Konde (Harmonize) acha kutumia "sembe" inakuharibia career yako ya muziki

Konde (Harmonize) acha kutumia "sembe" inakuharibia career yako ya muziki

Achana nao hao mashabiki maandazi..wasafi wameicheza game yao kwa akili nyingi sana always hawaruhusu damage kwenye brand yao.

Konde hii kwake sio kiki ni mtihani, kuna watu mpaka sasa awatomchukilia tena serious brand imechafuka kuna deals hatozipata kamwe.
Deals zipi
Usiishie njiani weka kila kitu hapa
Usiishie kusema tu hakuna deals atakazozipata.....humu sio insta
 
Nimeishia njiani kusoma

Nataka nikuulize swali ule uzalishaji wa ovyo wa mond sio long term effect kwenye kiki zake???

Punguza mahaba ilo ni moja tu kati ya mengi aliyofanya mondi juzi tu kamkana baba ake...ngoja niishie hapa
Uzalishaji hovyo ina uzito kuliko picha za ngono? Uzalishaji hovyo tangu lini ikawa kiki. Tofautisha kukana na kusema ukweli.
 
Nimeishia njiani kusoma

Nataka nikuulize swali ule uzalishaji wa ovyo wa mond sio long term effect kwenye kiki zake???

Punguza mahaba ilo ni moja tu kati ya mengi aliyofanya mondi juzi tu kamkana baba ake...ngoja niishie hapa
Hawajaliona hilooo!!ahsante
 
Kwa upande wangu vibaya, melody iko poa kuliko nyamaza ila vany kuandika na kuimba anamuacha mbali kondeboy hilo tuache unafki aisee.

Kwasababu kondeboi hubadilika kwenye nyimbo zake chache tofauti na mwenzie na hata idea za nyimbo vany ana idea nying tofauti tofauti. Jaribu tu kuskiza ngoma zao ambazo kila mtu kaimba peke yake.

WOTE NI WAKALI waache tu huu udwazi umeniboa kinoma

Naona nae ibra kaingilia katoa ngoma boko kishenzi huyi dogo nae bna
Harmonize mkali ila kwa rayvan bado unajua tukiacha unazi Ray van tatu Bora ya wasanii wazuri Tanzania hakosi.Diamond,Alikiba na rayvana ndio tatu bora .
Swengine tunampenda konde sababu ni Mmakonde chale😀😀😀😀😃mwenzao.
 
Harmo msanii mzuri Sanaa ila tatizo anashindana na watu ambao hawawezi hata afanye nini.
Ogopa Sana mtu anayekujua undani wako.
 
Kila jambo linataratibu zake msanii Harmonize asipobadilika anaelekea kujiharibia ktk tasnia yake ya muziki.

Wito kwa watu wake wakaribu wamshauri jinsi gani ya kutumia mitandao ya kijamii na jinsi gani ya kutengeneza kiki sababu kila uchwao anelekea kudrop katika fani, Harmo wa WCB sio huyu wa sasa kashfa nyingi,kazi hazina ubora ,michambo na mabifu na watu kila kukicha.

Tahadhari kwa sisi mashabiki wake tunaona mwisho mbaya kwake anatakiwa apate washauri na wasimamizi watakaomshauri na kumuelekeza nini afanye nini aache kulinda weledi wa tasnia yake.

Watanzania hawakawii kumchoka mtu mifano hai ipo mingi kwa wasanii wenzake, anatakiwa akumbuke alipotoka na aangalie alipo na anapokwenda.

Kikawaida katika nchi yenye kulinda tamaduni na ustaarabu ktk jamii kitendo cha kuonesha picha za utupu mitandaon ni cha fedhea kwa msanii mkubwa Kama yeye.

Kitendo cha kula kuku na mayai yake ni kudhalilisha wanawake na hakivumiliki, kitendo cha kutukana watangazaji na kuwapa vitisho kama alivyomfanyia Maimartha wa Jesse ni ulimbukeni na upungufu wamaarifa, kitendo cha kutengeneza lebo ya kusimamia wasanii halafu wasanii hao hawatoi nyimbo wala hawasikiki na wanavipaji ni kuua vipaji vya wasanii wetu.

Mimi shabiki namba moja wa Harmonize na nimechukizwa na mienendo yake, naomba abadilike bado tunampenda kushindana na WCB kutamuharibia wale watu hawawezekaniki wana nguvu na vipaji na washapiga hatua kubwa Sana .
Unaweza shangaa management inasapoti haya mambo....

Nchi ngumu hii ukifikiria sana utakonda bure kwa mawazo
 
Back
Top Bottom