Wildchild
JF-Expert Member
- Aug 29, 2018
- 19,411
- 21,938
Hasa akiwa kwenye SII hasa🏃Mr Dudumizi unajua kusifia!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hasa akiwa kwenye SII hasa🏃Mr Dudumizi unajua kusifia!
Kivipi mkuu, au kwa vile wazungu hawakuwahi kuliweka kwenye ile Big 5 kwahiyo ndo maana unamchukulia poa. Ila ni sawa, wazungu walishindwa kumuweka kwa Big 5 kwa sababu wanyama hawa hawapatikani kwao ulaya. Laiti wangepatikana ulaya basi leo mnyama huyu angekuwa habari nyingine. Mnyama kama cheetah ambae ni mchumba tu mbele ya hili dubwasha kawekwa kwenye Big 5 afu linalostahili hiyo nafasi kaweka nje ya Big 5.Mr Dudumizi unajua kusifia!
Hahaha.. mimi ni mzalendo, kwahiyo kote nipo mkuu 😂😂😂.Hasa akiwa kwenye SII hasa🏃
Kenge peke yake kumkimbiza shughuli, ije kuwa dubwasha kama hili lisilojulikana kama ni mamba, kenge, nyoka, mjusi au mnyama wa aina gani?
Kijana anazungumzia mjusi kafili huyo. He have no idea about this dubwasha hatari zaidi duniani.
Wala haujakosea mkuu.
Nalijua sana niko siriuzi sitanii,ila hayo kwa kwetu tz hayako,hilo hata ukiingia you tube tunauaona pembezoni mwa bahari au mto linavizia mnyama akija kunywa maji linaenda kimya kimya linang'ata mguu karibu na kwato alafu unaona linalala chini linatulia yule mnyama akikimbia kama mita 5 hivi mbele unaona anachechema huku anakosa nguvu miguu inakuwa mizito mara analala hapo hapo hilo dude linaenda linatoboa sehemu laini kama tumboni hivi fasta linaingiza kichwa linanyofoa maini mapafu na moyo kabisa linameza na baadhi ya nyama laini.hawa wanyama wadogo dogo kama mbwa mtoto wa mbuzi paka nyani mdogo au ngedere wao wanamezwa wazima wazima hadi manyoya na ngozi kabisa.ki ukweli hilo lijamaa ni hatari sana hata mtoto mchanga analiwa
Anapatikna wapi tumle supu!
Huyo dawa yake ni AK 47
Hakika wewe ni mfuatiliaji wa animals, mimi pia ni mpenzi sana wa NAT GEO WILD
Hivi unawajua vzr waHadzabe? [emoji38][emoji38][emoji38] Huyu anachomwa vzr anakaushwa anawekewa munyu anakorea anapigwa[emoji23][emoji23][emoji23] mkuu hili dubwasha ulione hivi hivi pichani. Usimbe livamie kijiji, litauwa wanyama, mifugo na wanaofuga wote kwa pamoja.
Ya na mimi nimeshaiona hiyo.Niliona moja ivi akimgonga nyati maji hadi kufa
Hapo kwenye meno kwa kweli sina idea yoyote. Maana akimng'ata mtu mfano mguuni lazima amchane au amtoboe mguu. So sijui anatoboaje toboaje. Pengine ana meno ila madogo madogo sana kama msumeno.Hana meno bhana ni kama kenge yeye ana magego magumu anachana shimo anavuta zile nyama laini za tumboni kama maini mapafu moyo na utumbo nyama kama nyama ile ngumu yenye ngozi hawezi ing'ata hadi kuikata kama tunavyoona simba chui au fisi
Hahaha. Wahadzabe nawajua, ni mabingwa kweli kwa namna yao, lkn mwamba hili dubwasha sifa zake ni zaidi ya vile unavyofikiria wewe. Huyu kuna video flan alimkuta sijui kobe mkubwa au kasa yule nchi kavu. Akaenda na kuanza kutafuta jinsi ya kumla. Alivyoona lile jumba la kobe linamuingizia usiku kula kitoweo chake basi jamaa alimeza vyote kobe na jumba lake kwa pamoja. Na baada ya hapo nikakaa nione kama litapata madhara yoyote kwa kumeza lile jumba.Hivi unawajua vzr waHadzabe? [emoji38][emoji38][emoji38] Huyu anachomwa vzr anakaushwa anawekewa munyu anakorea anapigwa
Ya na mimi nimeshaiona hiyo.
Afu eti mtu anakuja kuleta habari za nyoka koboko ambae anadhibitiwa hata na yule nguchiro anaeitwa mangoose.
