Kombe la dunia lakuza uchumi wa Tanzania

Kombe la dunia lakuza uchumi wa Tanzania

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Kama tunakumbuka vizuri Rais Samia Suluhu alifanya ziara ya kikazi nchini Qatar na akafanikiwa kudumisha mahusiano mazuri ya kibiashara (Diplomasia ya uchumi) baada ya ziara hiyo Tanzania tumenufaika zaidi katika biashara mbalimbali ikiwemo ya uuzaji nyama katika nchi hiyo ya kiarabu.


Tanzania imefanikiwa kuvuna Tsh Bilioni 12.5 kutokana na Kombe la Dunia.
Usafirishaji nyama kwenda Qatar umeongezeka kwa asilimia 125.
Oktoba 2022: Tani 632
Novemba 2022: Tani 1,423
Asilimia 37 ya nyama yote ambayo Tanzania iliuza nje, ilikwenda Qatar.

Chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu fursa nyingi za kibiashara zinaendelea kujitokeza.
 
Wao Qatar watafanya lini ziara Tanzania ili kudumisha mahusiano?
 
Tanzania imevuna TZS Bilioni 12.5 kutokana na Kombe la Dunia, Usafirishaji na uuzaji wa nyama kwenda Qatar umeongezeka kwa 125%. Oktoba mwaka huu Tani 632 ziliuzwa na Novemba Tani 1,423 ziliuzwa. Qatar inaingiza nyama nyingi kutoka Tanzania hususani nyama ya Mbuzi.

Ikumbukwe mapema mwaka huu Rais Dkt. Samia Suluhu alifanya ziara yake Qatar, Saudi Arabia na Oman ambako nchi hizi zote ni wanunuzi wa nyama kutoka Tanzania. Serikali imeendelea kuboresha sekta ya mifugo nchini ili kuendelea kuuza zaidi kimataifa kwani mbali na Qatar nchi ya Tanzania inapeleka nyama katika mataifa ya Oman, United Arabs Emirates(UAE), Saudi Arabia na Bahrain.

Kufunguka kwa masoko ya kimataifa yanasaidia kukua kwa uchumi wa nchi na kuongezeka kwa pato la taifa. Wafanyabiashara wanapata fedha na wafugaji pia wanapata zinazowasaidia kuimarisha maisha yao.

kuongezeka mauzo ya nyama.jpg
 
07 December 2022

Mauzo: Meli Kuondoka Bandarini Lamu​

NA KALUME KAZUNGU

MELI inayostahili kusafirisha mifugo kutoka bandari ya Lamu hadi taifa la Oman imechelewa kung’oa nanga, kutokana na changamoto zilizoibuka kufikisha ngamia bandarini.


Ni mwezi mmoja sasa tangu meli hiyo MV Banyas 1 kuwasili kwa mara ya pili katika bandari ya Lamu kuchukua mifugo wanaopelekwa ng’ambo.MV Banyas 1 ilitia nanga Novemba 5, 2022 na ilifaa kuanza safari ya kuelekea Oman baada ya majuma mawili.

Katika shehena yake ni takriban mifugo 7,000 wanaojumuisha ngamia 1,000, mafahali 300 na mbuzi na kondoo 6,000.

Meneja Msimamizi wa Mizigo Bandarini Lamu, Bw Peter Masinde, alisema changamoto za kuleta ngamia kutoka kaunti kama vile Wajir na Garissa hadi Lamu ndizo zimechelewesha safari.

Wenye ngamia wanalazimika kutembea na mifugo wao hadi Lamu kwani kuna wanakabiliwa na tatizo kuwabeba kwa malori.

Bw Masinde alieleza kuwa juhudi zinaendelea kuhakikisha idadi ya wanyama waliopangwa kusafirishwa katika awamu hii ya pili, inatimizwa wiki hii ili meli iondoke.

mv-banyas-1.jpg
Meli ya MV Banyas 1 ikiwa imetia nanga bandarini Lamu. Meli hiyo ilifunga gati Novemba 5, 2022. PICHA | KALUME KAZUNGU
Kufikia Jumatatu, jumla ya ngamia 800, mafahali 580 na mbuzi na kondoo 3,000 tayari walikuwa wamefikishwa bandarini huku shughuli ya kuwapakia melini ikiendelea.

Biashara ya usafirishaji wa mifugo hadi mataifa ya nje kupitia bandari ya Lamu ilizinduliwa Oktoba 2022.

Shehena ya kwanza iliyoelekea Oman ilikuwa takriban mifugo 16,000 waliojumuisha mafahali 200 na mbuzi na kondoo 15,400.

Wakati wa safari hiyo, MV Banyas 1 ilisubiri bandarini Lamu kwa juma moja pekee.

Meli hiyo iliwasili Ijumaa, Oktoba 14, na kufikia Ijumaa iliyofuata, Oktoba 21, ilikuwa tayari imeng’oa nanga kuelekea nchini Oman.

Meneja wa mradi wa miundomsingi wa Lamu, maarufu Lapsset, katika ukanda wa Pwani, Bw Salim Bunu, jana alisema wafugaji wamepata afueni kwani awali walipata hasara tele kwa kukosa soko wa mifugo wao, walioishia kuangamizwa na kiangazi.

“Biashara inayoendelea ya mifugo imewainua wafugaji si Lamu pekee bali ukanda mzima wa kaskazini mwa Kenya,” akasema Bw Bunu
Source : Mauzo: Ngamia wachelewesha meli kuondoka bandarini Lamu – Taifa Leo
 
14 October 2022
Lamu, Kenya

Meli ya mifugo kufanya safari za ghuba toka Lamu



Meli ya Mv Banyas One imetia nanga katika bandari ya Lamu kaunti ya Lamu nchini Kenya ili kupakia mifugo na kuisafirisha nchini Omani.

