccm wanapaswa kuvifuta kwa njia ya kistaarab bungeni na si kwa njia hii ya sasa!
Sioni kama kuna tatizo,kwani kuliko kuwa na maigizo ya vyama vingi,ni bora visiwepo kabisa ili ccm ambao wako milioni 12, wafaidi kwa niaba yetu tusio na vyama.
 
..sawa.

..wapinzani wanatakiwa wabadilike.

..lakini naamini watawala, na haswa Raisi Magufuli, wanatakiwa wabadilike.

..katika mazingira hayo anatakiwa msuluhishi au wasuluhishi ku-facilitate hizo pande mbili kubadilika.
Magufuli abadilike ili aweje? Wa kubadilika ni hawa ambao wanatakiwa kushindana na mtu mwenye style tofauti na waliyekuwa wanashindana naye awali ambaye ni JK. Wanaolia lia ndo hao wa kubadilika.
 
Magufuli abadilike ili aweje? Wa kubadilika ni hawa ambao wanatakiwa kushindana na mtu mwenye style tofauti na waliyekuwa wanashindana naye awali ambaye ni JK. Wanaolia lia ndo hao wa kubadilika.

..Magufuli ana imani kwamba kila anayemkosoa anamtukana au halitakii mema taifa letu.

..sasa kila anapokosolewa anapandwa hasira, na kwasababu yeye ni amiri jeshi mkuu, vyombo vya dola navyo vinaambukizwa hasira na kupelekea kuumiza watu wa upinzani na hata wasiohusika mfano Aquilina Akwilini.

..Kwa hiyo Magufuli anatakiwa abadilike ili siasa zetu ziwe za amani na zisiingiliwe na vyombo vya dola.
 
Kama mmeshindwa kuwatii wazazi wenu (baba na mama) mtawatii majirani zenu? Kuna aliye bora kuliko baba na mama hapa duniani?
 
Kama mmeshindwa kuwatii wazazi wenu (baba na mama) mtawatii majirani zenu? Kuna aliye bora kuliko baba na mama hapa duniani?

..wazazi lazima waheshimiwe.

..lakini wapo wazazi wanaopoteza heshima ya watoto wao kutokana na wao wazazi kutojiheshimu na kutokuonyesha upendo kwa watoto.

..katika mazingira hayo majirani wana wajibu wa kuingilia kati ili kurejesha heshima, upendo, na masikilizano, ktk familia husika.

..
 
Kweli mkuu, Kwa wote hao hakuna atakaye rudi bungeni. Kwani kwa hali ilivyo hakuna cha kura,ni kutanganza wapendwa tu kama chaguo za marudio.
 
Unaona kuua ni sawa tu.Mwenyezi Mungu akusaidie.
 
Acheni ujinga, Tz kuna nini cha kusuluhisha?? Kuna mambo ya maana wanatakiwa kufanya sio huu upuuzi wa hapa.
Tatizo mnadhani Tz ndio dunia, hapa hamna kitu jawana muda wa kupoteza ndio maana UN licha ya kuwa na wawakilishi wake hapa, wako bize na mambo mengine.
 
Kama yupo mzazi anayemruhusu mwanae kuvuta ile kitu huyo siyo riziki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…