Komwe (frontal bossing): Sababu ni zipi? Ni njia zipi za kuzuia ili mtoto asiwe na komwe?

Komwe (frontal bossing): Sababu ni zipi? Ni njia zipi za kuzuia ili mtoto asiwe na komwe?

Nadhani ni maumbile yakurithi mara chache sana mtoto mdogo kuna namna yakumlaza na kumkanda kanda USO ili kutengeneza shape ya kichwa

Maumbile ya kurithi.

Mkuu, bora wewe umeongea sense. Genetic issue.
 
Kwa wenye uzoefu na malezi/uzazi...

Kila mzazi hutamani shape nzuri ya kichwa kwa watoto wake.

1. Je, ni kweli kuwa 'UTOSI' kufunga mapema sana husababisha komwe (forehead kuwa kubwa)?

2. Je, ni kweli kuwa 'CHANGO LA MTOTO' husababisha komwe?

3. Ni njia zipi (kienyeji au kitaalamu) zinasaidia kuzuia komwe kwa mtoto?

Nawasilisha.
Kiukweli wanawake wenye makomwe ni wazuri sana sasa sijajua kama ni mimi tu au la
 
Hivi kwani hilo komwe huwa ni tatizo,? Naonaga tu watu wakisema, ona komwe hilo ila sijawahi jua lina uzito mkubwa hivii.

Khaaaah jmn, komwe sio ugonjwa na halina tabu, tusifanye maisha kuwa magumu sana.
 
Kwani komwe ni ulemavu? Mbona mnapenda ku make big deal out of nothing?
Ni sawa uje kuuliza nini kimafanya mtu awe na kanyagio kubwa au pua kubwa au meno makubwa etc.
Kwan komwe lako linakupa changamoto gani on your daily activities hadi uje kufungulia uzi JF??
Hebu tufocus kwenye tangible issues.
Kabla ya kusoma comments, nilimshangaa mtoa mada..

Na comments nyingi, zimemshangaa pia
 
Kabla ya kusoma comments, nilimshangaa mtoa mada..

Na comments nyingi, zimemshangaa pia

Namimi nakushangaa vile vile.

Kuna makomwe ni 'too much' na huharibu muonekano na mtu.

Nadhani kunakuwa na kitu hakipo sawa (excessive in something, kitu kama hicho). Kama sio hormonal issue, basi ni defects kwenye ufungaji wa tosi za pande zote mwa kichwa. Ama genetic disorders.

Huko Developed countries, 'frontal bossing' ni medical issue kabisa. Ila Africa isn't an issue.

Ngoja wataalaamu waje watupe ABCs.
 
Kwa wenye uzoefu na malezi/uzazi...

Kila mzazi hutamani shape nzuri ya kichwa kwa watoto wake.

1. Je, ni kweli kuwa 'UTOSI' kufunga mapema sana husababisha komwe (forehead kuwa kubwa)?

2. Je, ni kweli kuwa 'CHANGO LA MTOTO' husababisha komwe?

3. Ni njia zipi (kienyeji au kitaalamu) zinasaidia kuzuia komwe kwa mtoto?

Nawasilisha.
Hii ni identity ya people za north. Ni moja ya tabia ya mwanadamu ya kurithi. Huwezi kilikombia wala kuliongeza. Hata hivyo komwe sio ulemavu, ni sawa na tulivyo na watu warefu ama wafupi.
 
Basi binti yangu nimelandisha komwe kama element ya pikipiki hila namuonea huruma mweeee

Pole sana mkuu.

Komwe likiwa 'too much' huyo binti yako kuolewa ni hadi atoe hongo ya mtaji Kwa mwanaume. Kidding mkuu 😂
 
Komwe ndiyo nini
Acha ujinga
Hakuna kitu kinaitwa komwe
Na kama kipo kila mtu analo
Huna hoja

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app

Kuna PAJI LA USO.
Kuna KOMWE.

N.B: Kila mwenye komwe ni lazima ana paji la uso. Ila sio kila mwenye paji la uso ana komwe.

So, relax mkuu na tuliza komwe hilo. Usipanic. Huu ni mjadala huru, sio vita ya mapanga na visu.😄
 
Nadhani kunakuwa na kitu hakipo sawa (excessive in something, kitu kama hicho). Kama sio hormonal issue, basi ni defects kwenye ufungaji wa tosi za pande zote mwa kichwa.

Developed countries ni medical issue kabisa.
Nenda basi kalipasue ulete balaa.
Mungu ndio ameshakuumba kamaliza.
 
Hii ni identity ya people za north. Ni moja ya tabia ya mwanadamu ya kurithi. Huwezi kilikombia wala kuliongeza. Hata hivyo komwe sio ulemavu, ni sawa na tulivyo na watu warefu ama wafupi.
Kuna wanaume wenye komwe??
 
Back
Top Bottom