Mafahali wa ng'ombe 200 pamoja na kondoo na mbuzi elfu 15,400 wanatarajiwa kusafirishwa na meli hii hadi Omani
 
Tanzania imevuna TZS Bilioni 12.5 kutokana na Kombe la Dunia, Usafirishaji na uuzaji wa nyama kwenda Qatar umeongezeka kwa 125%. Oktoba mwaka huu Tani 632 ziliuzwa na Novemba Tani 1,423 ziliuzwa. Qatar inaingiza nyama nyingi kutoka Tanzania hususani nyama ya Mbuzi.

Ikumbukwe mapema mwaka huu Rais Dkt. Samia Suluhu alifanya ziara yake Qatar, Saudi Arabia na Oman ambako nchi hizi zote ni wanunuzi wa nyama kutoka Tanzania. Serikali imeendelea kuboresha sekta ya mifugo nchini ili kuendelea kuuza zaidi kimataifa kwani mbali na Qatar nchi ya Tanzania inapeleka nyama katika mataifa ya Oman, United Arabs Emirates(UAE), Saudi Arabia na Bahrain.

Kufunguka kwa masoko ya kimataifa yanasaidia kukua kwa uchumi wa nchi na kuongezeka kwa pato la taifa. Wafanyabiashara wanapata fedha na wafugaji pia wanapata zinazowasaidia kuimarisha maisha yao.

View attachment 2451806

 
Ipo haja ya uharaka kabisa serikali kujenga bandari itakayokuwa mazingira na gati maalum kwa ajili ya kunenepesha, kudunga chanjo za wanyama ili wasafirishwe kwa meli kwenda ngambo.

Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na wingi wa mifugo barani Afrika lakini haina miundombinu wezeshi ya kuswaga ngombe toka Shinyanga, Lindi, Ihefu n.k hadi pwani wakanenepeshwa na kisha kusafirishwa kwenda soko la kimataifa Arabuni na kwingineko.



Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya mwaka wa Kilimo 2019 / 2020

3.3 Mifugo
Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya mwaka wa kilimo 2019/20 ilihusisha aina mbalimbali
za mifugo inayofugwa nchini. Aina kuu za mifugo iliyoainishwa katika taarifa hii ni ng'ombe,
mbuzi, kondoo, nguruwe na kuku. Taarifa kuhusu idadi ya mifugo zilikusanywa kama ilivyokuwa tarehe 1 Agosti 2020, na taarifa nyingine za mifugo zilikusanywa kwa kufuata mwaka wa kilimo wa 2019/20.

Matokeo ya Sensa yanaonesha kuwa, idadi ya ng’ombe ilikuwa milioni 33.9. Kati ya hao, wakulima wadogo walikuwa na ng’ombe milioni 33.8 na mashamba makubwa yalikuwa na ng’ombe 142,968.

Aidha, wakulima wadogo walikuwa na mbuzi milioni 24.5 na mashamba makubwa mbuzi 33,847. Kwa upande wa kondoo, wakulima wadogo walikuwa na kondoo milioni 8.5 na mashamba makubwa kondoo 24,075....na kuku milioni 75.1 na mashamba makubwa yalikuwa na kuku milioni 12.5 (Jedwali Na. 3.14).

Idadi ya ng’ombe iliyoripotiwa Tanzania Bara ni milioni 33.7 na Tanzania Zanzibar ni 270,998;
Idadi ya mbuzi Tanzania Bara ilikuwa milioni 24.5 na Tanzania ...
Source :
National Bureau of Statistics
National Bureau of Statistics - Home › machapisho
Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20
 
30 August 2022
Lamu port
Kenya

KENYA YAJIZATITI SOKO LA MIFUGO KIMATAIFA

Eneo tengefu la kupokea mifugo 500,000 kwa wakati mmoja tayari kuelekea bandari ya Lamu Kenya,

Mwaka jana nchi ya Kenya imeingia mkataba mpya wa kusafirisha mifugo 500,000 kwenda Oman. Ni baada ya mkwamo wa miaka 16 toka mara ya mwisho Kenya isafirishe bidhaa hiyo kwenda Oman.


The Kenya Ports Authority has set up a dedicated livestock bay at the Port of Lamu that will act as an inspection zone for exports. Officials say they want to leverage on the proximity of Lamu to northern parts of Kenya and the Middle East market to increase livestock exports.
 
22 November 2017
Bagamoyo, Tanzania

RANCHI YA MIFUGO YA MH. HUSSEIN BASHE
Mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe asifika kama mkulima mfugaji Tanzania

 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] ndio yale yale, hata ukiwa na cherehani moja Basi una kiwanda[emoji1787][emoji1787]
 
Samia nchi imemshinda ndugu zangu mbona mnalazimisha sana vihabari uchwara mara uchumi, sijui Tanzania imekua ya ngapi kwenye nini Africa, huyu nae tunauza nyama kombe la dunia,
 
Samia nchi imemshinda ndugu zangu mbona mnalazimisha sana vihabari uchwara mara uchumi, sijui Tanzania imekua ya ngapi kwenye nini Africa, huyu nae tunauza nyama kombe la dunia,
Sukuma gang, hamna jema, kila kitu chema kwenu kibaya tu dah, kuweni na shukurani.
 
Back
Top Bottom