Hili dubwasha linaweza kuwameza mangoose na koboko wake pamoja kwa muda wa dakika 3 tu aisee.
hawezi kuwemo kwenye kundi la wababe wa mwituni, kwasababu hapambani, yeye hushambulia kwa kushtukiza na kutimua mbio (kujihami)Kisha baada ya muda ndio hufuatilia windo lake kwa tahadhari ya hali ya juu.Kenge kwa kizungu anaitwa lizard, huyu anaitwa Komodo dragon.
Kwahiyo ni vitu viwili tofauti. Ni mfano umwite Tiger, Leopard au Cheetah (chui) paka eti kwa vile wanafanana muonekano wao. Hili dubwasha limeshindwa kupewa heshima na wazungu kwa sababu halikuwahi kuishi huko kwao ulaya. Hili lidubwasha lingekuwa linapatikana ulaya na Afrika basi lisingekosa kuwekwa katika wale tano bora ya wanyama hatari duniani. Kama chui ambae ni mchumba tu amewekwa kwenye list vipi hili dubwasha lenye uwezo wa kuangamiza kiumbe chochote hapa duniani anyimwe heshima hiyo ya tano bora?
HaHabari zenu wana JF wenzangu.
Leo nimekuja na mada inayohusu mnyama hatari kuliko wanyama wote duniani anaitwa Komodo dragon.
Mnyama huyu ana uwezo wa kuua wanyama wengine hatari kama vile
1) Tiger
2) Simba
3) Leopard, Cheetah (chui)
4) Mamba
5) King cobra, Black mamba nk.
6) Honey badger pamoja na uwezo wa kuishi karibu na wanyama wakali, lakini hawezi kufanya mzaha huo mbele ya Komodo dragon aisee atamezwa yeye na manyoa yake. Jamaa hana masihara na mnyama mwingine yoyote.
Komodo dragon ana venom (sumu kali) kuliko mnyama yoyote hapa duniani. Akiuma mara moja tu inatosha kumaliza mchezo. Hata iwe Tembo, kifaru, kiboko, simba nk hawawezi kufikisha dakika 5 bila kuanguka chini na kupararaizi, kisha Komodo anajivuta taratibu kuja kula nyama.
Haijalishi hapo mnyama atakuwa ameshakufa au bado anapumua, Komodo atachofanya ni kuanza kumtafuna mzima mzima huku anayetafunwa anamuona. Kwa vile atakuwa ameshapararaizi basi mshambuliwa hatokuwa na nguvu ya kumfanya chochote Komodo.
Mnyama huyu hata sumu ya koboko haimdhuru kutokana na aina ya uumbwaji wake ulivyo, ila yeye ya kwake inamdhuru koboko kwa sekunde tu, kwanza anaweza kummeza kwa sekundi 10 bila hata kutumia venom (sumu) yake.
Kwa upande wa binadam sometimes unaweza kuumwa na Simba, Tiger, Leopard, Mamba nk ila ukawa jasiri na kufanikiwa kujiokoa na kutoka nduki kuokoa maisha yako.
Ila mzee Komodo yeye akishakupiga jino basi ujue ni bye bye maana kama ukibahatika sana itachukua ni dakika 3 au 5 kuiaga dunia na pengine mzee wa kazi atakuja akutafune ukiwa bado hujafa hadi atakumaliza na kukumeza wewe wote.
Huyu mnyama akishakupiga jino hukaa pembeni umbali kidogo wa ulipo halafu anakusikilizia. So unaweza kutoka nduki ukidhani umepona kumbe dakika mbili au tatu za mbele utaanguka na kuanza kuishiwa nguvu, hapo ndo mzee wa kazi ataanza kukufuata huku akitumia pua yake kunusa kila sehemu uliyokanyaga hadi atakukuta ukiwa hoi na yeye au wao wakumalizie kabisa.
Huyo ndio Komodo dragon mbabe wa wababe wote duniani. Japo wengi huku Afrika hawamjui kutokana na wanyama hao kupatikana zaidi katika bara la Asia.
View attachment 2321342View attachment 2321345
Labda kengeNiliwahi mkuta kichakani nikamkimbiza huku mkononi nimeshika ndala moja alitoka baru hadi akaingia shimoni
Hahaha.. mzee wa kazi kwenye eneo lake la kujidai
Sijui ka unaelewa nini maana ya neno jamii ya..au kwa hio tuseme chui ni paka tofauti ni ukubwa maumbo kutokana na walipo ..kwamba chui yuko porini na paka anazunguka kwenye ma bar huku? Au tuseme chui ni duma tofauti maumbo? NO ni jamii moja ila ni aina mbili tofautiJama nshaangslia huyo mnyama kwenye national geographic. Kwa kifupi ni kenge. Ukubwa ni kutokan na maeneo