Watu hawajamuamulia tu, in a full-scale war North Korea haidumu hata wiki.
Mkuu hata Merikani ilikuwa inamcheka sana Mfaransa kwamba inakuwaje unashindwa kuwafyekelea mbali WavietNam, kwa nini mnapigana nao vita miaka nenda rudi bila mafanikio.
Wamerika wakajitapa mbele ya wafaransa kwamba wana uwezo mkubwa wa kupigana na VietNam na kumaliza kazi ndani ya wiki mbili kwa pigo moja lenye nguvu na lililo nyooka,baadae Mfaransa ilishindwa kuendelea na vita huko VietNam akaondoa majeshi yake na kuyarudisha Ufaransa kwa aibu.
Wiki chache baada ya Ufaransa kujiondoa VietNam, Jeshi la Merikani wakajiingiza kichwa kichwa VietNam wakiwa na imani kwamba vita ingemalizika ndani ya miezi michache, sasa nini kilicho jitokeza wakati vita ilipo pamba moto - Amerika ilipoteza ndege za vita, bombers na helicopters zaidi ya 20,000(elfu ishirini) kwa kudunguliwa na nyingine kuharibiwa beyond repair kutokana na makombora ya Warusi aina ya S-75 ya kutungulia ndege, strella manpad, triple As', RPG-7 nk the loss was massive, American Military haikutegemea kwamba ingeweza kupoteza idadi kubwa ya Military flying machine, si hilo tu vile vile maelfu ya wanajeshi wa Merikani walipoteza maisha.
Mwishowe baada ya miaka takribani 12 ya mapigano baina ya WavietNam kasikazini na jeshi la Merikani WavietNam waliwazidi kete Wamerikani na wakawashinda na kuwatia aibu - majigambo ya Uncle SAM hayakufua dafu mbele ya Field Marshal Nguyen Thin Bin chini ya uongozi thabiti wa Uncle Ho Chin Min.
Ninacho taka kukumbusha hapa ni kwamba someni kwanza historia ya kweli kuhusu vita vilivyo wahi kupiganwa karne hii huko Mashariki ya mbali - ma orientals si binadamu wakuchukulia poa hata kidogo regardless ya economic status za baadhi ya mataifa hayo - haya mambo ya kusema eti Merikani inaweza kuisambalatisha Korea Kaskazini ndani ya wiki hizo ni ndoto za Mchana - kumbuka Korea Kaskazini iliwahi kupigana vita na USA na washirika wake kuanzia 1950-1953,je,unajuwa kulitokea nini baada ya kupigana kwa miaka minne - USA ilizidiwa nguvu na Korea Kaskazini USA ikaomba umoja wa mataifa kuingilia kati kusitisha vita - hiyo ilitokea miaka hiyo ya zamani, je,unafikiri hivi sasa Korea Kasikazini imejihami vipi kijeshi ili ku-contain ubabe wa USA. FYI North Korea isn't a walk over at all, ndio maana USA inamugwaya sana Kiduku inaishia kwenye Pilitical rhetoric bila ya kumchukulia hatua yoyote kijeshi.