Korea yaikopesha Tanzania Shilingi Bilioni 400 za kujenga Hospitali ya Rufaa Zanzibar

Wao hawajali kwa kuwa huo Mkopo unalipwa na utalipwa na Watanganyika ....!!

Imagine Afya si swala la Muungano ... sijui inakuwaje serikali ya Muungano inakopa kwenda kujenga Hospital Zanzibar. Kweli Wajinga ndiyo waliwao.
Zanzibar ni sehemu ya serikali ya muungano....
 
#HABARI: Serikali ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Korea zimesaini Mkataba wa Mkopo nafuu wa Shilingi bilioni 422.16 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni, Zanzibar.

Mkataba wa Mkopo huo umesaimiwa Jijini Soeul na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Mwamba, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na kwa upande wa Korea umesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji Mwandamizi na Mjumbe wa Bodi wa Benki ya Exim - Korea, Mr.Hwang Kiyeon.

Bofya hapa.-https://www.itv.co.tz/news/korea-yatoa-bilioni-422-ujenzi-wa-hospitali-ya-binguni
 

Attachments

  • FB_IMG_1717593037381.jpg
    58.1 KB · Views: 1
Mkopo wa kijinga hiyo hospitali ya Zanzibar itakosa wateja

Population ndogo sana wangeendelea tu kuja Muhimbili kama kukihitajika huduma za kibingwa kama ambavyo wamekuwa wakifanya miaka yote

Wangeimarisha tu huduma za hospital ya Mnazi mmoja Zanzibar

Mabilioni yote hayo kuwekeza Zanzibar ni mkopo usio na tija huo heri ungekopwa labda hata kukopesha wavuvi wanunue meli kubwa za uvuvi za kisasa ili.kushiriki kikamilifu uchumi wa Blue

Ujinga mtu serikali imefanya kulipa huo mkopo

Uswahili tu umetumika hapo kuwa bara Kuna hospital ya rufaa na chuo kikuu Cha afya Muhimbili Kwa hiyo na Zanzibar inabidi iwepo .Utoto na ujinga mtupu

Muda utaongea
 
Zanzibar tena? Atakayelipa mkopo ni URT au visiwa? Kama tulikuwa na serikali moja isngekuwa hivi ni suala la muda tu
Serikali moja ni sawa lakini tuanze na Mama aendelee kutawala mpaka 2035.
Yaani awamu yake ya kwanza itaanzia 2025 ,
Awamu hii ya sita ni awamu ya mpito tu
 
Kwani huduma za afya ni mambo ya Kimuungano?

Yaani tunakopa Tanzania Bara halafu Hospitali inaenda kujengwa Zanzibar?

Deni tunakuja kulipa Tanzania Bara πŸ™†

It's unfair aisee πŸ™Œ
Ni balaa aise
 
Na daraja la Tanganyika hadi Zanzibar linaendeleaje huko? πŸ™
 
Swala sio wao kushindwa kujenga Bali ukumbuke hospitali itajengwa Zanzibar na mkopo utalipwa kwa jasho la watanganyika kwa jina la Tanzania.
Tatizo ni pale ambapo Zenji hawaruhusiwi kukopa wenyewe bila Tanganyika.
Hawaruhusiwi ht kujiunga na jumuia za kimataifa bila bara kuridhia. Refer issue ya OIC. That's why wanakopa URT na ndio watakaolipa
 
Je afya ni swala la muungano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…