Komodo dragon ndio mnyama hatari zaidi kuliko Black mamba (koboko), Simba, Mamba, Tiger na wanyama wengine wa aina hiyo

Kivipi mkuu, au kwa vile wazungu hawakuwahi kuliweka kwenye ile Big 5 kwahiyo ndo maana unamchukulia poa. Ila ni sawa, wazungu walishindwa kumuweka kwa Big 5 kwa sababu wanyama hawa hawapatikani kwao ulaya. Laiti wangepatikana ulaya basi leo mnyama huyu angekuwa habari nyingine. Mnyama kama cheetah ambae ni mchumba tu mbele ya hili dubwasha kawekwa kwenye Big 5 afu linalostahili hiyo nafasi kaweka nje ya Big 5.
 
Hasa akiwa kwenye SII hasa๐Ÿƒ
Hahaha.. mimi ni mzalendo, kwahiyo kote nipo mkuu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚.
Kuna mwamba wa bawacha kaanzisha uzi kuhusu bavicha.

Ila tulioingia kuangalia na kusoma ni wachache sana.
Hii inaonesha ni jinsi gani watu hawajishughulishi na si hasa tena ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Kijana anazungumzia mjusi kafili huyo. He have no idea about this dubwasha hatari zaidi duniani.

Nalijua sana niko siriuzi sitanii,ila hayo kwa kwetu tz hayako,hilo hata ukiingia you tube tunauaona pembezoni mwa bahari au mto linavizia mnyama akija kunywa maji linaenda kimya kimya linang'ata mguu karibu na kwato alafu unaona linalala chini linatulia yule mnyama akikimbia kama mita 5 hivi mbele unaona anachechema huku anakosa nguvu miguu inakuwa mizito mara analala hapo hapo hilo dude linaenda linatoboa sehemu laini kama tumboni hivi fasta linaingiza kichwa linanyofoa maini mapafu na moyo kabisa linameza na baadhi ya nyama laini.hawa wanyama wadogo dogo kama mbwa mtoto wa mbuzi paka nyani mdogo au ngedere wao wanamezwa wazima wazima hadi manyoya na ngozi kabisa.ki ukweli hilo lijamaa ni hatari sana hata mtoto mchanga analiwa
 

Hakika wewe ni mfuatiliaji wa animals, mimi pia ni mpenzi sana wa NAT GEO WILD
 
[emoji23][emoji23][emoji23] mkuu hili dubwasha ulione hivi hivi pichani. Usimbe livamie kijiji, litauwa wanyama, mifugo na wanaofuga wote kwa pamoja.
Hivi unawajua vzr waHadzabe? [emoji38][emoji38][emoji38] Huyu anachomwa vzr anakaushwa anawekewa munyu anakorea anapigwa
 
Niliona moja ivi akimgonga nyati maji hadi kufa
Ya na mimi nimeshaiona hiyo.
Afu eti mtu anakuja kuleta habari za nyoka koboko ambae anadhibitiwa hata na yule nguchiro anaeitwa mangoose.
Hili dubwasha linaweza kuwameza mangoose na koboko wake pamoja kwa muda wa dakika 3 tu aisee.
 
Hana meno bhana ni kama kenge yeye ana magego magumu anachana shimo anavuta zile nyama laini za tumboni kama maini mapafu moyo na utumbo nyama kama nyama ile ngumu yenye ngozi hawezi ing'ata hadi kuikata kama tunavyoona simba chui au fisi
Hapo kwenye meno kwa kweli sina idea yoyote. Maana akimng'ata mtu mfano mguuni lazima amchane au amtoboe mguu. So sijui anatoboaje toboaje. Pengine ana meno ila madogo madogo sana kama msumeno.
 
Hivi unawajua vzr waHadzabe? [emoji38][emoji38][emoji38] Huyu anachomwa vzr anakaushwa anawekewa munyu anakorea anapigwa
Hahaha. Wahadzabe nawajua, ni mabingwa kweli kwa namna yao, lkn mwamba hili dubwasha sifa zake ni zaidi ya vile unavyofikiria wewe. Huyu kuna video flan alimkuta sijui kobe mkubwa au kasa yule nchi kavu. Akaenda na kuanza kutafuta jinsi ya kumla. Alivyoona lile jumba la kobe linamuingizia usiku kula kitoweo chake basi jamaa alimeza vyote kobe na jumba lake kwa pamoja. Na baada ya hapo nikakaa nione kama litapata madhara yoyote kwa kumeza lile jumba.

Aisee dakika hiyo hiyo mwamba katembea zake kwenda kutafuta windo lingine ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Unaona domo hilo. Huwa linapanuka muda wowote kulingana na ukubwa wa mnyama anaeliwa.
 

Attachments

  • Screenshot_20220812-181951.jpg
    37.1 KB · Views: 9
Ya na mimi nimeshaiona hiyo.
Afu eti mtu anakuja kuleta habari za nyoka koboko ambae anadhibitiwa hata na yule nguchiro anaeitwa mangoose.
Hili dubwasha linaweza kuwameza mangoose na koboko wake pamoja kwa muda wa dakika 3 tu aisee.

Huyo koboko hata kwa eagle sidhani kama atafanya kitu ๐Ÿ˜
 
hawezi kuwemo kwenye kundi la wababe wa mwituni, kwasababu hapambani, yeye hushambulia kwa kushtukiza na kutimua mbio (kujihami)Kisha baada ya muda ndio hufuatilia windo lake kwa tahadhari ya hali ya juu.
 
Ha
Niliwahi mkuta kichakani nikamkimbiza huku mkononi nimeshika ndala moja alitoka baru hadi akaingia shimoni
Labda kenge
 
Jama nshaangslia huyo mnyama kwenye national geographic. Kwa kifupi ni kenge. Ukubwa ni kutokan na maeneo
Sijui ka unaelewa nini maana ya neno jamii ya..au kwa hio tuseme chui ni paka tofauti ni ukubwa maumbo kutokana na walipo ..kwamba chui yuko porini na paka anazunguka kwenye ma bar huku? Au tuseme chui ni duma tofauti maumbo? NO ni jamii moja ila ni aina mbili tofauti

Kenge , mamba, komodo ni jamii ya mijusi hata wale caiman

Hivo huyo sio kenge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