Kongole Rais Uhuru Kenyatta kwa kuheshimu adhana

Kongole Rais Uhuru Kenyatta kwa kuheshimu adhana

Adhana maneno yake ni matum kwa kila dini. Tafsiri ya haraka ya maneno ya Adhana kwa kifupi sana
MUNGU NI MKUBWA MUNGU NI MKUBWA, NJOONI TUSALI NJOONI TUSALI(Ukiyaangalia maneno haya hayachugui dini)
Sote tunajua Mungu ni mkubwa hilo ni bayana kwa kila dini.
Njoo tusali/tuswali hapa ni njooni TUMUOMBE/TUMWABUDU MUNGU, hii kila mtu anaweza kuombwa kuja kumwabudu Mungu mmoja aliye muweza wa kila jambo
 
Inapo pigwa azana inatakiwa watu wote wanyamaze na waache kila wanacho kifanya kwaajili ya kusikiliza wito kwaajili ya ibada kwakua anaetajwa ni mwenyezi Mungu
Allah Akbar manaa yake ni Mungu mkubwa

Hivyo hata mafunzo ya kiislam yanaamrisha hivyo kuwa watu wanyamaze lakin hata waislam weng huwa hawafanyi hivyo , Kenyatta kunyamaza kwake kumetoa funzo kubwa hata kwa waislam wenyewe.
Kabisa
 
Wakati Mh Rais Uhuru Kenyetta anatoa hotuba yake kulikuwa na mwingiliano wa Adhana kutoka moja ya msikiti ulio karibu na uwanja ule. Cha kushangaza mara baada ya kusikia hivyo alilazimika kusubiri mpaka adhana ile iishe. Hii inaashiria nini wanabodi.? Au alitulia tu kwa huzuni yake.?
Uhuru ni chapombe lakini huwaga ni mmoja wa marais waungwana sana (distinguished gents) barani Africa.
 


Na kapicha kake ninaka-post
Funzo kubwa sana kwa viongozi wetu.
 
Mkuu unawaza kuwa kiongozi mzuri popote utakapochaguliwa coz hupendi unafiki, hongera sana
Mkuu shukrani sana ni matumizi ya common sense tuu, wapo watu wanaishi karibu na makanisa na kuna kengele za kanisa na wana vumilia kwasababu vyote vinatukumbusha kumcha Muumba wetu.

Religious tolerance ni kitu muhimu katika ustawi wa nchi yoyote.
 
Wakati Mh Rais Uhuru Kenyetta anatoa hotuba yake kulikuwa na mwingiliano wa Adhana kutoka moja ya msikiti ulio karibu na uwanja ule. Cha kushangaza mara baada ya kusikia hivyo alilazimika kusubiri mpaka adhana ile iishe. Hii inaashiria nini wanabodi? Au alitulia tu kwa huzuni yake?
Kwa kawaida adhana inapopigwa hakuna mtu anayeruhusiwa kuongea na na miiko hii rais uhuru anaijua vyema sana kwasababu kenya kuna waislam na wanajua miiko katika ardhi yao.Hivyo kila mtu anapaswa kuepuka kuharibu ibada za wengine.

Kiufupi yupo vizuri sana ndiyo maana uwanja mzima walimpigia makofi kwa kufanya vile.Hakika ni jembe huyu jamaa.Nasi tujifunze kuhusu hilo maana kuna wengine hatujui hilo badala yake kuleta vurugu kwamba adhana ni kelele.

Kwa hiyo amani upendo na mshikamano wa taifa huanza na vitu vidogo kama hivi.
 
Back
Top Bottom